Kilimo cha Mapapai: Ushauri wa Kitaalamu, Changamoto na Masoko yake

Kilimo cha Mapapai: Ushauri wa Kitaalamu, Changamoto na Masoko yake

View attachment 668977 wadau wengi nimeona unaulizia upatikanaji wa mbegu jamani mbegu zipo madukani tembelea duka lolote la pembe jeo na mifugo ulizia mbegu ya papai hybrids , utapewa kazi ni kwako kuchagua unataka mapapai yepi yenye rangi nyekundu, karogi nk ni wewe tu

Mbegu hii huitaji kuiotesha wewe ni kuandaa mashimo vizuri kisha kuipanda nakuanza kuitunza tu

Hiyo mipapai katika picha ina miezi sita tu

Soko la papai lipo na kubwa tu sema watu hawastukia , unaweza tengeneza soko lako mwenyewe kwa kuwauzia mama lishe wa mitaani, pia katika hotel, pia katika hospital za mikoa, wilaya nk , haitaji utoe zao lako mkoani kupeleka dar hapo hapo ulipo unaweza fanya biashara

Wazo hili nilitoa hapa hapa JF nikalifanyia kazi na limezaa matunda, napokea sm kila siku watu wakitaji mapapai sababu ishajulikana namiliki mipapai kila mwezi na uhakika wa kutengeneza laki tano

Bei ya mbegu za hiyo mipapai inanzia elfu therathini na tano, inategemea na eneo ulilipo
Mkuu, mbegu kiasi gani?
 
mkuu mara nyingi wakulima huuza papai kwa maana ya kupeleka kama matunda sokoni. kuna kitu wanaita "papain" ukiweza kuigema ukapata soko zuri itakusaidia. pia yale ambayo hayako kiwango cha kuleta bei nzuri sokoni unaweza ukakausha. TATEDO wabatecnolojia hiyo. wabakutegenezea kaushio la matubda.
 
Habari wanajukwaa mimi ni kijana nimeamua kujihusisha na kilimo.

Nakusudia kulima papai mapema mwakani na nimedhamiria kuwa na mipapai takribani mia saba.

katika hiyo mia saba, mia tatu nakusudia kuifanyia kilimo cha umwagiliaji na ilobaki kilimo cha kutegemea mvua.

ENEO LA KILIMO, Nakusudia kulima kijiji cha SEGERA wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.

HITAJIO KUU: Nahitaji kujua wapi ntapata Soko la uhakika na aina gani ya papai inapendwa Sokoni.

Karibuni wadau.
michango yenu katika hili ni muhimu sana kwa kijana mimi nlie hamasika na kilimo

Mbeya mapapai matamu adimu sn kama ya kwako ni matamu nafikiri ukileta yatakuwa na soko sn jaribu kufuatilia...
 
Habarini wapendwa,
Nimejaribu kuotesha mapapi ila kidogo napata shida maana sina uzoefu kutokana na baadhi ya mabadiliko ninaokumbana nayo.
Naomba mwenye uzoefu tusaidieane pliz

Kama mnanyoona hapo kwenye picha kuna rangi ya kahawia kwenye maua sasa nimeshindwa nitumie dawa gani ili niweze kuzistawisha na kuzirudisha kwenye hali yake.mara ya mwisho nilipiga booster ya d1 grow red kutoka dyna pharm
Naomba msaada wapendwa kwenye hili plis dawa nzuri ya kuuua wale vidudu vyeupe kwenye machungwa ambayo vinayafanya yawe mweusi.
Regards
Dave
20180415_102312.jpg
20180411_113939.jpg
 
Kwa faida ya wengine tumia mbolea npk kiasi kikasha cha kibiriti .hii inasaidia kufanya Papai kuwa na shepu na tunda kuwa kubwa weka kila mwezi Mara moja na maji ya kutosha
 
Ingia facebook kuna group la wakulima wa mapapai wanatoa maonibyao ya kutosha ila ni wakenya...lugha kubwa ilingishi
 
Kwa faida ya wengine tumia mbolea npk kiasi kikasha cha kibiriti .hii inasaidia kufanya Papai kuwa na shepu na tunda kuwa kubwa weka kila mwezi Mara moja na maji ya kutosha

Nshukuru sana kiongozi nipo kwenye msiba nikiwa kwenye utulivu ndo ntakuchek.ila kwa faida ya wote hujataja aina gan ya mbolea na kwa kiasi gan unaweka
 
Ingia facebook kuna group la wakulima wa mapapai wanatoa maonibyao ya kutosha ila ni wakenya...lugha kubwa ilingishi
Thanks mkuu.hilo group linaitwaje maana nimesearch ila sijalipata labda unipe the actual group name.
 
Nshukuru sana kiongozi nipo kwenye msiba nikiwa kwenye utulivu ndo ntakuchek.ila kwa faida ya wote hujataja aina gan ya mbolea na kwa kiasi gan unaweka
Nimeonanni npk na kiasi ni size ya kiberiti. Kwa hizi mvua haitaleta shida?
 
Nshukuru sana kiongozi nipo kwenye msiba nikiwa kwenye utulivu ndo ntakuchek.ila kwa faida ya wote hujataja aina gan ya mbolea na kwa kiasi gan unaweka
Kataja NPK, hii kitu ina Nitrogen, Phosphorous na Potasium
 
Mkuu mimi nimeona bora nikutumie documents za kilimo cha mpapai zina mambo yote ya msingi kuhusu kilimo hicho na magonjwa yake na jinsi ya kuyatibu natumaini itakusaidia.


KILIMO BORA CHA PAPAI





Utangulizi:

Mipapai ni moja ya miti ya matunda inayolimwa ulimwenguni kote na hapa Tanzania, miti hiyo inalimwa karibu kila mahali.

Mipapai au kwa jina la kitaalam Carica papaya, ni miongoni mwa spishi 22 zinazokubalika katika jenasi ya Carica na familia ya Caricaceae.

Asili ya mipapai ni katika maeneo ya tropiki huko Amerika, pengine kusini mwa Mexico na nchi kadhaa za Amerika ya Kati.

  • Tunda la papai lina sukari, Vitamini A na C kwa wingi na huweza kuliwa kama tunda. Pia huweza kutengenezwa saladi, jamu na kukamuliwa kupata juisi.
  • Utomvu wa papai bichi hutumika kulainisha nyama na kutengeneza dawa mbalimbali.
Mazingira:

Ingawa asili ya zao hili ni kusini mwa Mexico (hasa maeneo ya Chiapas na Veracruz), Amerika ya Kati, na kaskazini mwa Bara la Amerika ya Kaskazini, kwa sasa mipapai inazalishwa kwa wingi katika nchi za kitropiki duniani.

mipapai huanza kuzaa miaka mitatu tangu kupandwa shambani. Hata hivyo, ni zao ambalo halihitaji unyevu mwingi na ndiyo maana linalimwa zaidi kwenye nchi za kitropiki ambako kuna joto.

Mipapai huhitaji jjoto la wastani kati ya nyzi 22 na 26 za Sentigredi na mvua kiasi cha milimeta 1,000 na 1,800 kwa mwaka. Zao hili linastawi vizuri kwenye udongo usiotuamisha maji kwani yakisimama kwa saa 48 tu mpapai unaweza kufa, wenye rutuba ya kutosha kwani mipapai haina mzizi mrefu, haihitaji udongo wenye kina kirefu na lazima udongo uwe na uchachu kati ya pH 6 na pH 7.

Upepo mkali huangusha mipapai, hivyo inashauriwa kupanda miti pembeni mwa shamba la mipapai. Inashauriwa kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka shamba lako, miti kama miparachichi, migravilea, vibiriti (leucaena Spp) na miembe pia inafaa. Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai kwa mita 10 mpaka 20 juu zaidi.

Kipindi cha jua kali mpapai usiachwe zaidi ya wiki 8 bila kumwagiliwa maji kama hakuna mvua ingawa wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hii huongeza ubora wa papai ikiwemo kutooza mapema sokoni.




Usipande mipapai mfululizo kwenye shamba moja kwa zaidi ya miaka mitano kwa sababu hiyo inaweza kusababisha usugu wa magonjwa. Unahitaji kubadilisha mazao japo kwa msimu mmoja ili kuua mzunguko wa magonjwa.

Mipapai inaweza kuchanganganywa na miembe na mimea jamii ya michungwa, pia mazao ya msimu kama mahindi, mtama, ufuta, alizeti na mboga mboga yanaweza kulimwa.




Aina za mipapai:

Kwa kawaida kwenye mipapai kuna mipapai ya jinsia tatu: midume, majike na yenye jinsia zote (hermaphrodite) ambayo huwa na mapapai marefu zaidi, na pia kuna isiyoeleweka ambayo huwa na mapapai mafupi sana.
Papai dume hutoa poleni peke yake, siyo matunda.



Papai jike linaweza kuzaa matunda madogo, yasiyolika ikiwa halikuchavushwa.

Mpapai wenye jinsia zote mbili unaweza kujichavusha wenyewe kwa sababu maua yake yana stamens za kiume na mayai ya kike. Kwa kawaida bustani nyingi za mapapai ya biashara zina miti yenye jinsia zote, yaani hermaphrodite.


kuna aina nyingi za mipapai lakini zinazolimwa zaidi nchini Tanzania ni aina ya Solo, Hortus Gold na aina za kienyeji.

Solo ni aina ya mipapai ambayo maua yake yana mbegu za kike na kiume katika ua moja. Mapapai ya Solo yana umbo lililochongoka kidogo mfano wa yai au kama tunda la peasi na nyama yake ni nyekundu. Matunda yake hukua hadi kufikia uzito wa nusu kilo.



Hortus Gold ni aina ambayo mbegu za kiume na kike zinapatikana katika maua tofauti lakini katika mmea mmoja. Rangi ya nyama yake ni ya dhahabu na matunda yake hukua hadi kufikia uzito wa kilo moja na nusu mpaka kilo mbili. Mapapai ya Solo ni matamu zaidi kuliko ya Hortus Gold na ndiyo yenye soko kubwa.



Utayarishaji wa shamba:

Shamba litayarishwe mwezi mmoja kabla ya kupanda. Wakati wa kutayarisha shamba punguza miti, ng’oa visiki na fyeka majani, halafu yakusanye pamoja na yachome.

Chimba mashimo yenye ukubwa wa sentimeta 40 upana, urefu na kina. Nafasi kati ya shimo na shimo iwe meta mbili au tatu na mstari na mstari iwe meta mbili na nusu hadi tatu. Baada ya kuchimba mashimo jaza mbolea ya samadi au takataka zilizooza vizuri (mata mahuluku) kiasi cha debe mbili kwa kila shimo.




Upandaji:

Mbegu za mipapai zinaweza kupandwa moja kwa moja shambani au kuoteshwa kwanza kitaluni na baadaye miche kuhamishiwa na kupandikizwa shambani.

Kama zitaoteshwa kitaluni zipande katika nafasi ya sentimeta mbili na nusu kutoka shimo hadi shimo na sentimeta 10 kutoka mstari hadi mstari.

Mbegu za mipapai zinaweza kupandwa kwenye viriba vilivyojazwa mchanganyiko wa udongo na mbole za asili. Kwenye kila pakiti weka mbegu 2 – 3.

Kwa kawaida, mbegu huota baada ya wiki mbili na miche huwa tayari kupandikizwa shambani kuanzia wiki sita hadi nane ambapo wakati huo miche huwa na urefu wa sentimeta 20-40. Kama udongo unatuamisha maji panda kwenye matuta yenye urefu wa sentimeta 40 – 60.

yaliyokwishatayarishwa mapema. Mbegu nane zipandwe katika kila shimo maana miche mingine inaweza kufa kwa magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota dume.

Katika kuandaa mbegu, kusanya mbegu kutoka kwenye mapapai makubwa na yaliyokomaa na kuiva, kausha mbegu vizuri kabla ya kupanda. Kama utapata mbegu za kununua ni vizuri zaidi. Baada ya kukausha hakikisha unazipanda ndani ya wiki moja.




Utunzaji wa shamba la mipapai:

Kupunguza miche

Baada ya mbegu kuota, miche ipunguzwe na kuacha miche minne katika kila shimo. Maua yakishatoka mipapai isiyotakiwa. Baada ya miezi 3 – 5 tangu kupandwa shambani mipapai itatoa maua na hapo jinsia ya mipapai itajulikana na mingine itabidi ipunguzwe na hasa midume, mipapai yenye jinsi zote inatakiwa isizidi asilimia 10 – 20 na midume ibaki mmoja katika kila mijike 25. Kama umepanda aina ya mipapai ambayo maua yake yana mbegu za kiume na kike, ondoa mipapai yote ya kiume. Mimea yenye magonjwa pia inabidi ing’olewe.




Urutubishaji wa udongo

Ili mimea iweze kukua haraka, inashauriwa kuweka mbolea za kukuzia kama vile SA au Urea. Kiasi kinachotakiwa ni kilo 200 za SA au kilo 100 za Urea kwa hekta moja. Mbolea za asili kama vile samadi na mbolea vunde ziwekwe kila mwaka kiasi cha kilo debe moja hadi mbili kwenye kila mpapai ili kuongeza ukuaji na uzazi. Mabaki ya mimea yanaweza pia kuwekwa kama matandazo na h ii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu usipotee.




Palizi

Palizi katika shamba la mipapai ni muhimu hasa wakati wa mwanzo. Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka Ili kuzuia uotaji wa maggot. Magugu yang’olewe yakiwa machanga na epuka kuchimbua chini sana maana mizizi ya mipapai huwa juu juu. Njia nzuri Ni kuweka matandazo kwenye shamba lote Ili kuzuia uoataji WA maggot.

Mipapai iangaliwe dhidi ya magonjwa, ing’olewe na kuchomwa au kufukiwa chini ikiwa itabainika kuwa na magonjwa, piga dawa dhidi ya magonjwa ya fangasi na virusi mara yanapoibuka ili kuongeza uzaaji na kipato chako.

  • Ondoa matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai wako, na hii ifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.
  • Ondoa mapapai yote ambayo yatakuwa hayakuchavuliwa vizuri na acha yale yenye afya tu
  • Weka miti ya kuegemea kama mpapai utazaa matunda mengi na hasa wakati wa upepo mwingi ili kuzuia mipapai isivunjike
  • Mipapai ikitunzwa inaweza kuishi mika mingi, ila kwa ajili ya mazao bora ondoa mipapai na upande mingine baada ya kila miaka mitatu (3) kwani mpapai unapo kuwa mkubwa basi rutuba yote huishia kwenye mti wenyewe



Magonjwa na wadudu waharibifu:

a) Magonjwa

Mipapai hushambuliwa zaidi na magonjwa ya ukungu na virusi.

Magonjwa ya ukungu





Magonjwa ya ukungu huababisha majani na matunda kuwa na uyoga mweupe na madoa meusi ya mviringo. Mizizi huoza kutokana na athari za magonjwa hayo na mmea hufa.




Kuzuia

- Kupanda mipapai katika sehemu isiyotuamisha maji

- Kuweka shamba safi wakati wote

- Kuepuka kujeruhi mizizi wakati wa kupalilia

- Kubadilisha mazao

- Kunyunyiza dawa za ukungu kama vile Dithane M 45.




Magonjwa ya virusi





Magonjwa ya virusi husababisha mmea kudumaa, majani kukunjamana na kilele kuwa na kitita cha majani. Magonjwa hayo huenezwa na panzi na vijidudu aina ya vidukari.




Kuzuia

- Kutumia dawa kama vile Sumithion au Killpest ili kuangamiza wadudu wanaoeneza magonjwa hayo.




b) Wadudu waharibifu

Wadudu wanaoshambulia zaidi zao hili la mipapai ni vidukari na minyoofundo.




Vidukari

Vidukari hivi hufyonza utomvu wa majani.




Dalili

Mmea hudumaa.




Kuzuia

Nyunyizia mojawapo ya dawa kati ya Sumithion au Dimethoate.




Minyoofundo

Minyoofundo hushambulia mizizi na kuifanye iwe na nundunundu.




Kuzuia

Kubadliha mazao. Baada ya kung’oa mipapai panda aina nyingine ya mazao ambayo haishambiliwi na minyoofundo kama vile mahindi na mazao jamii ya mikunde.




Wadudu na wanyama wengine waharibifu ni ndege na panya.




Uvunaji:

Mipapai huanza kuzaa katika kipindi cha miezi minne had inane.

Mapapai kwa ajili ya matumizi ya nyumbani yavunwe wakati yanaanza kubadilika rangi kutoka kijani kibichi na kuwa njano. Mapapai kwa ajili ya kusafirishwa yachumwe yakiwa yamekomaa lakini bado yakiwa na rangi ya kijani.

Uvunaji wa mapapai ni wa kutumia mikono au kutumia vichumio maalum. Vuna mapapai na vikonyo vyake ili kurahisisha ubebaji na kuzuia kuingia kwa vimelea vya magonjwa. Weka mapapai kivulini baada ya kuvuna.

Mipapai iliyotunzwa vizuri inaweza kutoa tani 40 kwa hekta kwa mwaka kwa mzao wa kwanza na tani 25 kwa hekta kwa mzao wa pili. Mavuno hupungua katika mzao wa tatu na kuendelea.
 
Ule ni ugonjwa wa fangas chukua omo au hata sabuni ya maji changanya na maji kisha pulizia kwrnye majani siku 3 mfululizo mara 1 kwa siku....utaisha...
[emoji28][emoji28]Mkuu nisije ua miche yangu we nipe jina la dawa ya dukani maana mapapai yako so delicate
 
[emoji28][emoji28]Mkuu nisije ua miche yangu we nipe jina la dawa ya dukani maana mapapai yako so delicate
Wee mkulima muoga balaa...unajifunza kutokana na makosa...

madawa ya madukani hayo hapo umeandikiwa kwenye makala na mdau mmoja...

ila pia ukienda duka la kilimo watakuambia madawa yotee...

ila usisahau kabla hazijaanzisha hoapitali babu zetu walitibiwa na wengine walizaliwa kwa mbinu na medani za kimila za babu zetu.
 
Wee mkulima muoga balaa...unajifunza kutokana na makosa...

madawa ya madukani hayo hapo umeandikiwa kwenye makala na mdau mmoja...

ila pia ukienda duka la kilimo watakuambia madawa yotee...

ila usisahau kabla hazijaanzisha hoapitali babu zetu walitibiwa na wengine walizaliwa kwa mbinu na medani za kimila za babu zetu.
[emoji28] sina uonga mkuu sema naogopa nisije ingia cha kike
 
Jamani wandugu, naomba kujuzwa kiundani kuhusu kilumo cha kisasa cha mapapai. Nasukia kinalipa kweli.
 
Back
Top Bottom