PreGE2025 Kilimanjaro: Mbunge Esther Malleko atekeleza ahadi yake, akabidhi Mashine za kutotolesha vifaranga vya kuku

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
819
Reaction score
1,093
*UKOMBOZI WA KIUCHUMI NA AFYA MKOA WA KILIMANJARO
*
Mbunge Esther Malleko atekeleza ahadi yake,akabidhi Mashine za kutotolesha vifaranga vya kuku UWT Mkoa wa Kilimanjaro.

Na Mwandishi wetu.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Esther Malleko, ametimiza ahadi yake kwa wanawake wa mkoa huo, kwakuwakabidhi mashine 169 za kutotolesha vifaranga vya kuku (incubators) kwa kata 169 za Mkoa wa Kilimanjaro, zenye thamani ya Shilingi milioni 84.5.(84,500,000)
IMG-20250414-WA0076.jpg

Hafla ya kukabidhi mashine hizo imefanyika jana aprili 13,2025, ambapo pia ameahidi kuwapatia mitaji ya Mayai kwaajili ya kuanza mradi huo,pamoja na kuwapelekea watalamu kwenye kata ili kuwafundisha matumizi sahihi ya mashine hizo pamoja na ufugaji bora wa kuku na utunzaji wa fedha ili kuhakikisha mradi huo unaleta tija.

Amesema ametoa mashine hizo, ambapo ni sehemu ya hadi aliyotoa kwa lengo la kukuza uchumi wa wanawake kwenye kata na matawi ,kwa lengo la kukuza uchumi,lishe pamoja na kuwaunganisha wanawake wote kwenye kata na hata kuondokana na mikopo ya kausha damu ambayo imekuwa ni chanzo cha migogoro kwenye familia nyingi na kuwàrudisha nyuma wanawake wengi kimaendeleo.

"Wanawake wa Kilimanjaro mlinikopesha imani ninawalipa imani, leo nimekuja kutekeleza ahadi kwa kuwakabidhi rasmi mashine hizi (Incubators) ambazo mtazitumia kupitia vikundi vyenu na kunyanyuka kiuchumi," amesema Malleko.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Incubator hizi 169 zimegharamu kiasi cha sh.milioni 84.5 (84,500,000)," ameongeza.

Aidha, amepongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,kwa kuupatia Mkoa wa Kilimanjaro trilioni 1.2 katika kipindi chake cha uongozi, amewatua wanawake ndoo kichwani kwa mradi mkubwa wa maji Same Mwanga Kilimanjaro,amejenga hospitali,vituo vya afya na zahanati,amejenga madarasa,barabara na kuboresha utalii katika kipindi chake cha miaka minne katika mkoa huo.

"Sisi Wanawake wa Kilimanjaro hatuna deni na Rais Dk.Samia Suluhu Hassani,tunaahidi kumpigia kura nyingi apate ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi 2025," amesema Malleko

Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Kilimanjaro Ndg.Mercy Mollel, amepongeza Mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi yake kwa wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro, na kuwasihi kwamba Mashine hizo wazitunze ili ziwanufaishe kuwakwamua kiuchumi wapate nguvu na hamasa ya kwenda kuzitafuta kura za CCM.

Na baadhi ya wanawake hao, wamempongeza Mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi yake, na kwamba mashine hizo sasa zinakwenda kuwainua kiuchumi,kujenga afya ya familia na kuwaunganisha wanawake.
 
Wakati wa kupiga picha na kujikomba kwa wapiga kura ndiyo huu. Kwa sasa hata maji machafu mtakunywa na wapiga kura wenu. Lakini mkichaguliwa tu shwaaa hamuonekani. Mko bungeni huko kusinzia tu na kugonga meza kishabiki huku mkigawana posho. Useless politicians! 🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮
 
Muda wa kuhadaa wapiga kura wajinga. Tena usishangae hizo mashine ni zake, bali kawachukua washikaji zake kawapa kitimoto na bia wapige nazo picha ili kusaka kiki za hadaa.
 
"Sisi Wanawake wa Kilimanjaro hatuna deni na Rais Dk.Samia Suluhu Hassani,tunaahidi kumpigia kura nyingi apate ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi 2025," amesema Malleko.
Mama atashindana na nani? Hashimu Rungwe? Prof. Lipumba? Momose Cheyo? Kwa nini asipate ushindi wa kishindo?

Acheni kupotezea watu muda. Ingekuwa ni mimi Mama angetangazwa tu na mabilioni yote yaliyopangwa kuteketea kwenye uchaguzi feki wa rais yangeelekezwa kwenye shughuli zingine za kimaendeleo japo hata huko nako pengine yataishia kuibwa tu na wajanja 🚮🚮🚮
 
*UKOMBOZI WA KIUCHUMI NA AFYA MKOA WA KILIMANJARO
*
Mbunge Esther Malleko atekeleza ahadi yake,akabidhi Mashine za kutotolesha vifaranga vya kuku UWT Mkoa wa Kilimanjaro.

Na Mwandishi wetu.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Esther Malleko, ametimiza ahadi yake kwa wanawake wa mkoa huo, kwakuwakabidhi mashine 169 za kutotolesha vifaranga vya kuku (incubators) kwa kata 169 za Mkoa wa Kilimanjaro, zenye thamani ya Shilingi milioni 84.5.(84,500,000)
View attachment 3304364
Hafla ya kukabidhi mashine hizo imefanyika jana aprili 13,2025, ambapo pia ameahidi kuwapatia mitaji ya Mayai kwaajili ya kuanza mradi huo,pamoja na kuwapelekea watalamu kwenye kata ili kuwafundisha matumizi sahihi ya mashine hizo pamoja na ufugaji bora wa kuku na utunzaji wa fedha ili kuhakikisha mradi huo unaleta tija.

Amesema ametoa mashine hizo, ambapo ni sehemu ya hadi aliyotoa kwa lengo la kukuza uchumi wa wanawake kwenye kata na matawi ,kwa lengo la kukuza uchumi,lishe pamoja na kuwaunganisha wanawake wote kwenye kata na hata kuondokana na mikopo ya kausha damu ambayo imekuwa ni chanzo cha migogoro kwenye familia nyingi na kuwàrudisha nyuma wanawake wengi kimaendeleo.

"Wanawake wa Kilimanjaro mlinikopesha imani ninawalipa imani, leo nimekuja kutekeleza ahadi kwa kuwakabidhi rasmi mashine hizi (Incubators) ambazo mtazitumia kupitia vikundi vyenu na kunyanyuka kiuchumi," amesema Malleko.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Incubator hizi 169 zimegharamu kiasi cha sh.milioni 84.5 (84,500,000)," ameongeza.

Aidha, amepongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,kwa kuupatia Mkoa wa Kilimanjaro trilioni 1.2 katika kipindi chake cha uongozi, amewatua wanawake ndoo kichwani kwa mradi mkubwa wa maji Same Mwanga Kilimanjaro,amejenga hospitali,vituo vya afya na zahanati,amejenga madarasa,barabara na kuboresha utalii katika kipindi chake cha miaka minne katika mkoa huo.

"Sisi Wanawake wa Kilimanjaro hatuna deni na Rais Dk.Samia Suluhu Hassani,tunaahidi kumpigia kura nyingi apate ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi 2025," amesema Malleko

Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Kilimanjaro Ndg.Mercy Mollel, amepongeza Mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi yake kwa wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro, na kuwasihi kwamba Mashine hizo wazitunze ili ziwanufaishe kuwakwamua kiuchumi wapate nguvu na hamasa ya kwenda kuzitafuta kura za CCM.

Na baadhi ya wanawake hao, wamempongeza Mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi yake, na kwamba mashine hizo sasa zinakwenda kuwainua kiuchumi,kujenga afya ya familia na kuwaunganisha wanawake.
View attachment 3304398

View: https://x.com/Jambotv_/status/1937125622976831668?t=6I6OO1Cukd_EqJ7fiDUXJg&s=19
 
Back
Top Bottom