Kilimo cha kitunguu msimu wa Kiangazi nyanda za juu kusini

Kilimo cha kitunguu msimu wa Kiangazi nyanda za juu kusini

INSONSILE

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
1,960
Reaction score
2,945
Iko hivi wadau. Katika kubadilishana mawazo na mdau mmoja, nikampa wazo kwamba baada ya kuvuna mahindi sasa tugeukie kilimo cha mali mbichi hususan Kitunguu maji. Malengo ni kwamba at least mwezi November mzigo unavunwa.

Mazingira ya shamba ni safi hivi najiandaa kuvuna mahindi. Maji yapo yalichimbwa borehole, so ni ya uhakika. Ila huyu mdau akanikatisha tamaa kwamba eti kitunguu kinafanya vizuri sana msimu wa kupanda february au machi kuvuna mei au Juni.

Akaongezea kwamba hiyo ya kulima kiangazi yana changamoto sana magonjwa kama kaukau yanavamia. Naomba kuuliza wazoefu mnisaidie hivi kuna ukweli wowote au ni fix tu za huyu mdau isije kuwa ni wivu tuu. Natamani sana uzoefu wa mtu aliye shamba na aliyewahi kulima kiangazi.

Lakini pia vipi kuhusu bei kwa mzigo utakaovunwa mwezi November utanikata au itakuwa super (assuming kwamba hizo changamoto za magonjwa hazitakuwa shida). Karibuni
 
2018 kidogo nijichanganye nikalime kitunguu Iringa....... ningefirimbwa... mshikaji wangu alinishawiishi sana .... tushee mtaji..... faida itadabo, badae nikabadili gia angani ...

Akaenda mwenyewe, alizika karibia 18m, kidogo achanganyikiwe huku biashara zake zinayumba, nguvu nyingi alielekeza kule
 
Hiyo kisima inakupa maji kiasi Gani kwa wiki heka moja ya kitunguu kwa drip irrigation inatakiwa uwe na maji walau Lita 40,000 kwa siku

Kuhusu Bei November December Bei hua ni nzuri sana tu.

Na kulima kiangazi kitunguu kinafanya vizuri tu Tena kiangazi kinaenda haraka zaidi siku 90 tu umevuna.

Wastani wa mavuno kwa drip irrigation ni gunia 80 -100

Kila la heri
 
Maji hata lita laki 5 kwa siku unapata bosi
 
Kama una mtaji mkubwa na hujawahi kulilima nakushauri uanze na eneo dogo.

November bei sio kubwa kuna kitunguu kingi kutoka njombe na Songea.
kama utakuwa na Stoo ya kuhifadhi uuze december mwishoni au january mpk Februari itakuwa poa sana
 
Back
Top Bottom