Nipo mpwapwa Dom, moja kati ya kilimo kinacholimwa sana huku. Mvua za mwezi wa 12, wa 1 hata wa pili unaweza ukapanda kimsingi ni zao linalovumilia ukame haliitaji mvua nyingi. Kukodi shamba huku ni elf 30 na kulima (wanatumia ng'ombe au powertiller) 25 - 30k kupalilia per acre 30k. Ni kilimo flan hv hakina mambo mengi sn sabab wenyej wa huku hawatumii mbolea ardhi kwa sehem kubwa ina rutuba. Hakuna matumizi ya viwatilifu (japo magonjwa au wadudu yanaweza kutokea). Mavuno baada ya miez 3-4. Makadirio unaweza pata gunia 3-4 kwa eka. Palizi hata ukipalilia mara moja unaweza kuvuna.