Kilimo cha Mapapai: Ushauri wa Kitaalamu, Changamoto na Masoko yake

Kilimo cha Mapapai: Ushauri wa Kitaalamu, Changamoto na Masoko yake

Nafikiria sana niingie kwenye Biashara ya Kikimo 2019 kwa sasa nipo kwenye tafiti ya kusoma sana aina mbali mbali ya kilimo baada ya hapo nitafanya ziara kwa wakulima waliofanikiwa ili nipate ujuzi zaidi ili nitakapo ingia basi niwe na ABC ya kilimo husika kwa kuanza nipo kwenye utafiti wa kilimo cha Papai najua hapa nitapata wale ambao wapo kwenye kilimo hiki ni gependa sana kupata ujuzi toka kwao.

Pia si vibaya tukapeana mbinu za kilimo hiki, changamoto na nk.

Binafsi nimepitia bandiko moja mahali kuhusu kilimo cha papai.

Kama ifuatavyo:

Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia linawezakuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi.

Uzalishaji wa papai nchini Tanzania ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji ya watumiaji, hivyo inahitajika nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao hili.

Kijinsia mpapai umegawanyika katika aina tatu.

Mpapai wenye maua kiume tu. Mpapai wenye maua kike tu. Mpapai wenye maua ya jinsia zote (Hermaphrodite papaya).

Katika uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana uweza kujirutubisha wenyewe.

Kutokana na jinsia ya maua mpapai huweza kutengeneza matunda yenye maumbo tofauti. Matunda yanayotengenezwa kutoka katika mpapai wenye maua ya kike tu huwa na umbo la mviringo zaidi au yenye umbo la yai na matunda yanayotokana na mpapai wenye maua ya jinsia zote mbili huwa na umbo la refu zaidi au umbo la pear.

UZALISHAJI WA ZAO LA PAPAI.
Miche ya mpapai Katika uzalishaji wa miche ya mpapai kuna aina mbili za mbegu ambazo huweza kutumika:

1. Mbegu za Kawaida (Local seeds).
Hizi ni mbegu ambazo huweza kukusanywa toka katika mipapai ya kienyeji. Aina hii ya mbegu ni vigumu kujua kati ya mbegu ni ipi dume, jike ama yenye jinsia zote.

Hivyo itakulazimu kung'oa baadhi ya mipapai dume pindi itakapo weka maua hivyo kuacha majike na yenye jinsia zote mbili. Mapapi yenye maua ya kiume uachwa kwa uwiano wa 1:50 ya mipapai yenye maua ya kike.

2. Mbegu chotara (Hybrid seeds)
Aina hii ya mbegu ni nzuri kwa sababu mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye maua ya kike na ya kiume pamaja (Hermaphrodite papaya)na pia hukua haraka na kutengeza miti mifupi yenye uzao mkubwa ukilinganisha na ile ya kienyeji. Mfano. Red royolen F1 au MALAIKA F1.
UPANDAJI.

Panda mbegu moja tu kwa kila kiriba chenye udongo uliochanganywa vizuri na kujazwa robo tatu. Kisha weka viriba vyako venye mbegu chini ya kivuri kisha mwagilia maji. Baada ya kumwagilia unaweza pulizia kiasi kidogo cha kiuwatilifu (fungicide & Insecticide) kwenye udongo wako ili kuzuia wadudu na fungasi wasiathili mmea wako.

Mbegu ya papai uweza chukua siku 8 hadi 15 kuchomoza toka kwenye udongo. Hivyo hakikisha unamwagilia maji kila siku kwa kiasi. Usimwagilie maji mengi sana. Mpapai huweza kuamishwa toka kwenye kitalu baada ya wiki sita hadi nane.

KITALU CHA MIPAPAI NA BAADHI YA SABABU MUHIMU ZINAWEZA ATHILI UKUAJI WA MIPAPAI.
Mpapai upendelea zaidi udongo unaopitisha maji na mzuko wa hewa kirahisi na wenye makadilio ya Ph 6.5. Inapowezekana zuia kupanda mimea yako kwenye udongo wa mfinyanzi na wenye magadi. Kiasi cha maji kilichopo kwenye udongo huweza kuonyesha ukubwa wa matunda.

Eneo lenye udongo wenye unyevunyevu mwingi huweza tengeneza matunda makubwa na yaliyoja maji maji na eneo lenye unyevunyeku kidogo hutengeneza matunda madogo na magumu. Mpapai hawezi kuvumilia upepo mkali, maji yaliotwama pamoja na ukame.

UANDAAJI WA SHAMBA.
Njia ya kuandaa shamba itategemea na eneo (topography), aina ya udongo, vifaa vinavyotumika kuhudumia shamba. Nafasi kati ya mmea na mmea ni mita 2 hadi 2.5 na kati ya mstari na mstari ni mita 2.5 hadi mita 3.

Andaa mashimo yenye upana na urefu wa sentimita 60. Tenga udongo wa chini na wa juu. Kisha changanya udongo wa juu na mbolea ya samadi. Katika kurushisha kwenye shimo tanguliza udongo ulochanganywa na mbolea ya samadi chini na juu malizia na udongo uloutoa chini wakati wa kuchimba shimo.

Kiasi cha mmea huwa kati ya 1000 hadi 2000 kwa hekta (400 hadi 800 kwa ekari) Kupanda mimea shambani Baada ya hizo wiki sita hadi nane hamishia mimea yako shambani. Kazi ya uhamishaji wa mimea ufanyika wakati wa asubuhi sana, jioni ama kukiwa na mawingu ili kuzuia madhara ya jua kwa mimea.

UWEKAJI WA MBOLEA.
Zuia matumizi ya mbolea zenye chlorine maana mipapai uathiliwa na chlorine. Wiki moja baada ya kuhamisha miche yako weka mbolea gramu 28 kwa kila mche. Tumia mbolea yenye phosphate kwa kaisi kikubwa.

Mfano; - 12:24:12. (NPK) Baada ya hapo kila baada ya wiki mbili weka mbolea yenye Nitroni kwa kiasi kikubwa kiasi cha gramu 56 kwa mmea. Mfano. 20:10:10 (NPK) Potassium inahitajika kwa maua na kuweka matunda hivyo tumia mbolea yenye potassium kiasi kikubwa mara baada ya kuona mmea wako umeanza kuweka maua, kiasi cha gramu 114 cha mbolea huitajika, fanya hivyo kila baada ya mwezi. Mfano. 12:12:17 + 2 (NPK) . Weka mbolea ya majani yenye virutubisho vidogo vidogo ikiwemo boron kila mweze. Boron ni mbolea ya muhimu katika kupata matunda mazuri.

UMWAGILIAJI.
Maji ni sehemu ya muhimu sana katika maisha ya mmea kwa kipindi chote. Maji ni ya muhimu sana katika kuweka maua, matunda na ukuaji wa matunda. Katika ukuaji wa matunda hakikisha unaweka lita 23 kwa kila mmea kwa wiki.

Magugu Hakikisha unazuia magugu kipindi cha mwanzo ili kuzuia ushindani kati ya mimea na magugu kwa virutubisho na maji. Na pia kuzuia magugu kubeba vimelea na wadudu wanaoweza kuathili mazao yako.

HATUA ZA UKUAJI WA MPAPAI.

Kitalu - Wiki 1 - 6 -Hatua ya ukuwaji wa haraka baada ya kuamishiwa.Shamba - wiki 7 -16 -Maua na kuweka matunda.Wiki 17 - 21 -Kukua kwa matunda.Wiki 22 - 26 -Mavuno ya kwanza Wiki 37 -kuendelea Week 37 ni miezi tisa au kumi sio kwa hiyo kilimo cha mapapai huchukua miezi 10 kupata mavuno

GHARAMA

Kununua ekari moja inategemea na eneo ulipo na bei husika. Kununua mbegu tsh 50,000-100,000.Kumwagilizia kila siku -upandaji -kuhamisha kutoka kwenye vitalu hadi kwenye shamba -machine ya kumwagilizia 1,500,000/- Generator tsh lak 6 Mbolea tsh 100,000 kila mwez -na vibarua shambani -kulima kwa trekta 40,000 Gharama zote kama mil 3-4 hiv mpaka kuvuna.

MAVUNO NA FAIDA.
Kama umelima ekarI moja unaweza ukapata matunda 15- 35 kwa mvuno wa Kwanza tu twende kimahesabu EkarI ina miche 400-800 Tuseme tupate miche 600 kwa ekari, kila mche utoe matunda 20 chini kabisa 600×20=12,000.

Matunda Soko Kwa sasa unaweza ukauza kwa jumla jumla tsh 1000-3000 Tuuze kwa bei ya chini 1000 kwa kila papai 12000×1000=12,000,000/- Ukitoa Gharama za uendeshaji unaweza ukabaki na tsh 8,000,000.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kwa maarifa kiingozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii post ni ya mwaka 2011, ni miaka 8 sasa imepita Je kuna mtu alijaribu kilimo hiki - any feedback?
 
Lete mrejesho mkuu au Kama umekwama mahali niambie Mimi naendelea Kuna papai kila week
IMG_20190331_173728_2.jpeg
IMG_20190417_181555_0.jpeg
 
Bei ya papai hapa dar Ni sh 1500 bei kuuza kwa jumla
 
Acha kulalamika kwenye keyboard mkuu ,mi nalima papai huu mwaka wa tatu sijawahi kudodewa na papai .Kama unazo nikupe connection

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Naomba kujifunza zinastawi katika Mazingira gani (Udongo), gharama za Miche na madawa. Na Eneo la heka moja unaweza kupanda Miche mingapi. Bila kusahau inachukua muda gani Hadi kukua
 
Back
Top Bottom