Kilimo as solution to unemployment

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,136
Reaction score
32,268
Hello JF,

Katika threads zangu za nyuma,niliuliza mtu aliyeishia standard seven ama form four anaweza kufanya shughuli gani ya kipato

Jibu ambalo lilikua common ni Kilimo na kazi za vibarua….

Sijajua status ya Viwanda viko vingapi ..na walio tayari kufanya kazi hizi ni wangapi…pia Kilimo status yake

However ,

nimefikiria hili kundi la wanaofeli la saba na form four ni kubwa sana,wazazi wengi hawawezi ku afford shule private...

Na pia japo Elimu ni bure,bado kuna kundi kubwa ambao hawana elimu….

Ukumbuke hawa ni VIJANA (18-24)...tunapoteza nguvu zao ..

Nguvu ambazo zingekua invested zingetuletea matokeo chanya…

Ningependa kuishauri serikali yetu kuandaa initiatives/incetives za kilimo zinazo target this specific group..

Assume umempatia elimu kuhusu kilimo au na pia kumsaidia shamba huyu kijana...

Kwa kipindi cha miaka kumi (10) atakua amefikisha miaka 28-34,probably kaajiri watu kadhaa kwenye shamba lake...Sio tu ameongeza uzalishaji na kupunguza u dependency bali pia kuwa na CONFIDENCE ..as watu wengi kwenye kwenye 30's hawana furaha na kujiamini..ndio muda wengi wanaanza kujilaumu labda amefanya wrong career choice.

nimeweka Klimo kama solution,as nimeona mahali Kilimo kinacontribute to GDP 28.3% na hapo we haven't utilize our arable land properly(only 33 percent of 44 millions hectares is used)....

Tusiwaige nchi zilizoendelea walivyojikomboa kiuchumi,

Lets use what we have to go to the next level...

Kama wao wanatumia Tecnology sisi tutatumia Kilimo...

AU vipi????😁😁😁

Nakaribisha maoni


.
 
Hawa vijana hawajaandaliwa kwa maisha ya kuzalisha kupitia kilimo. Hawana elimu ya ukulima bora, hawana vifaa vya kufanyia kazi. Hivi kijana aliyezaliwa 2000 tunategemea azalishe kwa kutumia jembe la mkono?

Mazao hayana soko la uhakika. Msimu uliopita mbaazi ziliozea mashambani.
 
Sijui unaongea nini wewe!

1.Wanaofeli la saba na form four wawezeshwe wasikae idle.

2.Vijengwe vyuo vingi vya KILIMO

3.Tuna arable land kubwa haijawa fully utilized.

4.Kutoa mashamba na elimu ya kilimo kwa vijana 18-24

5.Litapunguza tatizo la ajira as most of vijana watakua busy na mashamba.if not creating job for themselves basi itakua for others.

6.Vijana watakua na confidence of having income. Unlike now watu wamesoma mpaka elimu ya juu na hawana confidence juu ya kipato and are frustrated of wasting all those years on education.

7.Kama nchi nyingine walipata maendeleo kwingine basi sisi tufanye mabadiliko ya Kilimo.

Mwisho ndio hii mkuu...kama hunielewi tuonane jumatatu lol
 
Kama hujatengeneza soko la uhakika la mazao hujamaliza tatizo.

Ningependekeza kila shule ya msingi kuwa na shamba la mfano na afisa kilimo akishirikiana na walimu, apange ratiba ya kufundisha vijana
 

Nilikua namaanisha kuwezeshwa ni kupewa Elimu pamoja na Mashamba..

Ilikuwa nije na topic nyingine ya jinsi ya kuwawezesha..

nilichotaka ku advise hivi vyuo vya kilimo vikianzishwa vianzishwe kwa kuzingatia mazingira yetu pekee..

mambo ya kukariri hapana...

.na lugha ya kufundishia iwe ya Kiswahili..sababu nimeona kuna barrier kwenye Elimu yetu sababu ya lugha.

nilichotaka pia ni kuona progression mtu anasoma kidogo kidogo hadi anafikia ngazi ya Chuo kikuu kama SUA .....anapata Degree yake...

hao waliozaliwa 2,000 na bahati mbaya wakafeli,wakionyeshwa alternative ya kuprogress katika Maisha yao..Im sure watafanya vyema tuu
 
Kama hujatengeneza soko la uhakika la mazao hujamaliza tatizo.

Ningependekeza kila shule ya msingi kuwa na shamba la mfano na afisa kilimo akishirikiana na walimu, apange ratiba ya kufundisha vijana

Nimependa wazo lako..

Dada mkubwa,nikisema Serikali iinvest namaanisha serikali itoe full commitment kwenye kilimo,,hii ni pamoja na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi....

Yote yanawezekana
 
ndiyo kinaweza kuwa mkombozi wa ajira. pamoja na uliyosema pia serikali inatakiwa kuhakikisha kilimo kinalipa, mtu akilima asiporwe mazao yake kwa kufunga mipaka au kwa kodi kandamizi. Pia tuwekeze kilimo cha umwagiliaji. Tanzania ni moja ya nchi chache zenye surface freshwater kwa wingi, fikiriaa hili, ziwa tanganyika lina 20
% ya maji hayo duniani,na nusu hiyo au 10% ipo Tanzania, bado maziwa mengine na mito. Tuna maji mengi sana. Mi naamini tukikamilisha haya kilimo kitakuwa ajira ya maana sana.
 

Wataalamu wa kilimo tunao lakini hawatumiki kwa ipasavyo. Fikiria kama kila kata ingekua na nyumba yenye basic needs na wanafunzi wa SUA kufanya field ya miezi mitatu kila mwaka kwenye kata na kuwatumikia walipa kodi wanaochangia elimu yao ingekuwa jambo lenye kheri.
 
Ruzuku pia husaidia wakulima wakati wa hali mbaya ya hewa. Ruzuku kwa wakulima huwa inawafikia kama ipo?
 

Asante mkuu i hope serikali itaamka sas na kuona Gap ambalo likiwa utilized fully tutasonga mbele kama taifa...

Pia ni vizuri umemention serikali ijali maslahi ya wakulima sio kuwa bully na kuwanyima ruzuku...

Magufuli tuna hamu na maendeleo..ume invest kwenye ndege sasa invest on people....LOL
 

Lenye kheri sana mkuu..,,asante kwa mawazo yako mazuri
 
Kama hujatengeneza soko la uhakika la mazao hujamaliza tatizo.

Ningependekeza kila shule ya msingi kuwa na shamba la mfano na afisa kilimo akishirikiana na walimu, apange ratiba ya kufundisha vijana
Uhakika wa soko na bei ndiyo kitu cha kwanza. leo waambie watu Congo gunia la mahindi ni 100,000. lima kauze! utaona watu wanalimia hadi mikono. Wauza karanga au wale wanazungusha mashati wawili hutawaona. hili linaongeza uzalishaji na si kuleta njaa kama tunavyoaminishwa.
 
Lazima serikali iweke mazingira ya kukifanya kilimo kiwavutie vijana, ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko kwa ajili ya mazao watakayozalisha
 
Lazima serikali iweke mazingira ya kukifanya kilimo kiwavutie vijana, ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko kwa ajili ya mazao watakayozalisha

Uko sahihi mkuu..

Mwanzoni itakua ngumu kidogo as vijana wengi Kilimo wanakiona ni cha waliofeli..

.itakua tabu kubadilisha attitude yao

...ila with time wataweza kuona mazuri yake na kutaka kuwa involved....

..Naona swala la kutafuta masoko ni swala ambalo limekua identified kama changamoto...

...mie nashauri COOERATION..kati ya wakulima na serikali,wananchi tunalima tunaipa serikali feedback...na serikali inachunguza upatikanaji wa masoko kwa mazao yanayozalishwa....
 
Currently tunatumia 33% ya arable land, let’s aim to use at least 50% in the next two years and see where it will leads us,

Private sectors mnaweza ku seize this opportunity..mnaweza anzisha hizi shule za Kilimo, nilikua na idea but ngawira sina lol😢😢
 
Jibu ambalo lilikua common ni Kilimo na kazi za vibarua….

Vibarua sawa... ila kwenye kilimo...

Hiyo professional kabisa watu wanaiosmea vyuoni miaka kadhaa...



Cc; mahondaw
 
Jibu ambalo lilikua common ni Kilimo na kazi za vibarua….

Vibarua sawa... ila kwenye kilimo...

Hiyo professional kabisa watu wanaiosmea vyuoni miaka kadhaa...



Cc; mahondaw

rejea topic yangu ni kazi gani mtu aliyemaliza la saba na form four wanaweza kufanya kazi gani >>> https://www.jamiiforums.com/threads...la-saba-na-form-four-anaweza-kufanya.1549820/

Mkuu hata hivyo sidhani kama umeielewa topic hii..nimeomba vijengwe vyuo vya kilimo,watu wasome kuanzia ngazi ya chini..kilimo kiwe respected just like any other profession..na mtu anaweza ku build up qualifications mpaka level ya degree.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…