Magezi bugaga
JF-Expert Member
- Jul 7, 2021
- 1,181
- 1,594
1. Sesa itapendeza kupata mavuno zaidi mstari hadi msitari 40 CM, mmea hadi mmea 10 cm Kwa kukadilia 2. Booster tafta zenye kuanzia 45% high potassium piga mara 4 3. Sumu nzuri tumia combination ya cypermethrin+ chlorpyrifos + LambdacyhalothrinWakuu salaam,
Natumaini mapambano yanaendelea.
Ninaomba kuelimishwa mambo yafuatayo katika kilimo cha maharage msimu huu.
1.Jinsi ya kupanda kwenye matuta au Sesa
2.Busta nzuri inayofanya vizuri kwenye maharage,hapa naomba mwenye kujua zaidi kuhusu hizi busta ambazo zinafanya vizuri maana hapa ndo kila kitu.
3.Sumu inayofanya vizuri kabla ya maharage kuweka maua
4.Sumu ambayo itafaa baada ya maharage kuweka maua ambayo haitakuwa na harufu kali kufukukuza nyuki.
5.Dawa ya ukungu inayofaa katika maharage
6.Dawa nzuri ya kuzuia magugu kabla ya kupanda.
Asanteni kwa mchanganuo mtakao nipa.
Nalimia wilaya ya Tanganyika Katavi.
Sent from my SM-A045F using JamiiForums mobile app
Kuhusu nyuki kipindi Cha wiki mbili za Maua kuchanua uwa utakiwi kuingia shambani kuepusha kupukutisha Maua hivyo zoezi la dawa ufanyika kabla ya maua kuanza mara nyingi maeneo ya joto ni wiki nne hadi tano tangu maharage kuota.
5.dawa za ukungu tumia hexaconazole au chlorothanolin hizi ni zile za maji Zina ufanisi mkubwa
6. Dawa unaweza tumia paraquat kuunguza majani kwani hii inafanya kazi Kwa mguso katika uso wa Jani ila kama shamba limeandaliwa vizuri aina haja kutumika .hipo cleanbeans ila inaitaji umakin wakati wa kutumia .
Pia unaweza kuainisha visumbufu Kwa zao la maharage katika ukanda huo Ili kuweza kusaidiwa zaidi pia matumizi ya mbolea nayo ni muhimu.