Kilimo cha Magimbi

Kilimo cha Magimbi

Teye

Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
39
Reaction score
3
Wakuu ,naomba ushauri kilimo cha Magimbi kabla sijajitosa.Nina shamba maeneo ya Mkuranga.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Ushauri upi?fafanua unataka upewe nasaa kwenye lipi,maana kama tayari unashamba maanaake umeshaamua kuyavulia nguo maji.
 
Chipukizi ,ninalo lakini sijaweka hilo zao
 
Jamani saa nyingine tunajibu haraka mno kwa nia sijui ya kushushua ama vipi. Mtu kuwa na shamba si lazima kuwa ana mazao yote. Huenda alikuwa analima vitu vingine sasa interest imehamia katika magimbi , hence kuomba kwake ushauri.

Sasa kama wewe unajua chochote , as long as ni ushauri, unampatia, kama huna , jaribu tu kukaza roho , uuzuie ulimi/mkono ukae kimya kusuburi wenye la kuandika.

Lakini hizi mambo za kushushuana na kutaka kuonekana tuko mbele kwa kila jambo, sio vema sana.

Nawasilisha.
 
nifahamuvyo mimi magimbi yanaota kwenye maji,au sehemu yenye maji mengi kila wakati hasa kwenye mito.hivyo hakikisha kuna maji ya kutosha,mnaojua zaidi mtujuze.labda kuna varieties zisizohitaji maji mengi.
 
Wataalam nasubiri ushauri au uzoefu wenu juu ya kilimo cha magimbi.Hasa ningependa kujua aina za mbegu,kipindi muafaka kwa kulima,magonjwa na tiba zake,upandaji kwa ekari na mavuno. Ahsanteni.
 
Jamani saa nyingine tunajibu haraka mno kwa nia sijui ya kushushua ama vipi. Mtu kuwa na shamba si lazima kuwa ana mazao yote. Huenda alikuwa analima vitu vingine sasa interest imehamia katika magimbi , hence kuomba kwake ushauri.

Sasa kama wewe unajua chochote , as long as ni ushauri, unampatia, kama huna , jaribu tu kukaza roho , uuzuie ulimi/mkono ukae kimya kusuburi wenye la kuandika.

Lakini hizi mambo za kushushuana na kutaka kuonekana tuko mbele kwa kila jambo, sio vema sana.

Nawasilisha.
ni kweli Kama mtu Hana cha kuchangia ni bora kukaa kimya. Magimbi yanahitaji Majibu Mengi sio ya kubangaiza au nchi yenye mvua nyingi Kama milimaa ya uluguru au rung we mbeya. Sulla la pili ni aina ya udon go unaohitajika. Hata sua inabidi watafute.
 
nifahamuvyo mimi magimbi yanaota kwenye maji,au sehemu yenye maji mengi kila wakati hasa kwenye mito.hivyo hakikisha kuna maji ya kutosha,mnaojua zaidi mtujuze.labda kuna varieties zisizohitaji maji mengi.

Yapo magimbi yanayostahimili udongo wa kawaida pia. Ni hasa ya purple.
 
Magimbi yanajulikana pia kama Coco yam, Arrow root, na Nduma kwa jirani zetu ukambani. Google kwa hizo.
 
Magimbi yanastahimili sehemu yenye maji mengi,,, udongo kwa wingi kuyafukia ili yawe makubwa pia ardhi yenye rutuba ili yawe na radha tamu.
 
Watanzania tuna shibe sana, kushiba kwetu kumepelekea uchaguzi ktk kla yetu, mfano, siku za nyuma huko Moshi/Bukoba ugali ulikuwa hauliwi kabisa, ukanda wa ziwa nyasa wali ni chakula cha siku kuu. Ukienda Musoma, wali sio chakula kwao,ila ugali, nk nk.

Magimbi yameangukia kuwa ni chaguo la mwisho kabisa ktk orodha ya vyakula, kwa huku Pwani kidogo ndio yana soko kiasi. Soko la magimbi lipo ila sio la scale kubwa kivile. Magimbi hayasumbui kabisa, kwa hiyo soko likiwapo la uhakika, ni option nzuri.

Sasa hivi jamii inabadirika sana, waliokuwa hawali ugali sasa wanachapa sembe, kama uonavyo, mihogo ilikuwa kwa ajili ya wachache ukanda wa pwani, sasa hivi mhogo ni dhahabu.

Kama upo Mkuranga, hakikisha shamba lako lina maji ya kutosha, udongo wa kilimo.
 
Siyo shibe mkuu, chakula chochote kikiwa hakipatikani sana maeneo flani basi hicho huwa hot cake, kuna jamaa yangu alifika kunitembelea kwangu akashangaa sana magimbi yanavopatikana kwa bei rahisi, basi yeye ikawa chakula chake kila siku usiku ni magimbi ya nazi kwa nyama! Nakumbuka wakati tunaishi kwetu extended family mzee wetu alikuwa mkulima mzuri wa mpunga, kuna kipindi mahindi yalikuwa adimu kiasi kwamba tunakula ugali wa mchele uliochanganywa na unga wa mahindi kidogo sana. Kwa hiyo unavolima zao flani kibiashara lazima uangalie sehem ambazo zao hilo halipatikani kirahisi hakika utapata bei nzuri, huyu jamaa yetu yeye nadhani ametarget soko la Dar, soko ambalo kila kitu kinahitajika kwa wingi, kuanzia senene wa bukoba mpaka machungwa ya Tanga!
 
Back
Top Bottom