kedekede
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 5,313
- 7,714
Wanajf heri ya krismasi wale wenzetu.Nawakilisha.Juzi tarehe 20/12/17 nilikuwa nasafiri kutoka Dar kuja Arusha,mbali na usumbufu wa kupata ticket na changamoto nyingine nyingi za safari kuna kitu niligundua.Mimi ninaposafiri kuja kaskazini nikitokea Dar au nikitokea Kaskazini kwenda Dar huwa mara zote napenda usafiri ule wa Neema Za Mungu(Dar express),Ukiona nimesafiri na usafiri mwingine labda nimepata Lift au Nimekosa Ticket.Kama ilivyo ada ya huu mwezi wenzetu huwa hawakai Daresalaam utafikiri Yesu alizaliwa kijijini kwao.Juzi nimebahatika kuwaona pale shekilango wamejazana wanasubiria mabasi ya Rombo,yalikuwa nadhani matatu,nikaona ya Arusha mengi wamejaa wao,na hata lile la Karatu nililopanda mimi lilijaa wao wao isipokuwa wachache kama mimi.Nikiwa pale nilikuwa naona toothpick zimewekwa kwenye bilinganya na hapa kifuani pamejaa matikiti maji yale makuuubwa.Wenzetu vipi,kulikuwa na flat screen kibao pale shekilango lakini zimeegeshwa kwaenye Vijiti vya Kuchomekea nyama za mishkaki.Isitoshe hapa vifuanai pamejaa.Wenzetu vipi kuna mapungufu gani ya lishe kwenye mionekano Hii?povu Ruksa.Mshana hawa watani na jirani zako vipi?