Kilimo cha mbogamboga: Kwa hii business plan nitatokaje?

OIL CHAFU

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2012
Posts
996
Reaction score
773
Iko hivi,

Nataka nijiingize katika kilimo cha mboga mboga especially nyanya, pilipili hoho, vitunguu na bilinganya.
shamba iko ekari 10 tayari,na nimefanya survey tayari.

Eneo lilipo hilo shamba hakuna mto japo utafiti unaonyesha kuwa eneo hilo maji yako karibu sana nikiamua kuchimba kisima. Nikafikiri kuwa nikiweza kuchimba kisima, alafu nikapata maji ya uhakika, niweke pampu itakayopandisha maji kutoka kisimani kwenda kwenye tanki, alafu nimwagilie kwa mpira kutoka kwenye tank, naweza kutengeneza hela ndefu.

Nilifanya mahesabu nikagundua kuwa kwenye shamba la urefu mita 70 na upana mita 70, (ekari moja) naweza kupanda miche 19,600 ya pilipili hoho, na kila mche nikiupa mahesabu ya chini kabisa unizalie matunda 10, nitakuwa na matunda 196,000. Nikienda sokoni kwa bei ya chini ya kila tunda Tsh 100, ntakuwa na kipato cha 19,600,000 Tshs.

Sasa nikiamua kuweka ekari mbili nyanya, mbili hoho, mbili vitunguu na mbili bilinganya na zingine mbili nitaamua niweke nini. Na uzingatie kuwa vitu hivi matokeo yake ni miezi mitatu hadi minne tuu, hizo hela ninazo. Pia nitajenga mabanda ya kutosheleza kufuga kuku 1,000 ili mbolea yao iwe inaenda shambani kila wiki. Hapo nitakuwa nimeua ndege wawili kwa jiwe moja.

Tatizo langu hivi nitapata wapi mtaji wa kuchimba kisima na pampu? Hela ya kuweka simtank, ulimaji na, ununuzi wa mbolea na dawa na usimamizi kwa ujumla sitashindwa kabisa, iko ndani ya uwezo wangu.

Naomba wenye mawazo ya kunishauri wafanye hivyo ili nami nitoke kimaisha. I want to do away with this orthodox tradition ya huku vijijini watu kila kukicha wanalima mahindi na maharage na hawana uhakika wa kuvuna.

Eee Mungu sikia kilio changu.
 
Siwezi kumsemea, lakini nikisoma katikati ya mistari sioni kama alifikia lengo hata Kwa asilimia 20.
 
Anza na ulichonacho,usiwaze usichokuwa nacho bado ni mapema sana.Hayo ni Mawazo Anza Tuone kwanza pesa zipo utapata baadaye
 
Mrejesho mkuu, tupate walau motivation. Ndoto ilikuwa kubwa sana
 
Kilimo kwakweli ni kama biko au mkeka beti.

Sisi tulilima bamia kama nusu heka hivi lakini soko hakuna mazao yamejaa yanatoka mkoani ndoo ndogo ya lita kumi inauzwa 2000!!
 
Kilimo kwakweli ni kama biko au mkeka beti.
Sisi tulilima bamia kama nusu heka hivi lakini soko hakuna mazao yamejaa yanatoka mkoani ndoo ndogo ya lita kumi inauzwa 2000!!!!
Soko la wapi mzee ?
Au ulikamatwa na madalali

Currently kisado cha bamia kinacheza 3000-4000
 
Kwanza nikuongezee wazo kdg hapo ukilima nyanya au hoho au bilinganya au zao lolote la mda mrefu usipande miche mingi kama unavyowaza km plan ni miche 19600 bas panda 4000 mwezi huu,4000 mwezi ujao,5000 mwezi unaofuata itakusaidia sana mbele kwenye mambo ya masoko...na kwenye kila mpango wa kilimo usisahau mazao ya mda mfupi kama figili, mchicha, matembele, sababu ndo yanakupa pesa ndogondogo za kuendesha mazao ya mda mrefu.
 
Nimependa plan zako ili kwenye kila biadhara hasa za kilimo target yako isiwe kulima miche mingi bali kuhudumia vzr shamba..kila la heri i hope utafanikiwa..

mie kiukweli nina uzoefu na kilimo !kwa Tanzania yetu hii unaweza hudumia shamba lako vizurii lkikawa kama shamba darasa pia !nenda sasa sokoni ukutane na bei za ajabu ajabu !yaan madalal siwapend jaman !mxiew
 
Hello idea yako iko vizuri please unaweza kunicheki whatsapp kupitia 0758962301 au unisaidie mawasiliano yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…