Kilimanjaro: Mama adaiwa kumuua mwanae wa miaka mitatu kwa kumchapa fimbo

Kilimanjaro: Mama adaiwa kumuua mwanae wa miaka mitatu kwa kumchapa fimbo

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, linamshikilia mwanamke mwenye miaka 27, Mkazi wa Kibosho Kirima Juu, Wilaya ya Moshi kwa tuhuma za kumuua mwanae mwenye umri wa miaka mitatu na miezi sita kwa kumchapa na fimbo.

Akithibitisha hilo mbele ya waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, ACP Simon Maigwa amesema tukio hilo limetokea Jumapili Julai 31, 2022 majira ya saa moja asubuhi.

Kamanda Maigwa amesema Mama huyo alimchapa na fimbo mwanae katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku chanzo kikidaiwa kuwa mtoto huyo alifungulia bomba na kuchezea maji ya baridi yaliyokuwa yakitiririka.

" Baada ya kuona hali ya mwanae imezidi kuwa mbaya mama huyo alijaribu kutoroka ila wananchi walimdhibiti na Jeshi la Polisi tulifanikiwa kumchukia kwa taratibu za kisheria" Amesema Kamanda Maigwa.

Aidha Kamanda Maigwa ametoa wito kwa wazazi kutumia busara katika kuwaadhibu watoto wao pale wanapofanya kosa na sio kuchukua hatua kali hali inayopelekea kuhatarisha maisha.

"Kitendo cha kuchapa sio suluhisho kumfanya mtoto awe mtiifu, wazazi tumieni njia za busara, huyu mtoto alikuwa na miaka mitatu na miezi sita bado ni malaika haelewi chochote," amesisitiza Kamanda Maigwa.

Chanzo: Langola
hali si hali
 
Watu wengi wanazaa bila kupanga au kuwa tayari na haya ndio matokeo yake.
Inasikitisha sana.
Nilishagombana na dada mmoja vibaya mno kwa ajili hiyo, mtoto mdogo anapigwa kwa makosa madogo kisha akilia anapigwa tena, nikamtamkia kama mtoto amemshinda ampeleke vituo vya yatima tu.. alikuwa na stress za kuzalishwa na kuachwa pia
 
Inasikitisha sana

Ila pia mazingira hayaoneshi kama kulikuwa na dhamira ya kuua.
Kumchapa mtoto sehemu mbalimbali za mwili unasema hakuwa na dhamira ya kuua?

Ngoja tuletewe huyo mama huku kwenye mkono wa sheria tumnyooshe pumbav zake.

Mtoto asiye na hatia anakufa kisa kuchezea maji tu? Haiwezekani.
 
malezi ya singo parent yanashida siku zote, full stress.
 
Back
Top Bottom