Kilimo as solution to unemployment

Kilimo as solution to unemployment

rejea topic yangu ni kazi gani mtu aliyemaliza la saba na form four wanaweza kufanya kazi gani >>> https://www.jamiiforums.com/threads...la-saba-na-form-four-anaweza-kufanya.1549820/

Mkuu hata hivyo sidhani kama umeielewa topic hii..nimeomba vijengwe vyuo vya kilimo,watu wasome kuanzia ngazi ya chini..kilimo kiwe respected just like any other profession..na mtu anaweza ku build up qualifications mpaka level ya degree.

Naijua hiyo topic na nili comment humo... nimekuelewa sana...


Cc: mahondaw
 
Kwenye mambo karne ya automation na industrial farming..., small farmer ni vigumu ku-compete..., cha maana ni kurudisha vyama vya ushirika na kuwa na mashamba makubwa ya ushirika kwa faida ya watu wote.., ni upunguani kusema hakuna masoko na mazao yanaozea shambani wakati kuna watu wanalala na njaa.., hapo utagundua hakuna buying power (maybe capitalism is not working after all)
 
Kilimo chenyewe nacho ni aghali, na hakitabiriki, ikikosekana mvua basi mvua imezidi, na yote yana athari hasi kwa mazao. Usipozuka moto, basi wanyama na wafugaji waharibifu. Ukipata mazao, soko kama halikuingiliwa na wanasiasa, shukuru Mungu. Umasikini ni mzigo.
 
Kilimo chenyewe nacho ni aghali, na hakitabiriki, ikikosekana mvua basi mvua imezidi, na yote yana athari hasi kwa mazao. Usipozuka moto, basi wanyama na wafugaji waharibifu. Ukipata mazao, soko kama halikuingiliwa na wanasiasa, shukuru Mungu. Umasikini ni mzigo.

Kwa kweli ni changamoto ila tukishirikiana na wataalam hata wa environment wataweza ku predict Haya mambo ya mvua, na wanaweza pia kutupa strategies za kuhimili pale mambo yanapoharibika, so hili swala la kilimo lijaze Watsaalam mbalimbali kwa mtazamo wangu
 
Nilikua namaanisha kuwezeshwa ni kupewa Elimu pamoja na Mashamba..

Ilikuwa nije na topic nyingine ya jinsi ya kuwawezesha..

nilichotaka ku advise hivi vyuo vya kilimo vikianzishwa vianzishwe kwa kuzingatia mazingira yetu pekee..

mambo ya kukariri hapana...

.na lugha ya kufundishia iwe ya Kiswahili..sababu nimeona kuna barrier kwenye Elimu yetu sababu ya lugha.

nilichotaka pia ni kuona progression mtu anasoma kidogo kidogo hadi anafikia ngazi ya Chuo kikuu kama SUA .....anapata Degree yake...

hao waliozaliwa 2,000 na bahati mbaya wakafeli,wakionyeshwa alternative ya kuprogress katika Maisha yao..Im sure watafanya vyema tuu
Soko soko soko ni changamoto kubwa kwa wakulima
 
Assume umempatia elimu kuhusu kilimo au na pia kumsaidia shamba huyu kijana...

Kwa kipindi cha miaka kumi (10) atakua amefikisha miaka 28-34,probably kaajiri watu kadhaa kwenye shamba lake...Sio tu ameongeza uzalishaji na kupunguza u dependency bali pia kuwa na CONFIDENCE
Hapa umeandika kinadharia sana. Mpaka kufikia kwenye hayo matokeo kuna changamoto nyingi sana ambazo haziwezi kua addressed na elimu tu au mtu kua na shamba. Ikiwa wataalamu waliomaliza SUA hawajajiajili kwenye kilimo sembuse huyu aliyemaliza std vii? Kilimo kinahitaji mtaji mkubwa sana mfano kulima nyanya ekari moja unahitajika kua na si chini ya milion 1. Hapo bado gharama zako za kuishi ktk kipindi chote tokea unalima mpaka kuvuna. Na kama ukiamua kulima mazao kwa ajili ya export hayo ndo gharama zake Mara dufu. Tuje soko hapo hakuna tofauti na mchezo wa kubeti. Kilimo kinahitaji mtu awe mvumilivu sana, asiyekata tamaa baada ya kula loss,risk taker, asiwe na higher expectation.

Ushauri wangu:
Mafunzo bora ya kilimo kwa vijana waliomaliza darasa la saba yasitolewe vyuoni. Wachukuliwe hao vijana waingie mashambani waanze na hatua moja mpaka mwisho. Wakiwa huko wajitegemee wao kuanzia Chakula na kufanya kazi za shamba ili wajifunze uvumilivu, kujitegemea na stadi za kilimo kwa vitendo
 
Mada yako ni nzuri sana ila kinachonishangaza ni namna unavyoongea kuhusu kilimo as if ndo tumepata uhuru jana na hii nchi haijawahi kulima kabisa yani ndo inataka kulima kwa mara ya kwanza [emoji3]

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
 
Mada yako ni nzuri sana ila kinachonishangaza ni namna unavyoongea kuhusu kilimo as if ndo tumepata uhuru jana na hii nchi haijawahi kulima kabisa yani ndo inataka kulima kwa mara ya kwanza [emoji3]

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app

😂😂😂 kwa nini umesema hivyo mkuu???
 
Back
Top Bottom