Ubora: Mbegu ninazohitaji ni yale machipukizi yanayotokea chini mche wa nanani (‘suckers') au yale machipukizi ya pembeni chini ya tunda (‘slips') na sio ile sehemu ya tunda ya juu (crown) inayoachwa baada ya tunda kuliwa. ‘Suckers' ni bora zaidi kuliko ‘slips' na hata bei itazingatia tofauti hiyo na pia ukubwa wa mbegu yenyewe (ikiwa kubwa ni bora zaidi).
Mahali: Shamba lipo kilomita 5 kutokea kijiji cha Mwasonga wilaya ya Temeke (Dar). Kijiji cha mwasonga kipo kama kilometa kama 34 kutokea ferry (kigamboni) ama kama ni kupitia njia ya mbagala ni kama kilometa 50 hivi au kwa wale wanaopafahamu Kibada, ni kilometa 25 kutoka hapo. Barabara kutokea Kibada ni changarawe na kwa ujumla ni nzuri – all weather (sehemu kubwa ya barabara unaweza kuendesha mpaka speed 80-90km/h kwa gari dogo). Gari linafika mpaka shambani.
Bei: Kutegemeana na ubora, tupo tayari kununua kwa mpaka shilingi 130 (haipungui sh 120) kwa mbegu kama ikifikishwa mpaka shambani au mpaka shilingi 120 (haipungui sh 100) kama ikifikishwa kijiji cha Mwasonga. Aidha, tupo tayari kununua mpaka kwa shilingi 60 (range 0-60) kwa mbegu kama tukiifuata wenyewe katika sehemu ambayo inafikika kwa gari ya mizigo lakini eneo lenyewe liwe ni hapa Dar au kama ni nje basi lisilozidi kilometa 150 kutokea hapa Dar na mzigo uwe mkubwa unaoweza kufikia angalau tani mbili (roughly kama mbegu 5,000). Kama ni nje ya umbali huu, muuzaji mwenyewe itabidi afanye utaratibu wa kufikisha mzigo mpaka katika kituo ambacho kitakuwa ndani ya umbali/maeneo niliyotaja.
Uhakiki: Tunafahamu kuwa kama mbegu ni nyingi, inaweza kuwa ngumu kuhesabu mojamoja, hivyo katika hali kama hiyo tunaweza kukubaliana utaratibu rahisi zaidi wa kuhesabu (mf: kupima kwenye magunia au viroba na kutumia wastani wa mbegu zinazojaza gunia au kiroba husika). Tunaweza pia kutumia uzito katika kufikia idadi ya mbegu hizo. Kwa wastani, mbegu ya nanasi (suckers au slips) zina uzito wa gramu 350 mpaka 450 (i.e. pungufu kidogo ya nusu kilo).
Zingatia:
- Hakuna malipo ya kabla (advance payment).
- Kwa watakaotaka kuleta shambani, ukifikisha mzigo na kuhakikiwa unalipwa pesa yako (cash basis). Au kama tunakuja kuuchukua wenyewe mahali ulipo, tutalipa kabla hatujachuka mzigo wako (mara baada ya kuuhakiki).
- Kabla ya kuanza safari ya kuleta mzigo katika maeneo niliyotaja, tafadhali tuwasiliane na kukubaliana muda/siku kwanza.
- Hatutahusika na gharama zozote zitakazotokana na makosa ya muuzaji kuhusu vigezo na masharti tuliyoyataja hapo juu (aina ya mbegu, ubora, bei, mahali).