Kilimanjaro yafanya vizuri kielimu,Kigoma Singida wafanya vibaya

Makupa

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
6,822
Reaction score
4,034
Mkoa wa Kilimanjaro umekuwa kinara wa kuboresha elimu ya msingi kwa kupata wastani wa asilimia 82 sawa na daraja A wakati mikoa ya singida na kigoma wakifanya vibaya.Kilim kwa kufelisha zaidi ya asilimia 44 kwa mkoa wa singida na asilimia 66 kwa mkoa wa kigoma.Kilimanjaro inafanya vizuri katika mazingira yote ya kielimu ,mbali na ufaulu hali ya miundo mbinu pia ni nzuri na mkoa umevuka viwango karibu vyote saba vya mazingira ya kufundishia na kujifunza.

Chanzo : Uchambuzi wa Sera Haki elimu
 
Singida mtoto wa kike akifikia miaka 8 anawaza kuolewa na hawaoni umuhimu wa shule kule. Kigoma ukimwondoa Zitto, ni majanga matupu. Shule ya wanafunzi 200, ukienda utakuta 18 wengine wote wako mashambani, kuroga, ama wanabishana vijiweni kuwa Diamond ndiyo rais wa Tanzania.
 

hongera kilimanjaro, sababu ni tamaduni ya watu wa kilimanjaro kuwa na kipaumbele cha elimu kwa watoto...
 
Sio kwamba mikoa mingine haiwezekani! La hasha. Kuna jambo wanashindwa kulielewa. Nendeni kilimanjaro mkajifunze kutoka kwao. Hawategemei pesa ya serikali kujenga miundo mbinu ya shule. Wanajitolea wenyewe kifedha, nguvu kazi na kufadhiliana wenyewe kwa wenyewe. Wazazi wanasukumana na watoto wao kwenda shule. Waalimu wameyapenda mazingira ya kilimanjaro ambayo ni ya ukarim u. Kwa ujumla WANAJITUMA.
 

Waliing'amua ccm kuwa haitawafikisha popote wakaachana nayo.
 
Waliing'amua ccm kuwa haitawafikisha popote wakaachana nayo.

kuhusu ccm c kweli kwan mkoa wa kilimanjaro una majimbo nane ya uchaguz na ni majimbo 3 ndo yako chn ya chadema! (upinzan) sasa. so maendeleo ye2 ni jitihada 2 binafc na c vyama vya siasa
 
kuhusu ccm c kweli
kwan mkoa wa kilimanjaro una majimbo nane ya uchaguz na ni majimbo 3 ndo
yako chn ya chadema! (upinzan) sasa. so maendeleo ye2 ni jitihada 2
binafc na c vyama vya siasa

moshi mjini(chadema), moshi vijijin(ccm), rombo(chadema), same(ccm), vunjo(TLP), hai (chadema), siha(ccm)
 
Ewe Nyepesi pigania maendeleo ya elimu mkoani kwako kwanza usipende kila siku kuabudiwa kwa elimu yako hiyo.Mwambie "uliyemkumba" akakufuata pia mkoani kwake asijione ana akili sana kama hajawasaidia watu wake waamke kielimu wawe kama yeye.Aache majungu kwani yeye ni mwalimu.Mwisho msije mkatudanganya tena eti hayo maendeleo ya Kili ni kwa sababu ya ukanda wa CHADEMA!Kuna kazi ya kufikiri kabla ya kuja na masuluhisho rahisi rahisi.Mabadiliko huanza katika fikra.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

Pokea "like" Mkuu. Tatizo linaanzia hapa hapa kwenye uzi. Cheki pumba za wachangiaji wengine wanavyokimbilia kutabanaisha sababu kwa ushabiki uliopauka wa Vyama vya Siasa! Pathetic!
 

Nenda mbali zaidi zivunje vunje pia katika wilaya tuone ufaulu.
Mazingira ya ubora wa elimu kwa mkoa wa kilimanjaro yalitayarishwa hata kabla ya uhuru.(kncu). Hata Kagera mazingira yalikuwa mazuri ukiacha hivi sasa ugonjwa wa ukimwi uliathiri maendeleo ya elimu kwa kuacha yatima wengi.
Kigoma ni suala la kihistoria ongeza rukwa .lindi na mtwara na singida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…