Kilimo cha Mapapai: Ushauri wa Kitaalamu, Changamoto na Masoko yake

Kilimo cha Mapapai: Ushauri wa Kitaalamu, Changamoto na Masoko yake

Mkuu naomba recommend supplyer wa uhakika kwa hapo Kariakoo kama kuna unayemjua, bei ya mche mmoja shilingi ngapi?
Kariakoo wanauzi mbegu. Sio miche. Miche sikushauri. Unaweza kuuziwa miche dume.
 
Na mimi nimeanza baada ya kushawishika na hii thread...

bfeb72976792997b065184c8ecf054ee.jpg

Ila sijui kama hayo mabaka ni kawaida. Hope nitashauriwa hapa
 
Nashukuru mkuu, nitazijuaje mbegu ambazo siyo dume?

Ukinunua mbegu ambazo ni Hybrid F1 kunakuwa na mchanganyiko wa majike na hermaphrodite (Ina sehemu ya kike na kiume) ambayo yote yanazaa matunda mfano sinta F1
 
Ukinunua mbegu ambazo ni Hybrid F1 kunakuwa na mchanganyiko wa majike na hermaphrodite (Ina sehemu ya kike na kiume) ambayo yote yanazaa matunda mfano sinta F1
Ahsante mkuu, hivi ninaweza kuweka maembe na mapapai shamba moja?

Yaani upande huu mapapai upande huu maembe.
 
Hapana Mkuu, hapo sina utaalamu. Ngoja wataalamu waje.

Kwa ufahamu wangu utapata matunda ktk miti yote. Jambo muhimu Sana ktk mbegu za kununua omba ushauri kabla ya kupanda Na wauzaji wengine hawafahamu.

Ukinunua ziweke ktk maji Kwa siku tano huku ukibadili maji hayo kila siku. Baadaye weka ktk kitambaa chenye unyevu Kwa muda wa siku tatu ndio unaweza peleka kwenye viriba. Vinginevyo mbegu nyingi hazitaota hata kama utamwagilia Kwa miezi matatu!
 
Na mimi nimeanza baada ya kushawishika na hii thread...

bfeb72976792997b065184c8ecf054ee.jpg

Ila sijui kama hayo mabaka ni kawaida. Hope nitashauriwa hapa

Mkuu hongera unayo mingapi? kuhusu mabaka labda sijayaona au ni uelewa wangu finyu ktk eneo hili, vinginevyo naona unaendelea vizuri.
Jambo la mwisho unatumia dawa gani kukinga Na au kupambana Na wagonjwa?
 
KUmbuka kuwa inakadiriwa kuwa Gramu moja ya mbegu za papai inakuwa na mbegu kati ya 45 na 50. Hivyo uwe makini unapotaka kunua kwa gramu au kwa idadi ya mbegu. Kwa hekta moja utahitaji takriban gramu 80 za mbegu za mipapai ambayo ni hermaphrodite
 
Kariakoo wanauzi mbegu. Sio miche. Miche sikushauri. Unaweza kuuziwa miche dume.
Mkuu umenena vyema, kununua miche mara nyingi utapata hadi asilimia 30 madume ambayo Kwa hakika ni hasara kwani unatumia muda wa hadi miezi mitatu kubaini kama ni dume ilihali umepoteza raslimali nyingi.

Acha story za kufunga magunzi ya mahindi au kukata eti itabadilika, haina ukweli.
 
Aiseee bora ufate ushauri wa shossi,mche m1 wa mpapai ni kama buku hivi mikubwa ila ukinunua unaweza ukakuta yote mipapai dume haizai inatoa maua tu na huku uswazi wanasema unafunga bunzi la muhindi zen unabadilika sijui kama it works!
mpapai dume dah nimecheka sana japo nina maumivu
 
Mkuu hongera unayo mingapi? kuhusu mabaka labda sijayaona au ni uelewa wangu finyu ktk eneo hili, vinginevyo naona unaendelea vizuri.
Jambo la mwisho unatumia dawa gani kukinga Na au kupambana Na wagonjwa?

Mkuu,

Kuna mtaalam mmoja kaniambia tuipige dawa wiki hii mwishoni. Nitakueleza dawa atakazonambia nikanunue.

Nimepanda miche 14 nyumbani, pamoja na mipera bila kusahau mastaferi.

Tafakari.
 
Back
Top Bottom