Baada ya kusoma kuhusu kilimo hiki humu ndani nimeamua kujaribu
Nimekodi shamba sehemu za Kilombero Morogoro pembeni ya mto Ruaha.Mto ambao unatoa umeme wa kidatu. nimeshalima na andaa kuchimba kisima au naangalia uwezekano wa kutumia maji ya mto.
Tatizo ni mbegu.Kariakoo zinauzwa 15,000/ kwa pkt moja ya gramu 5 na ktk kuulizia nimeambiwa zipo 50 tu.Sasa kwa eneo nililoandaa kama eka 2 naweza kupanda roughly miche 1000.
Je kuna sehemu ambayo naweza kupata mbegu nzuri Malkia F1 kwa gharama ndogo kdg? au nitengeneze mwenyewe toka mapapai ya kisasa yaliyokomaa?