Kilimanjaro: Raia wa Sweden ahofiwa kuwa na CoronaVirus sampuli zake zatumwa maabara Jijini Dar

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amesema kuna mgonjwa mwenye dalili za maambukizi ya virusi vya corona ambaye amelazwa kwenye wodi maalumu katika hospitali ya Mawenzi mjini Moshi na tayari sampuli zake zimechukuliwa kwa uchunguzi zaidi.

Mama Mghwira amesema Mgonjwa huyo ni raia wa Sweden aliyeolewa na Mtanzania na alisafiri kwenda kwao likizo na wakati anarudi alipotia Marekani kwa siku 14

Haijajulikana ameambikizwa akiwa wapi kama ni Marekani au ni Sweden lakini aligundulika alipofika katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
 
Huku ndio kichaka cha kukimbilia wasipokuwa makini nakuchukua hatua stahiki za kufunga mipaka,kama mataifa mengine tutaangamia.
 
Tarehe 15 mwezi Feb Italy walikuwa na wagonjwa 3 wa Corona, leo wana wagonjwa 46,638.

Corona_Italy.jpg
 
Tarehe 15 mwezi Feb Italy walikuwa na wagonjwa 3 wa Corona, leo wana wagonjwa 46,638.

View attachment 1397031
Tatizo la nchi kama Italy na Japan ni ‘High life expectancy’, kukuta watu wa maika 70,80 na 90 ni Jambo la kawaida kwenye nchi zilizoendelea, hivyo wengi wa wanaoumwa hufa maana Corona huuwa wazee zaidi..
 
Ila si tumeshatoa amri ya Karantini siku 14 kwa gharama zake mwenyewe msafiri, awe na dalili au asiwe nazo?
Hatua nzuri, lakini bado naona wauguzi na madaktari watakao wahudumia watu waliokutwa na ugonjwa huko karantini wanakuwa na hatari zaidi ya kuambukizwa.
Pia huduma tulizotakiwa kuwapatia wagonjwa wetu wa ndani tutaanza kuzigawa na kwa hawa tunao waruhusu sasa kuja kukaa karantini nchini kwetu.

Hatuwezi kuwaacha waugue na kufa kama kuku, mzigo unakuja kwa serikali yetu.
 
Tumeshasema ni kwa gharama zake mwenyewe, so kabla hujasafiri kuja Tanzania utahakikishie kwamba una pesa za kutosha kwenye akaunti za kukutunza kwa siku 14, huna usije Tz.
 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amesema kuna mgonjwa mwenye dalili za maambukizi ya virusi vya corona ambaye amelazwa kwenye wodi maalumu katika hospitali ya Mawenzi mjini Moshi na tayari sampuli zake zimechukuliwa kwa uchunguzi zaidi.

Mama Mghwira amesema Mgonjwa huyo ni raia wa Sweden aliyeolewa na Mtanzania na alisafiri kwenda kwao likizo na wakati anarudi alipotia Marekani kwa siku 14

Haijajulikana ameambikizwa akiwa wapi kama ni Marekani au ni Sweden lakini aligundulika alipofika katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
Hivi hawa wapuuzi (wazungu) wanalanda kwetu kutafuta nini kwanini wasikae kwao watulie... [emoji20][emoji20][emoji20][emoji20]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la nchi kama Italy na Japan ni ‘High life expectancy’, kukuta watu wa maika 70,80 na 90 ni Jambo la kawaida kwenye nchi zilizoendelea, hivyo wengi wa wanaoumwa hufa maana Corona huuwa wazee zaidi..
Umeitaja Japani. Lakini japan wala hali siyo mbaya hivyo kama unavyotuaminisha na ndio inaongoza kuwa na wazee wengi...
 
Back
Top Bottom