Kilimo cha Mdalasini

Kilimo cha Mdalasini

Family_hammer

Member
Joined
Jan 2, 2016
Posts
29
Reaction score
11

Kitu ambacho kinafanya Mdalasin kuwa tofauti na mimea mingine zaidi ya kuwa kiungo bora pia utoa mafuta kutoka kwenye mizizi, gamba na majani, ambayo yana kemikali zinazotofautiana.

HALI YA HEWA NA UDONGO

Ubora wa Mdalasini utegemea udongo wenye rutuba na hali ya hewa nzuri.

  • Mvua nyingi za kutosha 1,750-3,500 mm kwa mwaka.
  • Udongo wenye rutuba na usioruhusu maji kutuama
  • Joto kwa wingi
  • Hewa yenye unyevunyevu

KUSIA MBEGU KWENYE VITALU

  • Mbegu hupatikana kwenye miti iliyokomaa
  • Sia mbegu kwenye kitalu zikiwa nusu sentimeta chini ya udongo
  • Baada ya kuchipua, mbegu huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kufikia umri wa kupandikiza shambani
  • Panda miche wakati wa masika
  • Panda kwa nafasi ya 2m x2m. Nafasi hizi huwezesha miti kutoa machipukizi mengi. Nafasi kubwa hufanya miti kuwa na matawi mengi pia mashina hayanenepi wala kurefuka.


UTUNZAJI

  • Acha machipukizi kwenye shina
  • Toa matawi kwenye mashina ili kunenepesha mashina
  • Weka shamba katika hali ya safi
  • Zuia magonjwa kama.Vinundu (galls)wanaosababishwa na utitiri na wadudu scales na mealbugs kwa kutumia dawa za sumu kama Selecron, Karate nk.

KUVUNA

Mdalasini uanzwa kuvunwa baada ya miaka mitatu toka upandwe na uvunwa mara mbili kwa mwaka.

  • Mazao ya mdalasini ni maganda ya mashina ya miti
  • Kata shina la mti,na tenganisha maganda na mti kwa njia ya kumenya
  • Kuwa mwangalifu ili ganda litoke vizuri bila kupasukapasuka
  • Seli za nje ya ganda la mdalasini ni chungu hivyo ni vizuri ziondolewe kwa kukaruza kwa kisu
  • Kausha vizuri siyo kwenye jua kali Mavuno
  • 0.25 kg – 10kg maganda yaliyokaushwa kwa mti mmoja. Kiasi cha mazao hutegemea ukubwa na umri wa mti
  • Ubora wa mdalasini hushuka kulingana na umri wa mti. Mti wa umri mkubwa hutoa mganda yenye ubora wa chini.

MATUMIZI
Mdalasini baada ya kukaushwa ikiwa umesagwa au bila kusagwa hutumika kama:

  • Kiungo kwenye chakula na vitafunwa kama keki, mandazi,vitumbua
  • Vikolezo kwenye vinjwaji km. chai, kahawa
  • Dawa ya tumbo hasa wakati wa kuvimbiwa, kutoa hewa tumboni pia kuongeza hamu ya chakula
  • Dawa ya ngozi
  • Husaidia kutibu UTI
  • Majani ya mdalasini uongeza radha kwenye chai.

Kwa mahitaji ya miche ya mdalasini tuwasiliane kwa namba 0713629999, Bei ya mche ni shilingi 5000 tu.




 
Back
Top Bottom