Kilimo biashara pekee inayolipa 100%, kilimo awamu ya pili.

Kilimo biashara pekee inayolipa 100%, kilimo awamu ya pili.

Ndugu zangu awali nilileta uzi uliokuwa unasema Kilimo ni biashara pekee inayolipa 100%, wapo waliopinga na wapo walikubaliana nami, lengo la uzi nilikuwa nimewalenga hasa vijana waliomaliza vyuo vikuu wanaozunguka na bahasha huku wakikidharau kilimo ambacho kinaweza kuwatoa na kupata mitaji. Wapo watu walihoji kwamba kama kilimo kinalipa mbona wazee wamejihusisha na kilimo kwa muda mrefu ni maskini? Wao wana hoja ya msingi ila wakumbuke watu wengi wanafanya kilimo cha kienyeji sana, hawatumii mbolea, hawapandi kwa vipimo matokeo yake huvuna mazao duni, lakini ukilima kisasa utakifurahia kilimo.

Awamu ya pili nimelima ila nikaongeza ukubwa wa shamba kidogo toka ekari mbili mpaka tatu, nilitumia takribani laki tisa kuandaa mashamba hayo mpaka kuvuna, kwa mchanganuo ufuatao.
Mbolea mifuko 4@61,000/=
Mbegu mifuko 16@10000/=
Kulima nilitumia ng'ombe zangu, ingawaje kama nisingetumia ng'ombe hizo gharama yake ingelikuwa 200,000/=
Kupanda mashamba yote 75,000/=
Palizi awamu ya kwanza na ya pili jumla 210,000/= awamu ya kwanza 105,000/= @ekari 35,000/=
Mpaka sasa nimevuna ekari 2 nilizivuna mwishoni mwa mwezi wa tano, nilitumia Tsh50,000/=
Mifuko 40@10000=40,000/=
Kupukuchua 1@2000 nilivuna gunia 38@2000=76,000/=
Huo ndio mchanganuo ninaoukumbuka katika awamu ya pili ya mahindi niliyolima.

Katika ekari mbili nilizo vuna nimepata gunia 38, ambazo niliziuza 3,465,000/=
Hivyo mtaji wangu wa kilimo misimu miwili una jumla ya milioni tano.

Katika kukuza mtaji nimechukua milioni mbili iliyobaki mwaka jana baada ya kutoa gharama za kilimo awamu ya pili nimeongeza za sasa hivi nimeanza kununua mahindi maana bei kwa sasa imeshuka gunia la mahindi linauzwa Tsh 50,000/=ila nina uhakika kwa hali ya chakula iliyopo nchini kufikia mwezi wa tisa gunia litakuwa linauzwa laki,maana nimetembelea mikoa ya Geita, Tabora, Mwanza, baadhi ya maeneo mkoa wa Mara na simiyu, katika mikoa hiyo hali ya chakula ni tete.
Ekari ya tatu ambayo sijavuna nategemea kupata gunia 17~20 haya nitayachanganya na ambayo nanunua sasa hivi ili niyauze bei ikipanda.

Faida nyingine niliyoiona kwenye kilimo ni kwamba ni biashara pekee ambayo usimamizi wake ni mdogo mimi nipo Mwanza lakini nafanya kilimo Tarime na mambo yanasonga tu, katika mashamba yote nilienda kuvuna tu wakati mwingine wote nilikuwa natuma pesa..

Nawaasa vijana wenzangu ambao hamjapata ajira msikae kuzunguka na bahasha tuu, geukieni kilimo kinalipa, sisemi kwamba muwe wakulima, hapana, ila kilimo ni njia nzuri ya kupata mtaji kwa haraka kama nilivyo fanya mimi.

Rejea,
Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%
Vema sana Molembe... naomba ni pm namba yako nahtaji kujifunza zaidi kutoka kwako, ahsante.

Sent from my SM-T231 using JamiiForums mobile app
 
Unakuwaga ka-pili kuchangia lakini huwaga huna point sijui kwa nini?
Ee sinaga point mkuu...We unategemea kila mahali ni pa kutoa point? Kwani kusema sawa mkuu wewe inaonekana imekuuma sana na wakati mtu ametoa ushauri nami nikamsapoti kwa kusema sawa...Hahaha anyways, tusipangiane cha kupost mkuu, hivyo tu mkuu..Asante
 
Ni kweli ninachokifanya mashamba yapo karibu na nyumbani, mama hunitafutia watu wa kufanya kazi wakimaliza huniambia niwalipe na huwa mara nyingi nawatumia kwenye simu zao.
Mkubwa hizo mbolea ni zile za kupandia tu na za kukuzia pia unaweka
 
Kabla hata ya uzi huu nimeona matunda ya kilimo kupitia wakulima kadhaa na kwa kweli msimu huu naingia kwenye risk.nauza gari langu moja na pesa hiyo naendea shambani maana mifano nimeshaiona kupitia kazi niliyowahi kufanya hapo nyuma ya kuingia vijijini,niliona wakulima wengi wakipata mazao na kuishi bila shida japo wao walikosa tu ile elimu ya watumieje kilimo kuwafanya waishi maisha ya raha,waliendelea kuishi ktk nyumba zisizo imara na zisizo na usafi zaidi ya kuongeza kununua mifugo tu.lakini kama unamshuhudia mkulima anavuna mahindi gunia mia tano mpaka mia6 maana huyu anacheza na milion 40 mpka 50 ktk mavuno yake,kitu ambacho kwa maisha ya mjini kwa wengi unaweza piga kwata miaka na miaka hujawahi kuiona hiyo milion 40 zaidi ya kuishia kukopa ofisini milion 10 na kununua Alteza.tutake tusitake tukitaka mali tutaipata shambani

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Very true.
 
At least huyu jamaa huko realistic sio wale WA gunia 30,by the way kilimo ni hesabu Kali na timing
 
Ni kweli kilimo kinalipa kama ukiamua kuweka mikakati na kujitoa pia tumia ubunifu siyo lazima kulima mazao ya msimu kama kuna sehemu ambayo maji yanapatikana kwaajili ya umwagiliaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nategemea kuanza kufanya kilimo cha umaagiliaji cha bustani na eneo langu ni heka moja tuu ila natarajia kuliweka katika kilimo cha custom garden ipo cku ntafanikiwa mungu akipenda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom