SoC03 Kilimo cha Azolla kiwe chaguzi la kwanza kwa wakulima na wafugaji nchini

SoC03 Kilimo cha Azolla kiwe chaguzi la kwanza kwa wakulima na wafugaji nchini

Stories of Change - 2023 Competition

Clark cian

Senior Member
Joined
Jul 3, 2021
Posts
154
Reaction score
146
UFUNGUZI
kutokana na teknolojia ya uchanganyaji wa vyakula inavyokua kwa kasi na kutuletea vyakula vyenye uwiano sahihi ,sasa basi kwa namna moja ama nyingine baadhi ya wafugaji wamekuwa wakilazimika kutumia gharama nyingi katika upatikanaji wa vyakula hivyo kwa ajili ya mifugo yao;hivyo kupelekea baadhi ya wafugaji wenye vipato vyachini kutoweza kupata vyakula hivyo kwa kiwango stahiki na muda sahihi.
Hali kama hii imechochea afya za mifugo kuzorota kutokana na matumizi ya malisho yenye uwiano wa virutubisho usio sahihi kwa mifugo yao, pia uzalishaji kwa mifugo kuwa mdogo ukilinganisha na kawaida.
Hivyo basi kutokana na mhemko wa kufungua akili za watanzania na kubadilisha mfumo wa maisha uliozoeleka, pamoja na kupitia tafiti mbalimbali juu ya mimea mbalimbali hasa juu ya virutubisho vilivyopo ndani mwao;ugunduzi wa mmea wenye asili ya gugumaji unaofahamika kwa jina la AZOLLA umekuwa msaada mkubwa kwa wafugaji hasa wenye kipato cha chini kutokana na mmea huo kuwa na uwiano sahihi wa virutubisho muhimu kwenye makuzi na uzalishaji wa mifugo yetu na sio tu mifugo kama vile ngombe ,mbuzi ,kondoo ,kuku, nguruwe pia hata samaki.

Mmea wa azolla ni upi?
ni aina ya mmea wa kijani ambao hupendelea zaidi kustawi kwenye mazingiza ya maji maji. mmea mmoja kati ya mingi wenye uwiano sahihi wa virutubisho muhimu vinavyohitajika na mifugo yetu.

Mmea wenye sifa ya umbo dogo,rangi ya kijani inayovutia ,mizizi mifupi inayoelea ndani ya maji, na mimea ambayo inaweza kuota eneo lolote ilimradi liwe na maji yaliyotuama .

images (4).jpeg


Muundo wa mmea wa azolla kikemikali ni upi?
Mmea wa zolla umeundwa na uwiano tofauti tofauti wa virutubisho ambavyo husaidia katika makuzi na uzalishaji wa wanyama wetu na huo uwiano ni kama ufuatao
Protini ghafi – asilimia 24 -30
mafuta ghafi – asilimia 3.3-3.6
Nitrojeni- asilimia 4-5
Phosphorus- asilimia 0.5-0.9
Kalsium- asilimia 0.4-1
Potasiam- asilimia 2-4.5
Magnesium- asilimia 0.5-0.65
Manganezi- asilimia 0.11-0.16
Madini chuma – asilimia 0.06-0.26
Kabohyadrate tata {starch}- asilimia 6.54
Crude fibre {nyuzi nyuzi ghafi}- asilimia 9.1
Sukari mumunyifu {glucose}- asilimia 3.5

Kutokana na uwiano huo,mmea huu umepewa sifa ya kuwa na uwiano wa virutubisho ulio sahihi hivyo kuwa halali kwa malisho ya wanyama wetu wafugwao ikiwemo Ng’ombe, mbuzi ,kondoo ,sungura, nguruwe,kuku na samaki pia ili kuweza kuboresha afya za mifugo yetu pamoja na kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa mifugo hiyo

Faida za mmea huu wa azolla
Kwenye sekta ya kilimo
Ni chakula kwa wanyama wote wafugwao kutokana na kuwa na uwiano sahihi wa virutubisho

Pia hutumika kama mbolea pale inapovunwa na kuhifadhiwa eneo lisilo na hewa {visima} hivyo kusababisha kuoza hivyo kutengeneza mbolea kwa ajili ya mazao mashambani

Kwenye sekta nishati
Mmea huu wa azolla pia hutumika kwenye upatikanaji wa nishati ya biogass , na hii ni baada ya kuvuna na kujaza ndani ya visima vilivyozibwa pande zote ,hivyo kuruhusu joto na unyevu unyevu kuozesha {decompose} mimea hiyo na kuzalisha gesi mbali mbali aina ya methane ambayo hutumika kama chanzo cha nishati mbadala kwa matumizi ya majumbani kwetu mfano kupikia

Kwenye mazingira
Mmea huu hasa maeneo ya jua kali {tropical region} husaidia kupunguza kiasi cha uvukizi [ evaporation] wa maji kwenye vyanzo vya maji hivyo kusaidia katika kutunza na kuendeleza vyanzo vya maji kwenye maeneo hayo hasa wakati wa wote wa kiangazi .

Pia mmea huo hutumika katika kupunguza kiwango kikubwa cha upotevu wa gesi ya oksijeni kikemikali na hata kibaiolojia kwakuwa hutumia kiasi kidogo cha gesi hiyo kwenye makuzi yake binafsi hivyo kufanya mzunguko wa gesi hiyo kwenye mazingira kuwa mkubwa wakati wote hasa usiku.Pia mimea hiyo husaidia katika kuboresha maji taka ni pamoja na kupunguza madini mbalimbali hatarishi yanayopatikana kwenye maji taka mfano nitrojeni na phosphorus .

Pia Mmea huu pia umeajiri watu ,baadhi ya watu wanajiingizia kipato kwa kuuza mbegu pamoja na kuuza mmea huo uliochakataliwa {processed} kama chakula cha mifugo moja kwa moja ,pia watu wanaweza kujipatia kipato kupitia uchimbaji wa visima sahihi kwa ajili ya uzalishaji wa mmea huu.


ANGALIZO JUU YA MMEA HUU
Kutokana na kuwepo kwa faida ya mmea huu pia mmea huu ni hatari kwenye mazingira yaliyokuwa na uhitaji wa mvua nyingi mfano mazingira ya wakulima nahii ni kwa kupunguza kiasi cha uvukizi wa maji kwenye vyanzo vya maji hivyo kuaribu mzunguko mzima wa upatikanaji wa mvua.

Ni kwa namna gani naweza
kuzalisha mwenyewe ?

Ni rahisi sana haina haja ya tractor ya kuchimba kisima ila ni wewe na jembe la mkono tuuh kwasababu visima hivyo huwa sio vyenye kina ,huwa ni visima vyenye urefu mdogo kwenda chini,hivyo basi chakufanya pima urefu na upana utakao pendelea kutokana na uzalishaji uutakao
images (6).jpeg


Width {UPANA}
Length {urefu}
Eneo la kisima ni sawa na uso wa maji


Baada ya hapo anza kuchimba kwa kuzingatia vipimo vyako na hakikisha hauchimbi kwenda chini sana ni kwa kiasi tu kwa makadirio ni kama inchi 5-6 kwenda chini,


Screenshot_20230707-002847_1.jpg


Source; agroimage




Baada ya hapo chagua kati ya kusakafia kwa cement au kufunika eneo la ardhi na plastics cover ili kusababisha maji kutuama eneo husika hivyo kukamilisha zoezi zima la uandaaji wa visima mahususi
kwa uzalishaji wa azolla
Comp3-6.jpg
images (5).jpeg
source; agroimage.com




Baada ya hapo changanya udongo wenye rutuba pamoja na mbolea zitokanazo na wanyama pamoja na maji safi, kisha jaza kisima chako na mchanganyiko huo.kisha hatua ya mwisho ni kuweka miche yako ya azolla na kuiacha kwa ndani ya wiki mbili tu hapo ndipo mda wa mmea huo kuchipua na kutanda ndani ya maji yako na hapo ndo ndipo utaweza kuvuna na kwenda kulisha wanyama wako
download (1).jpeg



Kuzingatia
Zao la azolla linaweza kustawi katika maeneo yote ya ardhi lakini hasa kwenye maeneo ya maji yenye kiasi cha hydrogen [Ph range] 3.5 hadi 10,na katika nyuzi joto 18-26.pia ni zao zuri Hali athiriwi na mabadiliko ya tabia za nchi kama yalivyo mazao mengine ya chakula
images (2).jpeg

Source;google azzolla

HITIMISHO
Azolla ni kama silaha kwa wafugaji na wakulima ,bila ya kuitumia itakuwa ni vigumu sana kukwepa vikwazo katika shughuli za kila siku kwasababu inapunguza gharama ya malisho kwa mifugo na pia ina chochea makuzi kwa mifugo yako.wafugaji kwa wakulima ni wakati wa mabadiliko kuhusiana na masuala ya malisho kwa mifugo yetu basi haina budi kubadilika.

ONGEZA UZALISHAJI KWA MATUMIZI YA AZOLLA ‘’
Asanteni sana mungu awatunze wote wafugaji pamoja na wale wanaovutiwa kwenye hii sekta

Fuatilia zaidi kuhusu uzalishaji Azolla kupitia link zifuatazo

outu.be/HL1oPqu-srU
 

Attachments

  • download (1).jpeg
    download (1).jpeg
    4.7 KB · Views: 9
Upvote 5
Back
Top Bottom