SoC01 Kilimo cha Alizeti ni Utajiri

SoC01 Kilimo cha Alizeti ni Utajiri

Stories of Change - 2021 Competition

MTEGULE

Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
15
Reaction score
22
PATA FAIDA KUBWA KUPITIA KILIMO CHA ALIZETI. KWA MTAJI WA LAKI MOJA NA AROBAINI (140,000) KWA HEKALI MOJA NA KUPATA ZAIDI YA MILLION MOJA NA LAKI NNE (1400,000/=) KWA SIKU TISINI (90).

Ndugu Wapendwa hapana shaka ya kuwa mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa la Tanzania.Ikiwa ni tofauti basi Mungu akufanyieni wepesi na mrudi katika hali zenu njema za awali.

Leo ningependa kuwapa mbinu au njia bora ya kuongeza kipato kwa kulima zao la alizeti kwa kutumia kiwango kidogo mnoo cha pesa ambacho ni laki na arobaini tu (140,000/=) na kuweza kupata faida zaidi ya millioni moja na nusu (1500,000/=) kwa siku tisini (90).Natambua kuwa una hamu na shauku ya kutaka kufahamu ni kwa namna gani kilimo hichi kinafanyika.

Alizeti ni miongoni mwa zao muhimu sana ambalo hutoa mafuta mazuri yasiyo na lehemu kwa ajili ya matumizi ya mwanadamu ya kila siku. Alizeti ni zao linalolimwa hasa maeneo ya ukanda wa kati hapa Tanzania kama vile Dodoma, Singida, Manyara na hata Tabora.

Alizeti ina sifa ya kustahimili ukame na ndiyo maana utaona hata mikoa ambapo hulimwa zao hilo haina sifa ya uwepo wa mvua nyingi.

Zao la alizeti limekua na soko kubwa mnoo hapa Ulimwenguni kutokana na uhitaji wake mkubwa, sambamba na hayo mwaka 2017 Tanzania ilitangazwa kuwa ni nchi ya pili katika uzalishaji wa zao la alizeti hapa barani Afrika.

Moja kwa moja nielekee na nieleze ni kwa namna gani unaweza kutumia mtaji kidogo sana na kuongeza faida maradufu ndani ya siku tisini.

Katika jimbo la Kibakwe, wilaya ya Mpwapwa iliyopo mkoani Dodoma..hii fursa adhimu ndipo inapatikana.Kwanza ifahamike kwamba katika vijiji mbalimbali vinavyopatikana jimbo la Kibakwe mfano.Chamtumile,ikuyu,chogola,winza,makose n.k) ardhi kwa ajili ya kilimo cha alizeti inapatikana ya kutosha na ni kwa bei rahisi mnoo.

Mchakato wenyewe uko hivi:

(i)Mbegu nzuri lita 2 ni Tsh 20000/=

(ii) Kukodi shamba hekali moja ni Tsh 20,000/=

(iii) Kusafisha shamba(Kuberega) hekali moja ni Tsh 10,000/=

(iv) Kulima na jembe la plau (Kutifua) hekali moja ni Tsh 20,000/=

(v)Palizi ya kwanza na ya pili..ni Tsh 20,000/= kwa hekali moja.

(vi) Kukata, kuzipiga, usafirishaji mpaka mashineni ni Tsh 50,000/=.

Jumla ya gharama zote ni Tsh 140,000/= .

Kwa kawaida hekali moja ya alizeti hutoa gunia 12 hadi 15 kwa makadirio ya chini. Na katika maeneo ya huko huko zipo mashine maalumu kwa ajili ya kukamua alizeti na bei yake huwa ni chini sana na kama unayaacha mashudu huwa hakuna tozo yoyote.

Lakini pia, ifamike kwamba Gunia moja la alizeti ambazo huwa ni debe 6 tu. Hutoa mafuta kuanzia lita 18 hadi 25(Kwa makadirio ya chini) kutokana na vile alizeti ilivyokomaa.

Hivi sasa lita moja ya alizeti ni Tsh 7000/=kwenye maeneo mengi ya mjini lakini tujaalie wewe utauza kwa Tsh 5000/= kwa lita kwa sababu ni mali yako toka shamba.

Ikiwa umepata gunia 13 kwa hekali moja, kila gunia ukapata lita 22 za mafuta(Kwa makadirio ya chini) utakuwa na lita jumla 286 ukizidisha kwa (5000/=) utapata Milioni moja laki nne na elfu thelathini TSH 1430,000/=

Tsh 140,000/= Hadi Tsh1430,000/=

Faida iliyopatikana ni milioni moja laki mbili na tisini Tsh 1290,000/= kwa siku tisini (90).

Naomba kuwasilisha.
 
Upvote 12
niko katika mchakato na Kijana wangu kutoka singida. yaani somo limekuja kuniengezea spidi. nimekupa kura. naomba nawe nipe kura yako ndugu
 
Kuna Uongo au Upotoshaji katika habari hiii...Moja yawezekana wewe una shamba unataka ukodishe au wewe ni dalali au wale wanojiita Motivational speaker....

Vigezo vinavyosababisha nitie shaka

1. Kupalilia Heka moja nzima kea elf 10!

2. Kupanda Mpaka kuvuna heka kwa laki na 40...

haiwezekani...Heka inalimwa na Ngombe kwa siku 3 au hata 4 Ina maana unawalipa elf 5 kwa siku???
 
Ndugu Yangu kabla ya kuandika chochote jitahidi kutafakari unachokiandika..hizo gharama na shughuli zote ni kutokana na maeneo ambayo mimi nina ushahidi nayo kama nilivyoyaanisha hapo.

Na hili lipo wazi kuwa gharama za kilimo hutofautiana kulingana na sehem husika, mfano kuna sehem huwez kukodisha shamba hekali moja kwa elfu ishirini ila kwetu ni jambo la kawaida na kuna kipindi hushuka kwa hiyo bei.
 
Gharama zako ni za chini sana kuliko uhalisia, bei yako ya mafuta kutoka shamba ni kubwa sana kuliko uhalisia. In fact nimenunua mafuta ya alizeti lita kwa shilingi 5500 hapa Dar, sasa iweje wewe shambani uuze kwa 7000?

Itoshe kusema hakuna uhalisia katika kilimo hiki. Tutarajie kuliko kwa atakayefuata mwongozo huu
Kaka gharama ni za chini kulingana na sehemu nilipo, ukisoma vizur hiyo post bila shaka utaelewa..
 
hivi watu mnashindwa kabisa kujiongeza 🤣 🤣 🤣 mtu ameongelea gharama kwa mazingira anayoishi alafu mtu unabisha,wapo wanaopalilia mpaka kwa elfu 5 kwa heka! nadhani mtoa uzi ungeweka disclaimer kwamba unachosema hapa kinaweza kisiwe applicable kwa watu wengine ile ubusti wale ambao huchota taarifa kama zilivo bila kungalia mazingira yao
 
Mimi mtoa mada ntajaribu kumuongezea kuwa hakuweka gharama za usafiri ila mengine siwe kupingana nae sana maana ata mm mwaka jana niliweka watu wakapalilia hekari 3 kwa 60,000 yaan kila ekari ni 20,000 (mbinga) wakati mbeya ekari moja kupalilia ni 50,000 so kutokana na maeneo gharama hupanda na kushuka ata kulima hvyo hvyo pia kwenye mavuno ni sahihi mwaka 2018 niliwahi kukamua alizeti (songea) gunia la debe 7 nikapata NDOO KUBWA 1 na KIDUMU cha LITA 5 ni alzet nilizokuwa nimechanganya ndani ya shamba la mahindi.
Tatizo weng humu wanasikia tu vitu ila practically hawajawahi kabisa kwa sasa alzeti wengi wanapiga pesa sana kuliko ata Mpunga mm mwenyewe najuta sijui shetan gan alinishauri nilime mpunga niache alizeti.. mpunga gunia 40,000 alaf alzeti gunia hyo hyo kupata 100,000 ni kugusa tu.
 
Mm n mwenyej wa maeneo ya huku,weng tunalima zao la alzet kwa kuchanganya na mazao mengne Ktk shamb 1 kam mahnd,mbaaz,mtama karanga nk,ukichachanya mazao n rahsi kupata faida hata kama utakosa moj jngne litakubeba au hata kama zao moja bei ikiwa ndogo jingne ltakubeba mfano kwa mwaka huu mahind bei ipo chn lkn mbaaz kilo n 1500 alzet gunia linakaribia lak karanga gunia 40+

Gharama kwa shamba la eka 10

Kukodi eka 1@ 20,000=200,000
Kulima na trekta eka 1@ 25,000=250,000
Kupalia eka 1@ 20,000=200,000

Gharama za chakula
kwa wakazi na usafiri = 70,000
Japo hii itategemea na sehem ulipo wapata hao wakaz.ikiwa utawapata wakaz karibu na shamba gharam itakuw chn zaid ya hapo

Jumla ya gharama ni 720,000

Hapa sijaweka gharam ya mbegu maana hii nayo itategemea aina za mbegu utazotumia.weng huwa wanashndwa kumud mbegu za kisasa hvo hununua mbegu zilizolimwa msimu mmoja au miwili maan nazo hutoa mavuno meng

Kwa kulima mbeg za kisasa zlizotumika msimu mmoja hazitatofautiana na bei ya ya mazao sokon mfano kwa eka 10 kulima na trekta utahtaj
debe 4 za mahind 1@7,000=28,000
debe 2 za alzet 1@15,000=30,000
Mbaazi kilo 10 1@ 1500 = 15,000
Karanga kilo 20 1@2300=46,000

Jumla ya mbegu=119,000
Japo sio lazm kulima mazao yote na pia unaweza kuongeza

Jumla kuu ya gharama ni 839,000 kwa eka 10
Pia utaweka na ya emergence
 
Ni jambo la kheri sana kama hivyo ndivyo ilivyo, ingawa mimi siku zote huamini kilichopo kwenye karatasi na kwenye hali halisi huwa ni tofauti. Huweza kuwa na matokeo hasi au chanya...ingawa matokeo hasi huwa na nafasi kubwa kwani ni mara chache sana Mtu anayenufaika kutoka mbele na kualika wengine.
 
Mm n mwenyej wa maeneo ya huku,weng tunalima zao la alzet kwa kuchanganya na mazao mengne Ktk shamb 1 kam mahnd,mbaaz,mtama karanga nk,ukichachanya mazao n rahsi kupata faida hata kama utakosa moj jngne litakubeba au hata kama zao moja bei ikiwa ndogo jingne ltakubeba mfano kwa mwaka huu mahind bei ipo chn lkn mbaaz kilo n 1500 alzet gunia linakaribia lak karanga gunia 40+

Gharama kwa shamba la eka 10

Kukodi eka 1@ 20,000=200,000
Kulima na trekta eka 1@ 25,000=250,000
Kupalia eka 1@ 20,000=200,000

Gharama za chakula
kwa wakazi na usafiri = 70,000
Japo hii itategemea na sehem ulipo wapata hao wakaz.ikiwa utawapata wakaz karibu na shamba gharam itakuw chn zaid ya hapo

Jumla ya gharama ni 720,000

Hapa sijaweka gharam ya mbegu maana hii nayo itategemea aina za mbegu utazotumia.weng huwa wanashndwa kumud mbegu za kisasa hvo hununua mbegu zilizolimwa msimu mmoja au miwili maan nazo hutoa mavuno meng

Kwa kulima mbeg za kisasa zlizotumika msimu mmoja hazitatofautiana na bei ya ya mazao sokon mfano kwa eka 10 kulima na trekta utahtaj
debe 4 za mahind 1@7,000=28,000
debe 2 za alzet 1@15,000=30,000
Mbaazi kilo 10 1@ 1500 = 15,000
Karanga kilo 20 1@2300=46,000

Jumla ya mbegu=119,000
Japo sio lazm kulima mazao yote na pia unaweza kuongeza

Jumla kuu ya gharama ni 839,000 kwa eka 10
Pia utaweka na ya emergence
Je Heka 10 inatoa gunia ngapi za alizeti?

Weka hesabu kuwa umechanganya mahindi na alizeti.
 
Je Heka 10 inatoa gunia ngapi za alizeti?

Weka hesabu kuwa umechanganya mahindi na alizeti.
Japo tuna mashamb meng lkn shamb la eka 10 ambalo linajtegemea limetoa mazao kama ifuatavyo gunia ktk ujazo wa debe 7
Alizet gunia 25
Mahind gunia 13
Mbaaz gunia 15
Kunde gunia 7
Karanga gunia 4

Mahind tumekosa sana kutokana na hali ya ukame lakn mazao mengne yanavumilia ukame
 
Kwa hio hii bei wanatuuzia ya mafuta ya alizeti huku mtaani wanatunyonya sio?Serikali itoe bei elekezi maana si kwa mapesa yote hayo.#Kilimokalamu.
 
Japo tuna mashamb meng lkn shamb la eka 10 ambalo linajtegemea limetoa mazao kama ifuatavyo gunia ktk ujazo wa debe 7
Alizet gunia 25
Mahind gunia 13
Mbaaz gunia 15
Kunde gunia 7
Karanga gunia 4

Mahind tumekosa sana kutokana na hali ya ukame lakn mazao mengne yanavumilia ukame
Hii ni kwa heka 10?Kilimo kumbe kigumu ee
 
Back
Top Bottom