strong star
Member
- Jul 15, 2021
- 36
- 42
Asilimia zaidi ya 80 ya watanzania wote tunajishughulisha na kilimo ambacho ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu, Ikiwa hivi ndivyo mbona hatuna maendeleo kuanzia kwa mkulima, jamii, wala taifa kwa ujumla?'
Ni kwa sababu bado hatuna kilimo chenye tija na kutuletea maendeleo
Sasa tunaenda kuona kilimo chenye tija ni kipi amabacho kitaenda kutuletea maendeleo zaidi
Tambua aina ya ardhi unayotaka kuanzisha kilimo
Kwanza kabisa mkulima unapaswa kutambua aina ya ardhi alionayo ili kujua inafaa sana kwa kilimo gani, kwani kila aina ya zao unalotaka kulima linakuwa na kustawai vizuri katika aina furani ya ardhi, hivyo basi mkulima anapaswa kuchagua ardhi kulingana na kilimo anachotaka kuanzisha .
Tambua hali ya hewa katika shamba lako
Hakikisha mkulima unakuwa na tahalifa sahihi za misimu na hali ya hewa katika shamba lako hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabia nchi na hali ya hewa, hii itasaidia kujiandaa vilivyo na mabadiliko yoyote ya hali ya hewa kwa wakati wowote na kuepusha hasara kubwa ya mazao yako.
Tafuta mbegu bora zenye mazao mengi na kuvumilia magonjwa
Mkulima unapaswa kutafuta mbegu bora zaidi na tuache kilimo cha mazoea cha kutumia mbegu za zamani, kwani misimu inabadilika na wadudu kugundua njia mpya ya kushambulia mazao yako, hivyo basi yatupasa kushilikisha wataalam na kutumia mbegu bora, zinazohimili magonjwa na kutoa mazao mengi.
Tafuta wakati unaofaa kupanda mbegu zako
Wakulima wengi tunakosea sana katika wakati ufaao kupanda mbegu kwani utumia mazoea na kujikuta tunapata hasala kubwa kwa sababu siku hizi kuna mabadiliko ya Tabia nchi na hali ya hewa kwa ujumla na kujikuta tunapata asala kubwa.
Chunguza kwa makini na kwa ukalibu zaidi maendeleo ya shamba lako
Mkulima unapaswa kuwa kalibu zaidi na shamba lako kwani hivyo usaidia kutunza na kulinda shamba pia kutambua wakati sahihi wa kuweka mbolea na vilitubishi mbalimbali ambavyo vitakuletea mazao bora na mengi zaidi mwisho kupata kilimo chenye tija na maendeleo.
Andaa mahali sahihi pa kuifadhia mazao yako
Mkulima unapaswa kuandaa mahali sahii (yaweza kuwa ghala au gulio), usafiri na pia vibarua watakao saidia kuvuna vizuri mazao yako na kuyafikisha nyumbani au sokoni salama zaidi, hii usaidia kuepuka mazao kukauka au kusahaulika shambani na kupunguza ubora yanapofika sokoni au kwa mtumiaji.
Tafuta soko lenye tija au wananuzi wa mazao yako
Ikiwa umeifadhi vizuri kabisa mazao yako itakuwa rahisi na itakupa mawanda mapana ya wewe kutafuta soko na wanunuzi watakao kupa bei nzuri ya mazao yako na kupata faida ya jasho lako na kunufaika na kilimo chako.
Hivyo basi, kwa njia na mbinu hizi. tutaweza kupata kilimo chenye tija na mandeleo kwa wakulima na kuondokana na janga la umasikini kupitia kilimo chetu.