Kilimo cha Canola (Rapeseed) kinaweza kutupunguzia uhaba wa mafuta ya kula

Fred Katulanda

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Posts
380
Reaction score
550

Nimeangalia na kusona sehemu ya maandiko kuhusu mmea aina ya Canola au Rapeseed, ambao unaweza kuzalisha mafuta ya Kula zaidi ya Alizeti.

Wenzetu Kenya wenye mashamba makubwa wameanza kulima, licha ya kuwapatia faida lakini kimekuwa ni kama kilimo cha muda kusaidia kurutubisha ardhi au kubadilisha mazao wakati wa kulima Ngano.



Imeelezwa kuna aina mbili kuu za mafuta yanayopatikana kutoka na mmea huu wa Rapeseed. Ipo inayotoa mafuta kwa ajili ya kupikia na mafuta ya tasnia ya kemikali za magari.


Kwa upande wa Kenya inaelezwa kuwa bei ya jumla ya mbegu za Rapeseed (canola) kwa mwaka huu 2022, inakadiriwa kuwa Kati ya US$ 5.2 na US$ 9 kwa kilogram au Kati ya US$ 2.36 na US$ 4.08 kwa pound(lb). Bei hii kwa Kenya ni sawa na Shilingi ya Kenya (KES) 566.45 kwa kilogram kwa Mombasa and Nairobi.

 
Upatikanaji wa mbegu ukoje kwa Tanzania Kuna sehemu wanalima hili zao?
 
Upatikanaji wa mbegu ukoje kwa Tanzania Kuna sehemu wanalima hili zao?
Nimejaribu kufuatilia sijaona wala kusikia wapi Canola inalimwa hapa Tanzania.

Lakini nadhani upatilanaji mbegu siyo tatizo sana, nimeelekeza wadau wangu wanisakie huko Kenya. Ila najua kupitia Jamiiforums pia tunaweza kufanikiwa kuipata maana hapa tupo wadau wengi.
 
tuna weza zalisha mafuta ya kila aina

1. mafuta ya mpunga
2. mafuta ya zabibu
3. mafuta ya alzeti
4. mafuta ya parachichi
5. mafuta ya nazi
6. mafuta ya chikichi
7. mafuta ya karanga
8. mafuta ya wanyama
9. mafuta ya canola
10. mafuta ya ufuta
11. mafuta ya pamba
12. mafuta ya mahindi
13. mafuta ya soya
etc

mafuta ya mpunga yana zalishwa na muwekezaji pale shinyanga na kusafirisha kwenda nje ya nchi...






















 
Unahitaji mbegu kiasi gani? Kuna Mzungu Arusha analima hii kitu, ingawa sijajua mafuta anauzia wapi my be wazunhu wenzake, ni Pm number yako au nicheki 0783691072
 
Unahitaji mbegu kiasi gani? Kuna Mzungu Arusha analima hii kitu, ingawa sijajua mafuta anauzia wapi my be wazunhu wenzake, ni Pm number yako au nicheki 0783691072
Mkuu details za upatikanaji wa mbegu kwa mzungu inakuaje..kwa maana ya anauza bei gani kwa kilo..na shamba la heka moja linahitaji kiasi gani cha mbegu.?

#MaendeleoHayanaChama
 
Kumbe mafuta yapo aina nyingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…