Kilimo cha mbogamboga

Kilimo cha mbogamboga

mvita

Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
11
Reaction score
0
Nahitaji kufanya kilimo cha mbogamboga na ardhi ya kwetu ni mawe ila natarajia kueka udongo juu.

Naombeni ushauri, itawezekana?
 
Kwanini isiwezakane kama utaweka udongo juu ?, Watu wanalima mboga mpaka magorofani, kuweka udongo juu itatosha mboga nyingi hazina mizizi mirefu, cha kufanya tengeneza raised beds kama eneo lako ni dogo this is the way to go:-

kwa maelezo zaidi soma hapa How To Make a Raised Bed Garden

na mfano wa picha;
th
th

kwahio mkuu hata gorofani au kwenye mifuko au mapipa ukiyakata nusu unaweza ukalima mboga
 
Afathali nimepata njia ya kulima katikati ya mji ambako hakuna mashamba
 
Unaweza pia ukatumia mifuko kama ya cement unaiweka miwili mmoja ndani ya mwingine,unaweka udongo ukiweza kupata na mbolea ya kuku ni nzuri then unaitoboa mifuko kwa pembeni unapanda mboga zako,
Afathali nimepata njia ya kulima katikati ya mji ambako hakuna mashamba
 
Kwanini isiwezakane kama utaweka udongo juu ?, Watu wanalima mboga mpaka magorofani, kuweka udongo juu itatosha mboga nyingi hazina mizizi mirefu, cha kufanya tengeneza raised beds kama eneo lako ni dogo this is the way to go:-

kwa maelezo zaidi soma hapa How To Make a Raised Bed Garden

na mfano wa picha;
th
th

kwahio mkuu hata gorofani au kwenye mifuko au mapipa ukiyakata nusu unaweza ukalima mboga

kabisa ndugu..enzi nikiwa nimepanga nilijaza gunia udongo na kulitoboatoboa kwa pembeni kama matundu 15 pamoja na juu..nikasia mbegu zangu za mnafu kwenye beseni..zilivyochipua nikazihamishia kwenye gunia zingine zikabaki kwenye beseni nikaweka pembeni ya mlango wangu..wakati wengine wameweka ndoo.za.maua mimi maua yangu yalikua mnafu..ulistawi na ukachipua kwa wingi na nilikula sana mboga ndugu..hata ukiwa ghorofani mboga unakula tu..
 
Unaweza kukuza mboga kwa kutumia mfumo unaoitwa aquaponics.

Mfumo huu unakuwezesha kukuza mboga kwenye kokoto. Kwa sababu umesema ardhi yako ni ya mawe, basi unaweza kutengeneza kokoto kwa ajili ya kukuzia mboga.

Mfumo huu unahusisha uzungushaji ukuzaji wa mboga na ufugaji wa samaki kwa pamoja. Maji huzungushwa toka ma-tanki ya kufugia samaki na kupelekwa kwenye bustani za kukuzia mboga. Bustani hizo za kukuzia mboga ni babeseni makubwa yaliyojazwa kokoto ambapo maji toka kwenye ma-tanki ya samaki huchujwa na hivyo kukuza mboga zilizooteshwa kwenye kokoto hizo.

Mfumo huu unahitaji mtaji mkubwa wa kuanzia, ila ukiweza, mavuno yake ni makubwa na ni ya kudumu.
Unaweza kupata maelezo zaidi ya mfumo huu wa aquaponics kwenye internet. Google neno 'aquaponics' halafu angalia maelezo na video zinazoonyesha jinsi mfumo huu unavyofanya kazi.

Aquaponics inavyofanya kazi (Mchoro toka internet)
simple+setup03.png

Mboga zilizooteshwa kwenye kokoto (kwenye mfumo wa aquaponics)
pif_aquaponics_CIN.jpg
[/quote]
 
Asante ila unaweza kunisaidia makisio ya kutengeneza miundo mbinu hiyo?
 
Kwakweli mimi nilijuwa hizo beds sana zinatengenezwa nchi za maulaya kumbe hatakwetu inawezekana ,nasema asante ameline kwa kunifumbua akili, nitaandaa na ninaimani nitafanikiwa na nitakukaribishenizanzibar (kazimkazi) kuja nitembelea.
 
Zanzibar kijijicha kizimkazi, huku hata ukijenga huchimbi msingi unaeka mawe vizuri tu unaendelea kujenda ni miamba mitupu.
 
kabisa ndugu..enzi nikiwa nimepanga nilijaza gunia udongo na kulitoboatoboa kwa pembeni kama matundu 15 pamoja na juu..nikasia mbegu zangu za mnafu kwenye beseni..zilivyochipua nikazihamishia kwenye gunia zingine zikabaki kwenye beseni nikaweka pembeni ya mlango wangu..wakati wengine wameweka ndoo.za.maua mimi maua yangu yalikua mnafu..ulistawi na ukachipua kwa wingi na nilikula sana mboga ndugu..hata ukiwa ghorofani mboga unakula tu..

Mkuu nina mpango wa kufanya hivyo, na nimekuwa nikiwazia hii kitu sana ila nilikuwa sijui miche nitaipandia wapi, ibu ninalo
 
Back
Top Bottom