Mtu wa Kigamboni
Member
- Jul 24, 2015
- 80
- 38
Mimi nina kisima cha pump ya umeme ninataka kutumia mpira hoose pipe. Kumwagilia heka moja nitakuwa sawa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante kwa ushauri mkuu....umenifungua machoKwanza hongera kwa kuamua kuingia shambani, mimi nalima matikiti na nimeshajilipua kulima ktk kipindi hiki cha masika, kubwa zaidi tafuta mbegu bora kwenye maduka ya kilimo mfano pitia kariakoo, mimi nalima Hybrid F1 sugar queen, na kiwango cha ekari moja utatakiwa kuwa na gram 300 na kila shimo panda mbegu 2 japo wapo wanaopanda mpaka 3, na hapa utatakiwa kuwa na mshimo kama 2000.
Andaa shamba vizuri japo wiki tatu kabla ya kupanda na hakikisha eneo lako lina maji ya kutosha kwani tikiti linahitaji maji mengi katika uhai wake, Panda kwa mbolea, ni vema zaidi kama utapata samadi na kama utatumia ya viwandani zipo kama vile winner(hapa kuna kiambato chake, utamuuliza muuzaji), kwa kukuzia utatumia CAN, andaa dawa za wadudu wanaokata majani pindi matikiti yanapoanza kuota tu na pindi unapoona dalili za matikiti kushambuliwa majani (karate itakufaa).
Unahitaji uangalizi wa karibu sana kuanzia mwanzo mpaka mwisho na hakikisha unakuwa na dawa za kutosha kwa ajili ya kuzuia wadudu waharibifu, ukungu hasa kipindi hiki na magonjwa yanayoshambulia majani, maua na matunda.
Gharama kubwa utakayoingia kwenye kilimo hiki ni kwenye mbegu( ekari moja ni gram 300= 250,000 kwa Dar), dawa( hapa inategemea na hali ya eneo na jinsi magonjwa na wadudu wanavyoshambulia), nguvu zako mwenyewe kwenye kumwagilia( hapa kama unatumia ndoo, ila kama unatumia mashine ya kuvutia maji basi utahitaji wastani wa lita 5 kwa ekari moja kila unapomwagilia) na kutunza shamba, kama unatumia kijana basi hapo ni makubaliano yenu, bomba la kupigia dawa ni muhimu sana.
Mavuno ni kuanzia siku 65 mpaka 75 inategemea na eneo lenyewe na aina ya mbegu, na kiasi cha mavuno kwa ekari moja ni kiasi cha matikiti kama 7000( kila mche mmoja utoe matikiti 2 tu yenye afya nzuri) na soko likiwa nuri basi utauza kwa wastani wa Tsh 1500 au zaidi shambani, na ukiMU kwenda mwenyewe sokoni mfano Buguruni unaweza kuuza bei nzuri kama ni kipindi mmea huo haupatikani.
Ushauri: usiende shambani na matarajio makubwa zaidi ya kupata hela nyingi ukasahau changamoto zake( mavuno kidogo, hasara na muda), shambani kunahitaji uangalizi wa karibu sana na usijaribu kulima kwa simu hasa kama una watu wasio waaminifu watakuua kwa ugonjwa wa moyo. Pia hizo faida zinazopatiakana ni pale tu utakapo fata ushauri wa kitaalamu na ukaamua kwa dhati kufanya kilimo. Nimejaribu kueleza kile ninachofahamu japo sio kwa utaalamu zaid, mengine wajuzi watakuja kujazia.
Karibu sana shambani
Nipo Magu, MWANZA.Upo Dar es saalam mkuu?
ndugu kilimo kinaitaji timing na kufuata taratibu zake zote, pia kua makini na madalali hawa wanaletaga presha zisizo na msingi, hawajui ugumu wa kazi ulivyo na gharama zake wao wanachojua ni kupiga faida tu kuijanjaujanja.nimeshauza mkuu ila nilipata hasara.
Chukua muda kuipitia thread yote hii kuna watu waliwahi kulima huko kigamboni wanweza kukusaidia humuWakuu, nani analima Matikiti maji huku kigamboni, nahitaji kupata connection.. Ikibidi nianze mwezi wa tano.
Ulikuja nazo? nazitafuta sana hizo mbeguWakubwa mimi nina swali moja, jee mbegu kutoka north america zinaweza kumea vizuri hapa nyumbani?
Na hz mvua? Sio hatari kwel? Au kuna mbegu znahimili mvua kubwa hiv? Naomba unijuze vizurnipo hapa mm nafanyia kibada mwasonga huku kigamboni
Mkuu mimi pia nataka kulima mwezi wa tano ila nimepata eneo dogo pale kibadaWakuu, nani analima Matikiti maji huku kigamboni, nahitaji kupata connection.. Ikibidi nianze mwezi wa tano.