Kilimo bila katiba mpya ni ndoto

Kilimo bila katiba mpya ni ndoto

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2019
Posts
1,213
Reaction score
1,918
Ajira mpya zimeshindikana kutengenezwa wakati Population ya watu inaongezeka kama utitiri.

Serikali imefeli kubuni na kuendeleza mifumo iliyopo ya kiuchumi ili izalishe ajira.

Kwa nchi yetu hii, Kiwanda pekee kinachoweza kutoa ajira kwa idadi kubwa ya watu ni KILIMO..

Tumeshindwa kufanya Uwekezaji mkubwa kwenye KILIMO, katika nchi ambayo kila KATA inalimika tunashindwaje kuwa na IRRIGATION SCHEMES wakati tumejaa na Maji kila kona ya nchi...

Nchi hi jumla ya KATA ipo kwenye 4,000 hivi, ina maana kama kila KATA ikiwa na IRRIGATION SCHEME ambazo nyingi zimejengwa na Serikali kwa gharama isiyozidi Bilioni 2/- basi nchi nzima tunahitaji kama Trilioni 8..

Nchi inakopa MATRILIONI kibao lakini MKULIMA kule chini bado MASIKINI wa kutupwa.
Screenshot_20230204-140421.jpg


Ni wazi Serikali imeshindwa kukipigania KILIMO, Kiwanda kinachotegemewa na zaidi ya robo tatu ya nchi, sasa kwanini wasitafutwe watu wa kuwekeza kwa makusudi kabisa kama ilivyo kwenye MADINI?

WATENDAJI wetu wakuu wanapenda hela inayozalishwa PAPO KWA PAPO ili wapige 10% watambae na chao.

Hakuna anayemfikiria mwanachi wa mwisho kabisa kule kijijini anayetaabika na jembe la mkono.

Serikali inatoa Ruzuku kwenye Mbolea, vipi kuhusu pembejeo zingine na gharama za Kilimo? Kilimo bado ni cha mazoea huku wakulima wakiendelea kuwa Masikini.

Endapo KILIMO kikitengeneza ajira, kitafungua ajira zingine nyingi sana.

Tanzania leo inaweza ikawa muuzaji wa mazao ya chakula na biashara kwa nchi nyingi sana haswa kwenye zama hizi na zijazo..

Kila Kanda ya nchi hii ina zao la biashara la kuliingizia hela..

Mwishowe inaonekana tunahitaji kugawa hii inchi KIKANDA ili tufanikiwe... Ndo tunafikia kwenye KATIBA 😂😂😂 ... Kila kitu nchi kimesimamishwa na KATIBA ya MKOLONI 🤣🤣

Hili BOMU la AJIRA ambalo wakubwa bado hawajalitolea macho ipo siku litawalipukia... Tengenezeni KILIMO kiajiri WATANGANYIKA, siye Watanganyika tukishakuwa na vijisenti mfukoni ya Chakula, Kodi na kulipa Ada za WATOTO wetu hatuna shida hiyo MIRADI mikubwa nyie gombanieni tu😁😁
 
Back
Top Bottom