GHARAMA KUBWA IKO KWENYE MBEGU, GRAM 250 ZA KUTOSHA EKA 1 ITAKUGHARIMU KATI YA 1110,000-140,000, GHARAMA NYINGINE NI YA MAJI (KAMA UTATUMIA PUMP, SO GHARAMA YA MAFUTA) KUTEGEMEA NA PUMP UTAKAYOKUWA NAYO UNAWEZA JIKUTA KWA SIKU UNATUMIA MPAKA LITA 7-10, SASA ZDISHA KWA BEI YA FUEL YA SASA MARA SIKU 70 ZA KUKAA SHAMBANI, SAMBAMBA NA HILO JE PUMP YA KUMWAGILIA NI YAKO.. KAMA NI YA KUNUNUA SI CHINI YA LAKI3 PUMP NZURI, YA KUKODI KWA MUDA WA MIEZI 3 HIYO SI CHINI YA LAKI 2. KUTEGEMEA NA MSIMU ULIOLIMA (JE NI WA JUA AU MVUA??) KAMA NI WA MVUA GHARAMA NYINGINE ITAKUWA KATIKA MADAWA YA UKUNGU NA WADUDU. KWA UCHACHE KABISA GHARAMA YA EKA 1 YA TIKITI MPAKA UNAVUNA ITAKUGALIMU SI CHINI YA MILIONI 2, GHARAMA NYINGINE NI MBOLEA UTAHITAJI MIFUKO MIWILI YA DAP=180,000, UTAHITAJI UREA MIFUKO MIWILI 140,000TSH, UTAHITAJI NA CAN YA KUMALIZIA MIFUKO 3 TSH 210,000 ETC...... KILIMO NI GHARAMA HIVYO NI VYEMA KUJIPANGA VIZURI, ANDAA 2.5 MILIONI NDIO UINGIE SHAMBA.