Kilimo biashara pekee inayolipa 100%, kilimo awamu ya pili.

Kilimo biashara pekee inayolipa 100%, kilimo awamu ya pili.

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,917
Reaction score
11,801
Ndugu zangu awali nilileta uzi uliokuwa unasema Kilimo ni biashara pekee inayolipa 100%, wapo waliopinga na wapo walikubaliana nami, lengo la uzi nilikuwa nimewalenga hasa vijana waliomaliza vyuo vikuu wanaozunguka na bahasha huku wakikidharau kilimo ambacho kinaweza kuwatoa na kupata mitaji. Wapo watu walihoji kwamba kama kilimo kinalipa mbona wazee wamejihusisha na kilimo kwa muda mrefu ni maskini? Wao wana hoja ya msingi ila wakumbuke watu wengi wanafanya kilimo cha kienyeji sana, hawatumii mbolea, hawapandi kwa vipimo matokeo yake huvuna mazao duni, lakini ukilima kisasa utakifurahia kilimo.

Awamu ya pili nimelima ila nikaongeza ukubwa wa shamba kidogo toka ekari mbili mpaka tatu, nilitumia takribani laki tisa kuandaa mashamba hayo mpaka kuvuna, kwa mchanganuo ufuatao.
Mbolea mifuko 4@61,000/=
Mbegu mifuko 16@10000/=
Kulima nilitumia ng'ombe zangu, ingawaje kama nisingetumia ng'ombe hizo gharama yake ingelikuwa 200,000/=
Kupanda mashamba yote 75,000/=
Palizi awamu ya kwanza na ya pili jumla 210,000/= awamu ya kwanza 105,000/= @ekari 35,000/=
Mpaka sasa nimevuna ekari 2 nilizivuna mwishoni mwa mwezi wa tano, nilitumia Tsh50,000/=
Mifuko 40@10000=40,000/=
Kupukuchua 1@2000 nilivuna gunia 38@2000=76,000/=
Huo ndio mchanganuo ninaoukumbuka katika awamu ya pili ya mahindi niliyolima.

Katika ekari mbili nilizo vuna nimepata gunia 38, ambazo niliziuza 3,465,000/=
Hivyo mtaji wangu wa kilimo misimu miwili una jumla ya milioni tano.

Katika kukuza mtaji nimechukua milioni mbili iliyobaki mwaka jana baada ya kutoa gharama za kilimo awamu ya pili nimeongeza za sasa hivi nimeanza kununua mahindi maana bei kwa sasa imeshuka gunia la mahindi linauzwa Tsh 50,000/=ila nina uhakika kwa hali ya chakula iliyopo nchini kufikia mwezi wa tisa gunia litakuwa linauzwa laki,maana nimetembelea mikoa ya Geita, Tabora, Mwanza, baadhi ya maeneo mkoa wa Mara na simiyu, katika mikoa hiyo hali ya chakula ni tete.
Ekari ya tatu ambayo sijavuna nategemea kupata gunia 17~20 haya nitayachanganya na ambayo nanunua sasa hivi ili niyauze bei ikipanda.

Faida nyingine niliyoiona kwenye kilimo ni kwamba ni biashara pekee ambayo usimamizi wake ni mdogo mimi nipo Mwanza lakini nafanya kilimo Tarime na mambo yanasonga tu, katika mashamba yote nilienda kuvuna tu wakati mwingine wote nilikuwa natuma pesa..

Nawaasa vijana wenzangu ambao hamjapata ajira msikae kuzunguka na bahasha tuu, geukieni kilimo kinalipa, sisemi kwamba muwe wakulima, hapana, ila kilimo ni njia nzuri ya kupata mtaji kwa haraka kama nilivyo fanya mimi.

Rejea,
Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%
 
Kilimo kinalipa kipindi cha njaa tu...kukiwa hakuna uhaba wa chakula ni hasara tu...
 
Kilimo cha google na makaratasi kizuri ila hakuna mkulima Tajiri.

Ila kuna wafanya biashara tajiri( wanaonunua mazao kwa wakulima)
 
Ukilima afu una hela hapo ndio utapata faida maana utauza wakati hakuna chakula sokoni
Tofauti na hapo utakua
 
Mkuu usije potosha watu walime kwa kutuma hela tu huku wakisubiri kwenda kuvuna. Wewe shukuru umepata watu waaminifu wanakutunzia shamba vizuri na hawakuibii.
Ni kweli ninachokifanya mashamba yapo karibu na nyumbani, mama hunitafutia watu wa kufanya kazi wakimaliza huniambia niwalipe na huwa mara nyingi nawatumia kwenye simu zao.
 
Kilimo cha google na makaratasi kizuri ila hakuna mkulima Tajiri.

Ila kuna wafanya biashara tajiri( wanaonunua mazao kwa wakulima)
Ni kweli mkuu, ila kwa kuanzia na kupata mtaji sio mbaya sana, lakini pia ujue kilimo ni biashara ambayo unaweza kufanya huku unaendelea na biashara zako.
 
Weka gharama za Usimamizi,hata Mama yako anahitaji kulipwa supervision fees!!
Jilipe pia Gharama unazotumia kama Investor.
Kisha weka hesabu vizuri.
 
Kuna kitu napenda kufahamu kutoka kwako. Tangu uzi ule wa mwanzo hadi huu, unasifia kilimo pekee ndio kinalipa Kwa asilimia 100.
Lakini sijafahamu nini unakifanya mwanza wakati unachokisifia sana kinafanywa tarime na watu wengine
 
Ni kweli kilimo hakimtupi MTU hasa cha umwagiliaji...njoon morogoro dakawa
 
Back
Top Bottom