Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ni kweli Kama mtu Hana cha kuchangia ni bora kukaa kimya. Magimbi yanahitaji Majibu Mengi sio ya kubangaiza au nchi yenye mvua nyingi Kama milimaa ya uluguru au rung we mbeya. Sulla la pili ni aina ya udon go unaohitajika. Hata sua inabidi watafute.Jamani saa nyingine tunajibu haraka mno kwa nia sijui ya kushushua ama vipi. Mtu kuwa na shamba si lazima kuwa ana mazao yote. Huenda alikuwa analima vitu vingine sasa interest imehamia katika magimbi , hence kuomba kwake ushauri.
Sasa kama wewe unajua chochote , as long as ni ushauri, unampatia, kama huna , jaribu tu kukaza roho , uuzuie ulimi/mkono ukae kimya kusuburi wenye la kuandika.
Lakini hizi mambo za kushushuana na kutaka kuonekana tuko mbele kwa kila jambo, sio vema sana.
Nawasilisha.
nifahamuvyo mimi magimbi yanaota kwenye maji,au sehemu yenye maji mengi kila wakati hasa kwenye mito.hivyo hakikisha kuna maji ya kutosha,mnaojua zaidi mtujuze.labda kuna varieties zisizohitaji maji mengi.
Yapo magimbi yanayostahimili udongo wa kawaida pia. Ni hasa ya purple.
Magimbi yanastahimili sehemu yenye maji mengi,,, udongo kwa wingi kuyafukia ili yawe makubwa pia ardhi yenye rutuba ili yawe na radha tamu.
Na wewe ni mkulima Mkuu?..Impressive! :ranger:
Mie ni mkulima mzuri sana,,, ukitaka kuelekezwa khs kilimo karibu sana
Watanzania tuna shibe sana, kushiba kwetu kumepelekea uchaguzi ktk kla yetu, mfano, siku za nyuma huko Moshi/Bukoba ugali ulikuwa hauliwi kabisa, ukanda wa ziwa nyasa wali ni chakula cha siku kuu. Ukienda Musoma, wali sio chakula kwao,ila ugali, nk nk.
Magimbi yameangukia kuwa ni chaguo la mwisho kabisa ktk orodha ya vyakula, kwa huku Pwani kidogo ndio yana soko kiasi. Soko la magimbi lipo ila sio la scale kubwa kivile. Magimbi hayasumbui kabisa, kwa hiyo soko likiwapo la uhakika, ni option nzuri.
Sasa hivi jamii inabadirika sana, waliokuwa hawali ugali sasa wanachapa sembe, kama uonavyo, mihogo ilikuwa kwa ajili ya wachache ukanda wa pwani, sasa hivi mhogo ni dhahabu.
Kama upo Mkuranga, hakikisha shamba lako lina maji ya kutosha, udongo wa kilimo.
Nashukuru sana mkuu, nina uhakika somo litapanda sana, nitakucheki nikishaandaa shamba!