Kilimanjaro: Diwani atoweka baada ya fumanizi

Madanda alisema diwani huyo alitoweka baada ya chama hicho kumdhamini kwa tuhuma za fumanizi la mke wa Katibu wa Siasa na Uenezi wa Kata ya Lundugai, Zebedayo Makalla na kuahidi kumlipa mwenye mke shilingi milioni 2.5 za ugoni.
Yaelekea mwenezi hakuwa anawajibika ipasavyo kwa mkewe
 
Na Gaudence Msuya, Hai

DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Lundugai wilayani hapa, Azizi Simbano anadaiwa kutoweka kwa kinachoelezwa kuwa ni kukimbia fumanizi la mke wa kiongozi wa chama hicho.

Aidha, CCM wilaya imetangaza msako dhidi ya diwani huyo aliyefumaniwa kwa nadhiri kwamba, apatikane asipatikane lazima hatua kali za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya tukio hilo lililothibitishwa pia na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Hai, Waguba Madanda, diwani huyo ametoweka na hata simu yake haipatikani.

Madanda alisema diwani huyo alitoweka baada ya chama hicho kumdhamini kwa tuhuma za fumanizi la mke wa Katibu wa Siasa na Uenezi wa Kata ya Lundugai, Zebedayo Makalla na kuahidi kumlipa mwenye mke shilingi milioni 2.5 za ugoni.

Alisema tangu atoe ahadi hiyo ni mwezi sasa hajaonekana na namba yake ya simu ikipigwa haipokelewi, hali inayoonesha kuwa amekimbia tuhuma hizo.

Madanda alisema wao kama chama wanaendelea na hatua stahiki baada ya zile za awali kukwama.

Makalla alikitaka chama hicho kuhakikisha diwani huyo analipa pesa zake ili akatafute mke mwingine kwa kuwa aliamua kumwachia tangu siku ya tukio, hivyo kwa kuwa chama kilibeba dhamana kwa kiongozi huyo, basi kisimamie haki itendeke.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Lundugai, Charles Kondema alisema matukio ya diwani huyo yamewachosha kwa kuwa, hana maadili mema na haitendei haki nafasi hiyo kwa matendo yake.

Gazetibla RAIAMWEMA Toleo la Jumanne Machi 29, 2022, Ukurasa wa 3
Kata inaitwa Rundugai Sio Lundugai punguza kipago.mzaramo
 
DIWANI KAACHIWA MKE WA MWENZAKE, KAAMUA KUKIMBIA!🤣
ALIYEIBIWA MKE NAYE ACHUKUE MKE WA DIWANI SASA.

KAZI NA IENDELEE
 
Huyo mwanamke asiye na maadili na kuchakatwa na wakuu wa chama chake ana hali gani kwa Sasa?
Je? Nikawaida yake kuwapa viongozi wake burudani au ni hiyo Mara moja tu?
 
Umemfumania mkeo halafu unampiga faini mgoni wako milioni 2.5, sasa kwanini usimuwekee mkeo bango usoni anauzwa kwa milioni 2.5 ili usisumbuane na watu?
 
Kwahio hili tukio polisi hawajaliona anasakwa na wanaCCM tu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Hakuna sehem mtoa mada kamnukuu OCD anamtafuta, zaidi ya mwenyekiti wa chama tu.

Eti "hatua kali za kinidhamu"??

Hio ni both criminal and disciplinary offence
 
Huyo jamaa ni tapeli na mshirikina mbobezi. Haha sifa za kuongoza kata yetu
 
Na Gaudence Msuya, Hai

DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Lundugai wilayani hapa, Azizi Simbano anadaiwa kutoweka kwa kinachoelezwa kuwa ni kukimbia fumanizi la mke wa kiongozi wa chama hicho.

Aidha, CCM wilaya imetangaza msako dhidi ya diwani huyo aliyefumaniwa kwa nadhiri kwamba, apatikane asipatikane lazima hatua kali za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya tukio hilo lililothibitishwa pia na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Hai, Waguba Madanda, diwani huyo ametoweka na hata simu yake haipatikani.

Madanda alisema diwani huyo alitoweka baada ya chama hicho kumdhamini kwa tuhuma za fumanizi la mke wa Katibu wa Siasa na Uenezi wa Kata ya Lundugai, Zebedayo Makalla na kuahidi kumlipa mwenye mke shilingi milioni 2.5 za ugoni.

Alisema tangu atoe ahadi hiyo ni mwezi sasa hajaonekana na namba yake ya simu ikipigwa haipokelewi, hali inayoonesha kuwa amekimbia tuhuma hizo.

Madanda alisema wao kama chama wanaendelea na hatua stahiki baada ya zile za awali kukwama.

Makalla alikitaka chama hicho kuhakikisha diwani huyo analipa pesa zake ili akatafute mke mwingine kwa kuwa aliamua kumwachia tangu siku ya tukio, hivyo kwa kuwa chama kilibeba dhamana kwa kiongozi huyo, basi kisimamie haki itendeke.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Lundugai, Charles Kondema alisema matukio ya diwani huyo yamewachosha kwa kuwa, hana maadili mema na haitendei haki nafasi hiyo kwa matendo yake.

Gazetibla RAIAMWEMA Toleo la Jumanne Machi 29, 2022, Ukurasa wa 3
Wameamuwa Walane wao kwa wao
 
haaaaa, nyie wapare si mngelipa huo ugoni.

Wengine washaamua kufanya wake zao vitega uchumi
 
Back
Top Bottom