Mimi nayalima ila nayalima kienyeji.
Gharama zake ni kama ifuatavyo
Kugeuza eka moja no 30,000
Kuotesha eka moja in 30,000
Kupalilia eka moja 30,000
Kila eka moja debe moja LA kg 20 linatosha
Kungoa maharage eka moja ni 10,000
Kupiga maharage ni 5000 KWA gunia, ambapo mara nyingi navuna gunia tatu(gunia LA 120 kg) hivyo kupiga 15,000 KWA eka
Mbegu nzuri ni ile ya gololi mana kuna njano ndefu na njano gololi
Kusafirisha kutoka shambani mpaka store kwangu ni 5000 KWA gunia
Soko langu mi huwa nauzia mashule KWA kg 2,500au2600 KWA kutumia kampuni yangu, ( nilisajili purposely KWA kuwa madalali wanaonea sana)
Shamba huwa sikodishi, naombaga tu MTU mmmoja Mmoja mpaka nafikisha ekari kumi ama kumi na tano tu, watu Wa huku hawakodishi mashamba, ila ukitaka unanunua sukari na blanket unaenda kuomba Shamba, ukiahapata hapo utalima mpaka atakapokuambia sasa nataka Shamba langu. (Advantage ya kuajiriwa kijijini)
Kuotesha ni kuanzi mwezi Wa tatu tarehe moja hadi tarehe 15, na ukichelewa sana basi ivuke tare 05/4 hujaweka mbegu chini
Maharage ya njano hayahitaji mvua nyingi sana na yanawahi kustawi haraka mno,
Ni matamu sana yakiwa mabichi, matamu mnooo, yaani matamu haswaaa sema ushuzi wake sio Wa nchi hii.
Nimeshaanda mashamba nasubiria march niweke mbegu chini.
Mi huwa nachanganya na mahindi pia shambani. Sipigi dawa yoyote ile
Nafanyia mkoa Wa Arusha.
Sent using
Jamii Forums mobile app