Hii ndo habari njema wakuu!
Mimi nalima harage ya njano. Nalima kwa surface irrigation (furrow method)
Njia hii utaimudu kwa ufasaha kulingana na muonekano wa shamba lako. (natoa huduma hii kwa mhitaji).
Huwa nalima kwa mahesabu make mi ni mwanahesabu tangu kuzaliwa kwangu;
Hiki ndicho nifanyacho:
1) Ekari1 huwa naigawa kwa mistari5 iliyo sawa;
Kawaida 1acre=>4000sqm. Kwahiyo basi
4000/(8m*2m)*10kg*2000Tsh@kg= Tsh5,000,000
Katika hesabu hii:
4000sqm ni eneo lote la ekari kwa square mita.
8m ni urefu wa kila kijaruba kwa kipimo cha mita.
2m ni upana wa kila kijaruba kwa kipimo cha mita
10kg ni uhakika wa mavuno ya kila kijaruba.
2000Tsh ni kiasi cha bei ya maharage ya njano kwa kila kilo.
Tsh 5,000,000/= ni mapato ya jumla katika kila ekari.
Ufuatao ni mchanganuo wa gharama ya hiki kilimo kwa ekari moja kulingana na eneo la kilimo kinapofanyika na msimu husika hasa kipindi cha jua kali.
1) Natumia 6ltr@acre
2) kawaida namwagilia mara 10 mpaka kuvuna maharage kulingana na hali ya hewa.(6ltr*10=2500*6*10=>150,000/-)
3) natumia mbolea ya CAN Kg50@are=>Tsh90000
4) Tsh 200,000 kulima na kuchora muelekeo wa utiririkaji wa maji.
5) Booster 2ltr@6000=>12,000
6) Fungicide=>40,000
7) Insecticide=>48,000
8) Mbolea supergro tsh 250,000.
9) Palizi nafanya mwenyewe
10) Navuna na kupokea mkwanja nikiwa shamba. Siku hiyo lazima nichinje jogoo kwajili ya mteja!
Karibuni sana shamba. Ukiamua kuchagua upande huu utakuwa njia sahihi.
Usimtegemee mwajiri wako maana anakutumia kwa ujira finyu na ukizeeka hatakuhitaji kamwe.
Janjaruka mwanangu usiwe poyoyo!!