Upiversity
JF-Expert Member
- Jun 19, 2015
- 3,487
- 2,632
......teh heh heh..acha nadharia;unaona watu wanatoa "majibu rahisi" wakati wewe ndo umekuja na mchanganuo urojo kabisa!!!hivi kwa nini tunatoa majibu rahisi tena ya kushindwa na kuwakatisha wengine tamaa? yaani majibu yote yaishie kwenye soko kweli? hakuna sababu nyingine? au hakuna kweli mafanikio katika kilimo hicho?
aliye leta mada kasema kwa mwaka tunaweza kupata kwa mti mmoja zaidi ya papai 250 ambazo sawa na papai 300,000 ambazo zinaweza kuleta pato la shillingi 150,000,000/- kwa mwaka. hivi kweli na hili ni la serikali? hata iweje gharama za uendeshaji hazizidi 50,000,000/- hilo pato bado?
tabu iko wapi kuajiri watu ukagawana nao hiyo mia iliyobaki?
nauhakika nyumba kwa nyumba ukiuza kwa mia tano wateja utapata. huku niliko wakati mwingine papai linauzwa mpaka shillingi 3000.
ijulikane kuwa tunapozungumzia soko tunazungumza zaidi katika vitu vikuu viwili uhitaji wa soko na pia wauzaji au wasambazaji wengine na hapa ndipo tunaweza kuweka bei ambayo itaweza kulipa.
mimi nauhakika soko lipo na la kutosha tabu bado hatujajibidisha katika kulifanikisha mfano jiji la dar peke yake lina watu 6,000,000 ambao hawawezi kushindwa kula mapapai 300,000. ambalo pato tunaliona pale juu.
tujenge ushawishi kwa mfano kwa mwenye matatizo ya kupata choo au anasikia maumivu wakati wa aja kubwa akila papai kila siku hiyo hali inaweza kuondoka.
kiukweli bado hatujafanya matangazo ya kutosha mfano hakuna hata tangazo moja la tv linalotangaza zao kama hilo hebu fikiri unaweza pata milioni 150 unashindwaje kufikiria kugharamia matangazo kwa milion 15?
yapo mengi ya kuelezana lakini kwa leo ni hayo
....tufanye hivi,anza wewe wengine tutafata,kwani wewe hutaki hela?????