Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Baadhi ya walimu wa shule ya msingi waliohamishwa katika shule mbali mbali katika wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wamesikitishwa na kauli iliyotolewa na Afisa elimu wa wilaya hiyo kuwa hata mahari yenyewe hawajamalizaga kulipa kwa hiyo hata malipo yao watalipwa kidogo kidogo.
Walimu hao wamesikitishwa na kauli hiyo kutoka Afisa elimu huyo ambae ni mwanamke na kuona kuwa wamedhalilishwa na kufehedheshwa kwani maswala yao binafsi hayahusiani na madai ya haki zao ama ajira zao bali wanachohitaji ni stahiki zao za malipo ambapo hadi sasa wamelipwa robo ya malipo yao.
Walimu hao wanadai tangu wapate uhamisho mwezi wa pili mwaka 2024 hadi leo pesa waliyolipwa ni robo tu ya pesa wanazodai.