Kilimo cha Mapapai: Ushauri wa Kitaalamu, Changamoto na Masoko yake

Kilimo cha Mapapai: Ushauri wa Kitaalamu, Changamoto na Masoko yake

hivi kwa nini tunatoa majibu rahisi tena ya kushindwa na kuwakatisha wengine tamaa? yaani majibu yote yaishie kwenye soko kweli? hakuna sababu nyingine? au hakuna kweli mafanikio katika kilimo hicho?

aliye leta mada kasema kwa mwaka tunaweza kupata kwa mti mmoja zaidi ya papai 250 ambazo sawa na papai 300,000 ambazo zinaweza kuleta pato la shillingi 150,000,000/- kwa mwaka. hivi kweli na hili ni la serikali? hata iweje gharama za uendeshaji hazizidi 50,000,000/- hilo pato bado?

tabu iko wapi kuajiri watu ukagawana nao hiyo mia iliyobaki?

nauhakika nyumba kwa nyumba ukiuza kwa mia tano wateja utapata. huku niliko wakati mwingine papai linauzwa mpaka shillingi 3000.
ijulikane kuwa tunapozungumzia soko tunazungumza zaidi katika vitu vikuu viwili uhitaji wa soko na pia wauzaji au wasambazaji wengine na hapa ndipo tunaweza kuweka bei ambayo itaweza kulipa.
mimi nauhakika soko lipo na la kutosha tabu bado hatujajibidisha katika kulifanikisha mfano jiji la dar peke yake lina watu 6,000,000 ambao hawawezi kushindwa kula mapapai 300,000. ambalo pato tunaliona pale juu.
tujenge ushawishi kwa mfano kwa mwenye matatizo ya kupata choo au anasikia maumivu wakati wa aja kubwa akila papai kila siku hiyo hali inaweza kuondoka.
kiukweli bado hatujafanya matangazo ya kutosha mfano hakuna hata tangazo moja la tv linalotangaza zao kama hilo hebu fikiri unaweza pata milioni 150 unashindwaje kufikiria kugharamia matangazo kwa milion 15?
yapo mengi ya kuelezana lakini kwa leo ni hayo
......teh heh heh..acha nadharia;unaona watu wanatoa "majibu rahisi" wakati wewe ndo umekuja na mchanganuo urojo kabisa!!!
....tufanye hivi,anza wewe wengine tutafata,kwani wewe hutaki hela?????
 
Habari wadau, nimevutiwa na maelezo ya kutosha kuhusu kilimo hiki na nilikuwa natamani sana kulima ila sikuwa na abc zake. Sasa naomba kuuliza je nikianza taratibu za kulima kuanzia January hii ni muafaka kwa hali ya hewa ya sasa na baadae kwa maneno yenye tija ??? Ni hapa hapa dar es salaam
 
Mada hii ilinivutia nikafanya majaribio Na sasa naweza kuripoti.
IMG_20170125_093838.jpg
 
Changamoto kubwa kwa sasa katika kilimo cha papai ni huyu mdudu anayeitwa papaya mealybug ambaye huweka utando mweupe kama pamba hivi. Huyu akivamia anaharibu kabisa ubora na kumdhibiti ni vigumu. Nitachangia baadae namna tegemeana za kuudhibiti. Yaelekea waliolima wote humu hawajakutana na changamoto hii
 
Leta mrejesho mpendwa. Mimi nimefanya majaribio nyumbani, na sasa nimeotesha miche 100 shambani tayari kwa kuanza mradi. Nitaangalia hiyo 100 itakavyokuwa halafu nikimudu nitaongeza miche baadae. Ila nimeanza na mbegu za kawaida ambazo zinadumu pia, zinachelewa kutepeta - ganda ni gumu. Za kisasa nimepata kidogo ziko ghali sana madukani na niliwahi pata pakti zimesagika zimo 2 tu. Huu uzi umenisaidia sana. Asanteni.


Mkuu mrejesho vipi. Tuambie kilichojiri
 
Changamoto kubwa kwa sasa katika kilimo cha papai ni huyu mdudu anayeitwa papaya mealybug ambaye huweka utando mweupe kama pamba hivi. Huyu akivamia anaharibu kabisa ubora na kumdhibiti ni vigumu. Nitachangia baadae namna tegemeana za kuudhibiti. Yaelekea waliolima wote humu hawajakutana na changamoto hii
Mkuu unavyosema ni kweli, nikitembea maeneo mengi naona shida hiyo. Mimi Nina miti kama 60 hivi. Hivi karibun nilipata miti mwili ikiwa na ugonjwa huo.

Nilichofanya ni kuchanganya dawa aina ya Victory 72 Na farm guard, nikarudia baada ya siku mbili lkn safari hii nilatumia Victory pekee. Naweza kuthibitisha kuwa nimetibu.
 
Wakuu kwa sasa hivi mche mmoja ni shilingi ngapi? Nikiwa maeneo ya Iringa naweza wapi kupata miche mizuri?
Naweza kuchanganya nusu mapapai na nusu maembe katika shamba moja?

Natanguliza shukrani
 
Hello. Miche hi i mifupi n.a. yenye Papai nyingi hivi mbegu nazipata wapi Jamani nataka nianze kilimo hiki bagamoyo. Mama mtu mzima mimi
 
Back
Top Bottom