rejea topic yangu ni kazi gani mtu aliyemaliza la saba na form four wanaweza kufanya kazi gani >>> https://www.jamiiforums.com/threads...la-saba-na-form-four-anaweza-kufanya.1549820/
Mkuu hata hivyo sidhani kama umeielewa topic hii..nimeomba vijengwe vyuo vya kilimo,watu wasome kuanzia ngazi ya chini..kilimo kiwe respected just like any other profession..na mtu anaweza ku build up qualifications mpaka level ya degree.
Kilimo chenyewe nacho ni aghali, na hakitabiriki, ikikosekana mvua basi mvua imezidi, na yote yana athari hasi kwa mazao. Usipozuka moto, basi wanyama na wafugaji waharibifu. Ukipata mazao, soko kama halikuingiliwa na wanasiasa, shukuru Mungu. Umasikini ni mzigo.
Soko soko soko ni changamoto kubwa kwa wakulimaNilikua namaanisha kuwezeshwa ni kupewa Elimu pamoja na Mashamba..
Ilikuwa nije na topic nyingine ya jinsi ya kuwawezesha..
nilichotaka ku advise hivi vyuo vya kilimo vikianzishwa vianzishwe kwa kuzingatia mazingira yetu pekee..
mambo ya kukariri hapana...
.na lugha ya kufundishia iwe ya Kiswahili..sababu nimeona kuna barrier kwenye Elimu yetu sababu ya lugha.
nilichotaka pia ni kuona progression mtu anasoma kidogo kidogo hadi anafikia ngazi ya Chuo kikuu kama SUA .....anapata Degree yake...
hao waliozaliwa 2,000 na bahati mbaya wakafeli,wakionyeshwa alternative ya kuprogress katika Maisha yao..Im sure watafanya vyema tuu
Hapa umeandika kinadharia sana. Mpaka kufikia kwenye hayo matokeo kuna changamoto nyingi sana ambazo haziwezi kua addressed na elimu tu au mtu kua na shamba. Ikiwa wataalamu waliomaliza SUA hawajajiajili kwenye kilimo sembuse huyu aliyemaliza std vii? Kilimo kinahitaji mtaji mkubwa sana mfano kulima nyanya ekari moja unahitajika kua na si chini ya milion 1. Hapo bado gharama zako za kuishi ktk kipindi chote tokea unalima mpaka kuvuna. Na kama ukiamua kulima mazao kwa ajili ya export hayo ndo gharama zake Mara dufu. Tuje soko hapo hakuna tofauti na mchezo wa kubeti. Kilimo kinahitaji mtu awe mvumilivu sana, asiyekata tamaa baada ya kula loss,risk taker, asiwe na higher expectation.Assume umempatia elimu kuhusu kilimo au na pia kumsaidia shamba huyu kijana...
Kwa kipindi cha miaka kumi (10) atakua amefikisha miaka 28-34,probably kaajiri watu kadhaa kwenye shamba lake...Sio tu ameongeza uzalishaji na kupunguza u dependency bali pia kuwa na CONFIDENCE
Mada yako ni nzuri sana ila kinachonishangaza ni namna unavyoongea kuhusu kilimo as if ndo tumepata uhuru jana na hii nchi haijawahi kulima kabisa yani ndo inataka kulima kwa mara ya kwanza [emoji3]
Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app