Iko hivi,
Nataka nijiingize katika kilimo cha mboga mboga especially nyanya, pilipili hoho, vitunguu na bilinganya.
shamba iko ekari 10 tayari,na nimefanya survey tayari.
Eneo lilipo hilo shamba hakuna mto japo utafiti unaonyesha kuwa eneo hilo maji yako karibu sana nikiamua kuchimba kisima. Nikafikiri kuwa nikiweza kuchimba kisima, alafu nikapata maji ya uhakika, niweke pampu itakayopandisha maji kutoka kisimani kwenda kwenye tanki, alafu nimwagilie kwa mpira kutoka kwenye tank, naweza kutengeneza hela ndefu.
Nilifanya mahesabu nikagundua kuwa kwenye shamba la urefu mita 70 na upana mita 70, (ekari moja) naweza kupanda miche 19,600 ya pilipili hoho, na kila mche nikiupa mahesabu ya chini kabisa unizalie matunda 10, nitakuwa na matunda 196,000. Nikienda sokoni kwa bei ya chini ya kila tunda Tsh 100, ntakuwa na kipato cha 19,600,000 Tshs.
Sasa nikiamua kuweka ekari mbili nyanya, mbili hoho, mbili vitunguu na mbili bilinganya na zingine mbili nitaamua niweke nini. Na uzingatie kuwa vitu hivi matokeo yake ni miezi mitatu hadi minne tuu, hizo hela ninazo. Pia nitajenga mabanda ya kutosheleza kufuga kuku 1,000 ili mbolea yao iwe inaenda shambani kila wiki. Hapo nitakuwa nimeua ndege wawili kwa jiwe moja.
Tatizo langu hivi nitapata wapi mtaji wa kuchimba kisima na pampu? Hela ya kuweka simtank, ulimaji na, ununuzi wa mbolea na dawa na usimamizi kwa ujumla sitashindwa kabisa, iko ndani ya uwezo wangu.
Naomba wenye mawazo ya kunishauri wafanye hivyo ili nami nitoke kimaisha. I want to do away with this orthodox tradition ya huku vijijini watu kila kukicha wanalima mahindi na maharage na hawana uhakika wa kuvuna.
Eee Mungu sikia kilio changu.