tyc
JF-Expert Member
- Feb 25, 2014
- 1,179
- 2,971
Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Kindi Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro anadaiwa kumuua mama yake mzazi, Marietha Mushi (62) kwa kumnyonga na shuka, kisha kumpiga na kitu kizito kichwani na kumng’oa macho.
Habari zinaeleza kuwa mama huyo alikuwa na ulemavu wa mkono jambo linalodaiwa kuchangia ashindwe kujitetea wakati akishambuliwa na binti yake huyo.
Akizungumza na Mwananchi Digital Jumanne Julai 6, 2021 mkuu wa Wilaya ya Moshi, Said Mtanda amesema tukio hilo limetokea Julai 5, 2021 eneo la Kibosho Sambarai.
"Mtoto amemuua mama yake na mtoa taarifa ambaye ni kaka wa marehemu ameeleza kuwa alibaini kuuawa kwa dada yake kwa kunyongwa na shuka kisha kupigwa na kitu kizito kwenye paji la uso. Alisema aling’olewa macho na huyu mwanaye wa kike ambaye anasoma kidato cha nne,” amesema Mtanda.
Amesema mwanafunzi huyo amekamatwa na uchunguzi wa Polisi unaendelea
Source: Mwananchi Newspaper