Kilimanjaro

kedekede

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
5,313
Reaction score
7,714
Wanajf heri ya krismasi wale wenzetu.Nawakilisha.Juzi tarehe 20/12/17 nilikuwa nasafiri kutoka Dar kuja Arusha,mbali na usumbufu wa kupata ticket na changamoto nyingine nyingi za safari kuna kitu niligundua.Mimi ninaposafiri kuja kaskazini nikitokea Dar au nikitokea Kaskazini kwenda Dar huwa mara zote napenda usafiri ule wa Neema Za Mungu(Dar express),Ukiona nimesafiri na usafiri mwingine labda nimepata Lift au Nimekosa Ticket.Kama ilivyo ada ya huu mwezi wenzetu huwa hawakai Daresalaam utafikiri Yesu alizaliwa kijijini kwao.Juzi nimebahatika kuwaona pale shekilango wamejazana wanasubiria mabasi ya Rombo,yalikuwa nadhani matatu,nikaona ya Arusha mengi wamejaa wao,na hata lile la Karatu nililopanda mimi lilijaa wao wao isipokuwa wachache kama mimi.Nikiwa pale nilikuwa naona toothpick zimewekwa kwenye bilinganya na hapa kifuani pamejaa matikiti maji yale makuuubwa.Wenzetu vipi,kulikuwa na flat screen kibao pale shekilango lakini zimeegeshwa kwaenye Vijiti vya Kuchomekea nyama za mishkaki.Isitoshe hapa vifuanai pamejaa.Wenzetu vipi kuna mapungufu gani ya lishe kwenye mionekano Hii?povu Ruksa.Mshana hawa watani na jirani zako vipi?
 
Kiki kwa baiskeli..

ngoja waje kukujibu,japo kwa sasa network za kaskazini zimezidiwa kwa idadi ya Wateja wengi
 
Kati ya Mimi na wewe kuna mmoja wetu amevuta bangi,
Ila si mimi
 
Nilichokigundua ni kuwa;
Kuna wengine hudharau vingine kwa sababu ni vya gharama sana kupatikana, japo nakitaamani lakini, sikitaki!! Hivyo vifaa ulivyoviona vyote hakuna kinacholala peke yake hata siku moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…