asante sana johnmashilatu, bado naendelea kupata ushauri maana sina uzoefu na ili ila nashikuru naanza kupata pichaKaribu sana.
Nina uzoefu kidogo Wa hii kitu. Sio kusomea nimefanya mwenyewe. Leo tuongelee mbegu.
Nakushauri nunua mbegu dukani zina Faida zaidi ya kuchukua za waitikaji au kula Papai na kuchukua mbegu
Ukinunua ziweke ktk maji kwa siku tano lakini badili Maji kila siku. Baada ya siku hizo zifunge ktk kitambaa kwa siku tatu.
Ukimaliza weka kwenye viriba ndio utapata matokeo mazuri. Nilinunua red royale f1, muuzaji hakunipa maelekezo hayo haikuota hats moja!
Uzoefu wangu unaonyesha kuwa Miche inayouzwa kwenye vitalu vingi haina u ora lakini kubwa utapata madume 20- 30 katika miti 100. Hii ni hasara kubwa.
Nunua mbegu kwenye maduka ya pembejeo zinauzwa kuanzia she 5000 had 16000.
Karibu na jipange kufanya kazi sio kutumia simu kufanya Kilimo.