Kilimo cha Bamia: Fahamu kuhusu mbegu bora, mazingira sahihi ya kulima, magonjwa na namna ya kuyakabili

Kilimo cha Bamia: Fahamu kuhusu mbegu bora, mazingira sahihi ya kulima, magonjwa na namna ya kuyakabili

UTANGULIZI
Bamia ni zao la mbogamboga linalolimwa sana sehemu za joto, kwa lugha ya kigeni inaitwa Okra. Zao hili hutumika kama mboga inayoliwa matunda yanayotokana na mmea. Zao hili linafaida sana kiafya, baadhi ya watu hutumia bamia kutengenezea mrenda. Aina za bamia zinazojulikana zaidi ni Clemson Spineless, Emerald Green, White Velvet, Perkins Mammoth na Dwarf Prolific.

ASILI YAKE
Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limeenea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia na Philipines. Zao hili kwa sasa hulimwa maeneo mengi.

HALI YA HEWA
Zao hili hustawi katika mita 1000 kutoka usawa wa bahari na hushindwa kuvumilia hali ya baridi kali. Hustawi katika katika aina nyingi za udongo na huhitaji mvua za wastani. Mimea yake haitumii chakula kingi kutoka ardhini. Iwapo ardhi haina rutuba ya kutosha inapendekezwa kuweka mbolea ya takataka au samadi.

UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Lima shamba lako vizuri kwa kutumia trekta, jembe la ng’ombe, jembe la mkono au pawatila, hakikisha shamba linakuwa halina nyasi, changanya samadi au mboji na udongo ili kuongeza rutuba.

UTAYALISHAJI WA MBEGU
Andaa mbegu mapema kwa kawaida inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji kwenye bustani.

UPANDAJI
Mbegu za bamia hupandwa moja kwa moja katika bustani au shamba, lakini pia kwanza zinaweza kupandwa kwenye kitalu na kuhamishwa baadaye. Mbegu zimiminwe kidogo kidogo na miche ifikiapo urefu wa sentimeta 10 hadi 15, idadi yake ipunguzwe. Umbali wa unaopendekezwa ni sentimeta 40-50 kati ya mimea na sentimeta 70-80 kati ya mistari. Kilo moja hadi moja na nusu ya mbegu hutosha robo hekta ya bustani (zaidi ya nusu eka hivi).Aidha kuotesha ili kurahisisha uotaji mbegu mbili zipandwe kwenye shimo moja.

nafasi ya upandaji iwe ni sentimita 30 toka shimo hadi shimo na sentimita 50 toka mstari hadi mstari. Kwa zile aina zinazorefuka sana iwe sentimita 40 kati ya shimo na shimo na sentimeta 70 kati ya mstari na mstari.

MBOLEA
Katika zao hili inashauriwa kutumia mbolea za asili (samadi na mboji) au takataka ili kurutubisha ardhi na kupata mavuno mengi.

UPALILIAJI & UNYEVU
Shamba la bamia inatakiwa lipaliliwe kwa kuondoa nyasi na liwe safi ili kudhibiti magonjwa na wadudu, unyevu unahitajika ili kuongeza mavuno.

MAGONJWA &WADUDU

MAGONJWA

Zao la bamia pia hushambuliwa sana na ukungu uitwao ubwiri unga, pia hushambuliwa sana na utitiri mwekundu na aphids. Kwa hiyo kila wiki dawa ya ukungu na sumu ya wadudu ipuliziwe kwenye mimea ili kuweza kukua katika ustawi uliobora zaidi, pia ni vyema kuzuia kwa kufuata mzunguko wa mazao na kutumia dawa kulingana na ushauri wa wataalamu wa kilimo.

WADUDU
Mosaic Virus– Huu ni ugonjwa mbaya sana, majani huwa na madoa madoa na huumuka. Haki hii hupunguza mazao. Nyunyizia dawa za sumu kuua wadudu.

UVUNAJI
•Bamia huvunwa kabla ya kukomaa yaani zikiwa bado changa.
•Kiasi cha kilo 8000 zaweza kupatikana katika ekari moja iwapo zitatunzwa vizuri.
•Hakikisha unavuna bamia na kikonyo chake, kisu kinaweza kutumika kwa kuvuna.

SOKO
Nchini Tanzania soko la bamia lipo. Inakadiriwa kuwa ifikapo kipindi cha masika bei ya bamia sokoni huwa juu. Hivyo mkulima atakayekuwa na mavuno ya bamia wakati wa masika anatarajiwa kuuza kwa bei ya juu kwa kuwa kipindi hicho zao hili huwa adimu katika soko.Ukilima eneo lenye ukubwa wa ekari 3 faida yake huwa kubwa zaidi kwani debe kidogoo cha lita 10 huwa 5000-6000 fedha za kitanzania.Ukilima kipindi cha kiangazi ambapo zao hilo huwa jingi sokoni hukadiriwa kidoo cha lita 20 huuzwa 3000-4000 fedha za kitanzania.

TIP: FAIDA ZA BAMIA KWENYE MWILI WA BINADAMU
Bamia ni miongoni mwa mboga za majani ambazo kwa kisayansi huitwa, ‘Abelmoschus Esculentus’.

Vitamini A itokanayo na bamia husaidia kuupa mwili wako kinga ya kupigana na maradhi. Kwa wenye matatizo ya kuona, kula bamia mara kwa mara kutaimairisha mwanga katika macho yako.

Wingi wa vitamini A huzuia maradhi yatokanayo na virusi kama mafua.

Uteute uliomo katika bamia husaidia kuunda tishu za mwili na ngozi. Watu wenye ngozi laini na zinazoteleza wana kiwango kikubwa cha ute ambacho husaidia kujenga ngozi.

Ulaji wa mboga za majani kama bamia, husaidia katika kulinda mapafu na saratani za mdomo. Bamia zina wingi wa vitamini K ambayo husaidia kuimarisha mifupa na kuganda kwa damu.

SOURCE:www.kilimotanzania.tk
 
Uko sahihii. Mfano sasa hivi ndoo ni 15000 bei shambani. Buyuni kigamboni
bamia kwa siku hizi limekuwamoja ya mazao yenye faida kwa mkulima
mbegu zipo kwenye maduka ya pembejeo
zipo zinazokomaa kwa siku 45 na kuendelea
soko ni njenje kwa mijini
kipimo chake ni plastiki ya lita 20 na lita 10
bei inategemea na uwingi wake sokoni
lakinni haina hasara ya kutisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba ni wale dondoo kidogo kwa sababu nina ndugu yangu anafanya hicho kilimo na nilimdadisi sana. Anasema alilima miaka zaidi ya mara 6 akipata hasara. Ikabidi aende kuomba kazi kwa mtu anaelima ma-acres ila lengo haikua kupata mshahara ila kwenda kuiba mbinu za jamaa. Ndipo akajua kilimo cha bamia ni timing kama mazao mengi kama nyanya....So karibu kudadisi wataalam. Nikipata right season kwake ntaleta tu shares
 

KILIMO BORA CHA BAMIA

UTANGULIZI


Bamia ni moja ya zao la mbogamboga ambayo asili yake ni hapa hapa africa na nchini Ethiopia ambapo kwa sasa linalimwa katika nchi nyingine nyingi. Bamia ni moja kati ya mazao ambayo yanafaida sana ndani ya mwili wa binadamu:

  • Husaidia kusafisha utumbo mpana
  • Husaidia kurainisha choo
  • Huondoa uchafu mwilini
  • Huongeza uroto kwa wale wenye upungufu wa uroto kwenye maungio
  • Pia ina vitamin C ambayo husaidia kulainisha ngozi

Na faidia nyingine nyingi ambazo siwezi kuzitaja zote kwa wakati huu. Bamia hustawi vizuri katika maeneo 1000 mita kutoka usawa wa bahari

KUANDAA SHAMBA

Kama mazao mengine shamba la bamia linatakiwa kusafishwa vizuri na pia unaweza kuweka mbolea ya asili kama vile mboji, samadi na mbolea ya kuku

UPANDAJI

Bamia ni moja kati ya mazao rahisi sana kuhudumia kama mtu ukiwa makini, kabra ya kupanda mbegu ya bamia inatakiwa kulowekwa kwenye maji ya uvuguvugu kwa masaa 24 kama unakwenda kupanda maeneo ambayo hayana unyevu wa kutosha.

Nafasi ya kupanda ni sentimita 40 kati ya mmea na mmea na sentimita 80 kati ya mstari na mstari. Bamia huchukua siku 8 hadi 10 kuota inategemea na eneo husika.


MBOLEA NA KUPALILIA

Katika zao la bamia sio lazima sana kutumia mbolea ya chemicali kama haiitajiki unaweza kutumia mbolea ya asili, tumia mbolea ya kemikali kwa maeneo yasio na rutuba ya kutosha na unatakiwa kipalilia nyasi na magugu pale unapoona yameesha anza kukua shambani.

KUVUNA

Bamia kawaida inatakiwa kuvunwa pale ambapo inakua haijakomaa sana na hiyo inaweza kuchukua miezi m3 kutoka mda uliopanda inategemea na eneo husika na kwa eka moja unaweza kuvuna kilo 8000 inategemea na eneo na huduma zako.

MAGONJWA

Magonjwa yanayo sumbua sana bamia ni pamoja na:

  • Uburi unga
  • Mosaic virus
  • Ukungu

Hivyo tumia dawa ya kuzuia ukungu pamoja na za kuuwa wadudu pale wadudu wanapo onekana shambani. Palilia mapema pamoja na usafi shambani ili kuepusha magonjwa na wadudu.
 

Attachments

Kuna kitu ambacho watanzania tunatakiwa kukielewa na kuzingatia. Sasa hivi duniani nchi zilizoendelea wanajitahidi sana kutotumia chemicals kwenye kilimo. Ukienda Super Markets utakuta karibu kila aina ya bidhaa kuna zenye label iliyoandikwa ''Organic'', kumaanisha kuwa kilimo cha zao hili hakutumia chemicals. Na bei yake huwa kubwa zaidi. Kwa uzoefu wangu Bamia ni zo linaloweza kukua bila chemicals. Ni bora tukaendeleza mtindo wetu wa kilimo cha asili kisichotumia chemicals!
 
Nililima Bamia kiangazi, za kumwagilia kwa pump!! Bei niliyopata nilipoanza ilikuwa 4000 ilishuka hadi 3000 kwa debe moja la ujazo wa lita 20.

Ustawi wa bamia ulikuwa wa kawaida nilikuwa natoa ndoo 13 kwa eneo la robotatu eka mavuno ni mara mbili kwa wiki. Naamini kwa ekari moja nigevuna debe 20. Kunastori watu huvuna debe 30 au zaidi kwa eka mimi hizo sikuziona.

Huwa zinashambuliwa sana na ukungu uitwao ubwiri unga, pia hushambuliwa sana na utitiri mwekundu na aphids. Kwa hiyo kila wiki dawa ya ukungu na sumu ya wadudu, ulipe mpiga dawa, petrol ya kumwagilia na malipo ya mmwagiliaji, wachumaji kila debe 1000/=.

Ili uone pesa ya bamia lima masika, lima eneo kubwa kama ekari kuanzia 3. Kumbuka eneo unalovuna debe 1 bamia eneo kama hilo ungevuna debe 10 za nyanya. bei ya bamia iikifikia chini ya 4000/= debe hailipi !!!!!

Nina ekari mbili jijini hapa (nje kidogo ya DSM) nikaamua msimu wa masika nilime bamia sikutaka zao umiza kichwa!

Niliuza sana coz ndoo ilifika 7000 ya lita kumi, kilichonikera ni kupiga dawa kila wiki na mbolea kila baada ya siku 21.

Ukipitisha wiki bila dawa wadudu na unga vinamwagika na mazao yanapungua. Si zao jepesi kama tudhaniavyo

Ila uhakika wa hela ni mkubwa kila wiki unavuna mara mbili hadi tatu napata ndoo 25+ na wateja walikuwa wananitafuta mie napakia kwenye kirikuu nawapelekea. Sikuhangaika kuhusu wateja japo mwanzoni nilihofu
 
okra.jpg

Bamia ni zao linalolimwa sana nchi za joto. Zipo aina nyingi za bamia, aina zile za kiasili nazo hutofautiana kulingana na eneo moja na lingine. Bamia huliwa kama matunda au hupikwa kama mboga pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine.

Mambo ya kuzingatia katika kilimo cha bamia
- Hakikisha unatumia mbegu bora
- Panda kwa nafasi
- Mwagilia maji ya kutosha kulingana na hali ya hewa
- Palilia shamba vizuri
- Dhibiti magonjwa na wadudu waharibifu kwa wakati
- Vuna kwa wakati unaotakiwa

Jinsi yakupanda

Mbegu mbili zipandwe kwenye shimo moja. Nafasi ya upandaji iwe ni sentimita 30 toka shimo hadi shimo na sentimita 50 toka mstari hadi mstari. Kwa aina ya bamia zinazorefuka sana iwe sentimita 40 kati ya shimo na shimo na sentimeta 70 kati ya mstari na mstari.

Namna ya Umwagiliaji
Kama unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji bustanini kulingana na hali ya hewa ya eneo husika.

Palizi
Hakikisha shamba ni safi wakati wote kwa kuondoa magugu mara tu unapoona yamejitokeza ili kuongeza uzaaji wa bamia.

Wadudu waharibifu

Wadudu wanaoshambulia zao hili la bamia kama vile kimamba, funza wa vitumba na
utitiri mwekundu. Dhibiti wadudu hawa kwa kufuata njia zinazopendekezwa na wataalamu wa kilimo Kwenye eneo lako.
Magonjwa

Bamia hushambuliwa na magonjwa kama ukungu, ubwiri poda na kunyauka huathiri zao la bamia hivyo ni vyema kuzuia kwa kufuata mzunguko wa mazao na kutumia dawa kulingana na ushauri wa wataalamu wa kilimo eneo ulipo.

Uvunaji wa bamia
images(1).jpg


- Bamia huvunwa kabla ya kukomaa yaani zikiwa bado changa.
- Unashauriwa kutumia kisu kuvunia na uhakikishe unavuna bamia na kikonyo chake ili kupunguza kuharibika kwa bamia
- Kiasi cha kilo 8,000 zaweza kupatikana katika ekari moja iwapo zitatunzwa vizuri.

Soko la bamia

Soko la bamia ni kubwa sokoni mahitaji ni makubwa kuliko uzalishaji, unasubiri nini kuanza na kilimo hiki ujipatie kipato.
 
Mi.i nataka kima za kula tu mwenyewe kwenye kaeneo kangu hapa nje
 
Nina ekari mbili jijini hapa (nje kidogo ya DSM) nikaamua msimu wa masika nilime bamia sikutaka zao umiza kichwa!

Niliuza sana coz ndoo ilifika 7000 ya lita kumi, kilichonikera ni kupiga dawa kila wiki na mbolea kila baada ya siku 21.

Ukipitisha wiki bila dawa wadudu na unga vinamwagika na mazao yanapungua. Si zao jepesi kama tudhaniavyo

Ila uhakika wa hela ni mkubwa kila wiki unavuna mara mbili hadi tatu napata ndoo 25+ na wateja walikuwa wananitafuta mie napakia kwenye kirikuu nawapelekea. Sikuhangaika kuhusu wateja japo mwanzoni nilihofu
Mkuu ulilima mbegu gani? Wengi wanasema masika bamia haikubali
 
Back
Top Bottom