Kilimanjaro: Akamatwa kwa kutumia sare za JWTZ kuwatapeli watu

Kilimanjaro: Akamatwa kwa kutumia sare za JWTZ kuwatapeli watu

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1626092757082.png


Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikiliia Daniel Ruzinokwa kwa tuhuma za kukutwa na sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambazo amekuwa akizitumia kufanya udanganyifu na matukio ya uhalifu katika mikoa mbalimbali nchini.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema Ruzinokwa aliwahi kuwa askari wa JWTZ na baadaye kufukuzwa, lakini hakurudisha sare hizo.

Amesema mtuhumiwa huyo amekuwa akizitumia sare hizo kufanya utapeli wa fedha kwa kuwalaghai watu, na kuwaahidi atawapeleka mafunzo ya usalama wa Taifa nchini Israel.

Kamanda Maigwa amesema Jeshi la Polisi limefanya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kukuta akiwa na kombati za Jeshi, kofia za pama, kofia za chepeo, mikanda miwili ya Jeshi, koti la mvua na kitambulisho cha JWTZ, vyote vikiwa mali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

Mwananchi
 
[emoji23][emoji23][emoji23] hivi wanaona usalama wa Taifa Kuna maisha mazuri et?

Mshana Jr njoo ushauri vijana huku
Ni ile proud tu nipo usalama... Now days vijana wengi wana somjo zakuwa wao ni usalama na inaonekana iyo title ya usalama ndo inafanya wadanganywe.... Na jamaa atakuwa kaupiga mwingi sana strees maana vijana wanapenda iyo job

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi hii ni nzuri sana ukiwa unaitafuta au unaona mtu anafanya, ila.........
NAWAZA TU.
 
Bongo hii ukitoa wanasiasa wengine wote wanaungaunga.
Bora hata umesema kweli, Kama mwingine hapa ni jirani yangu kila siku namwazima chumvi na ni usalama wa Taifa 🤪🤪🤪🤪 hivi nyie vijana mna matatizo et!?
 
Ni ile proud tu nipo usalama... Now days vijana wengi wana somjo zakuwa wao ni usalama na inaonekana iyo title ya usalama ndo inafanya wadanganywe.... Na jamaa atakuwa kaupiga mwingi sana strees maana vijana wanapenda iyo job

Sent using Jamii Forums mobile app
Wajinga sana Hawa vijana wa Siku hizi njooni huku Lupembe tulime parachichi Aina ya Hasi
 
Nawashangaa Sana kila siku natafuta kazi usalama loooh poleni sana sio kazi ya kutamani hata kidogo, [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Usalama unatakiwa ufanye kazi za kujitolea kwa moyo, ni kama upadre. Sasa wabongo walafi wanaenda na lengo la maslahi tu, TISS ingekuwa kweli inafanya kazi za kitaifa watu mbona tungeshapiga hodi kwenye ofisi zao.
 
Nawashangaa Sana kila siku natafuta kazi usalama loooh poleni sana sio kazi ya kutamani hata kidogo, 😭😭😭😭😭
Hata nyie wanajeshi pia bado njaa inawasumbua pia, kwa ufupi tu vyombo vya ulinzi na usalama kwa bongo maslahi kidogo yapo huko TISS na TPDF ila kwengine tia maji tia maji.
 
Back
Top Bottom