Beira Boy
JF-Expert Member
- Aug 7, 2016
- 25,050
- 45,202
Amani iwe nanyi watumishi wa MUNGU katika KRISTO YESU mtakatifu sana
Tukio hilo limetokea Kilimanjaro
Inauma sana dunia tulikofika kwa sasa
Kilimanjaro imekuwa mbaya Zaid ya Geita na Tabora kwa matukio ya kikatili
===============
Mtoto Ivan Innocent Chuwa mwenye umri wa miaka mitatu na nusu, anadaiwa kuuawa kwa kukatwa shingo na kijana jirani yao, kwa madai ya imani za kishirikina.
Tukio hilo ambalo limetokea Ijumaa Agosti 15, 2025, saa 10:00 jioni, wakati mtoto huyo akicheza kwa jirani, limezua simanzi na taharuki kwa wakazi wa eneo hilo, wazazi na majirani wakieleza kuwa ni tukio lililowasikitisha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Killmanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika kijiji cha Manushi Ndoo Wilaya ya Moshi na kueleza kuwa wanawashikilia watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya mtoto huyo.
Dada wa mtuhumiwa huyo, Mary Kiria, amesema siku ya tukio walikuwa nyumbani pamoja na mtuhumiwa na mtoto huyo wa jirani (marehemu).
Ameeleza kuwa alimuacha mtoto huyo akicheza na mwanaye mdogo huku akila chakula na yeye kwenda kwa jirani kuchukua pilipili kwa ajili ya chakula na mdogo wake huyo akiwa amekaa nje.
Mama wa mtoto, Lucy Chuwa amesema siku ya tukio mwanaye huyo alimuomba aende kwa jirani kucheza na mtoto na yeye akampeleka na kumuacha na dada wa mtuhumiwa kisha yeye kurudi dukani.
Baba wa mtoto huyo Innocent Chuwa, ambaye wakati wa tukio alikuwa akifanya shughuli zake za bodaboda, amesema alipigiwa simu na kuelezwa kuhusu kifo cha mwanaye.