Habari wanajukwaa mimi ni kijana nimeamua kujihusisha na kilimo.
Nakusudia kulima papai mapema mwakani na nimedhamiria kuwa na mipapai takribani mia saba.
katika hiyo mia saba, mia tatu nakusudia kuifanyia kilimo cha umwagiliaji na ilobaki kilimo cha kutegemea mvua.
ENEO LA KILIMO, Nakusudia kulima kijiji cha SEGERA wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.
HITAJIO KUU: Nahitaji kujua wapi ntapata Soko la uhakika na aina gani ya papai inapendwa Sokoni.
Karibuni wadau. Michango yenu katika hili ni muhimu sana kwa kijana mimi nlie hamasika na kilimo.