Kilimo cha tikiti maji (water melon)
HALI YA HEWA.:
mimea hustawi katika maeneo yenye joto la wastani (haihimili hali ya joto Kali sana wala baridi sana), wala haihitaji mvua nyingi. na hata udongo unaotuamisha maji.
zao hili hustawi vizuri maeneo yenye joto la 21-30 centigrade, yakipandwa kwenye maeneo yenye joto chini ya 15c huchelewa kuota.
mvua inayohitajika kwenye zao hili ni 400-600mm/msimu.
Maeneo yanayofaa kwa kilimo hiki Tanzania ni Tanga,morogoro, Dsm,mtwara, lindi na pwani. ambako kuna jua la kutosha.
UANDAAJI WA SHAMBA
Unashauriwa kusafisha vizuri shamba lako na kutibua udongo vizuri ili kurahisisha mizizi kupenyeza kwa urahisi kwenye udongo pia kutunza maji.
UPANDAJI
tikiti hupandwa moja kwa moja kwenye shamba.hauruhusiwi kuoteshea mbegu kwenye kitalu kwa maana mmea huu hauna mizizi ya kustahimili kuhamishwa.., piga mashimo kwa umbali wa mita 1 shimo hadi shimo na mita 2 mstari hadi mstari., panda mbegu 2-3 ila uje upinguzie na kuacha mimea 2 tu,
UWEKAJI MBOLEA
weka mbolea aina ya NPK au DAP wakati mimea inapokua midogo kwa wastani wa gram 10-20 kwa shimo, utaweka mbolea kila wiki Mara 1-2 hadi pale mmea utakapoanza kutoa maua jike ambapo utabadilisha mbolea na kutumia mbolea aina ya urea kwa wiki Mara moja.
UMWAGILIAJI
usimwagilie matikiti muda wa jion kwan utapelekea unyevu kudum kwa muda mrefu na hatimaye kurahisisha magonjwa.
WADUDU NA MAGONJWA
wadudu aina ya green peal aphids hushambulia sana zao hili, hupenda kujishkiza sehem ya chini ya jani na kuathili majani, utaona majani yanajikunja kabisa.ni vijidudu vidogo mfano wa utitiri., utakapoona vimeanza kushambulia wahi mapema kunyunyizia dawa aina ya Multimectin au Atakan Au hata farmguard, dawa hizi ndio hunesha ufanisi mzuri kuwaangamiza wadudu hawa kwa haraka .ila pia ni bora kupiga sumu ya wadudu kati ya izo apo juu kwa kila wiki walau Mara moja ili kuzuia wadudu .,
UKUNGU
ni ugojwa ambao hushambulia zao hili hasa wakati wa mvua au Baridi, utapiga dawa aina ya mancozeb au blue copper au nyingine yoyote ya ukungu, pia ni vema kupiga dawa ya ukungu kwa kila wk Mara moja ili kuzuiya tatizo hili.
sory: kwa eka moja utatumia mbegu gram 200 hadi 300, mbegu inayoshauriwa now zile za hybrid (f1), ni zile za zebra na nyingine ni kama kombati, aina Hz ndio zinapendwa sana na wateja, ..
tikiti huchukua miezi 2 -2.5 tangu kupanda hadi kuvuna.
MAVUNO
ikihudumiwa vizuri inaweza kutoa tani 10-14 kwa ekari moja,
tikiti huuzwa kwa kilo ambapo kilo moja huuzwa kati ya 250-400 kwa bei ya shambani........
kama utakua na swali waweza uliza ....