Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Wakulima Katika baadhi ya Vijiji Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro wamedai kupata hasara kubwa kutokana na uharibifu mkubwa uliotokea katika mazao yao baada ya wanyama aina ya Tumbili kuvamia mashamba yao na kula mazao mbalimbali shambani.
Baadhi ya mazao ambayo yameshambuliwa ni kwa kiasi kikubwa ni pamoja na ndizi, mahindi, maharage na kahawa zilizoiva.
Wananchi wa Vijiji vya Usari na Orori wanasema Mwaka 2023 walichangishwa kiasi cha Shilingi 1,000 na kuupa Uongozi wa Kijiji kwa ajili ya kuwapa Watu maalum watakakofukuza tumbili hao lakini hadi sasa hawajui pesa hizo zilipoenda.
Hata hivyo, idadi ya Tumbili hao imekuwa ikiongezeka siku hadi siku kutokana na kuzaliana kwa wingi.
Wanakijiji hao wanadai kuwa ni muda mrefu wameomba Wizara ya Maliasili waende wakasaidie kufukuza Tumbili hao lakini hadi sasa hawajapata mrejesho wowote, kwa kuwa wamekuwa wakisisitizwa kutowaua Tumbili kwa maelezo kuwa ni maliasili ya Taifa.