Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Timu ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) imefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu miaka zaidi ya 30 na hatimaye kufikia tamati.
Hayo yalijiri Februari 8,2025 baada ya timu hiyo kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu, taarifa ya utendaji kazi ya Huduma ya Msaada wa Kisheria bure kupitia “Mama Samia Legal Aid Campaign”.
Akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Wakili wa Kujitegemea kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dk. Belinda Chepchumba, alisema kupitia kampeni hiyo waliweza kutatua migogoro miwili ya ardhi Kata ya Mabogini Wilaya ya Moshi Vijijini ambayo imedumu kwa miaka mingi.
“Kupitia kampeni hii ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) tuliweza kufika Kata ya Mabogini iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini na tumeweza kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka zaidi ya 30, lakini pia tumetatua mgogoro mwingine wa ardhi uliodumu kwa miaka minne.”alisema Dk. Chepchumba.
Aidha Dk. Chepchumba ambaye pia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule ya Sheria, alisema kupitia kampeni hiyo waliweza kuzifikia Kata 10 na Vijiji 30 zilizoko Halmashauri hiyo na kufanikiwa kutatua migogoro 105.
“Migogoro ambayo ilijitokeza kwa wingi ni migogoro ya ardhi, ukatili wa kjinsia pamoja na masuala ya ndoa, ipo migogoro ambayo tuliweza kuitatua lakini pia kuna migogoro ambayo hatukuweza kuitatua hivyo itaendelea kutatuliwa na Wanasheria wetu wa TLS kwa kusikilizwa na kuhudumiwa bure kabisa.”alisema.
Source: Millard Ayo