Kilimo cha Mihogo (Cassava): Mbinu, Ushauri, Changamoto na Masoko yake

Habari za majukumu wadau wa Jf. Nahitaj mwenye mawazo au mwenye kuelewa anishauri. Nahitaji kulima mihogo kwajir ya biashara lakin nahitaji ushaur wa aina gani ya mhogo wenye soko kwa sasa. Pia masoko yake yapoje kwasasa. Bila kusahau changamoto zake.kilimo nafanya mkoa wa Tanga. Naomba kuwasilisha.
 
Kuna wanaolima au wanaoweza kuni link na wakulima wa miogo Iringa waniunganishe niwape dili zuri.
 
Wakuu ni mbegu gani kwa sasa inatamba sokoni ambayo muhogo wake bei iko juu kuliko mingine?

Pia napenda kujua kwa anaye ijua hii mbegu inaitwa MKURANGA ONE ina sifa gani?
 
Njoo bagamoyo kuna aridhi nzuri ya MUHOGO,NANASI,MAHINDI NA MIFUGO PIA KAMA MBUZI KUKU. Patakufaa tu.kwa hapa fukayosi kwa sasa bei ya shamba iko juu heka 1 ni 2 Million. Ila kwa kiwangwa heka ni laki 7 tu. Maongezi wanakubali pia. Mm majuzi nimechukua pale fukayosi heka zng mbili tu.kwajili ya project zangu kama hz.


 
Naomba nisaidie mawasiliano yako mkuu.
 
Bei ya muhogo kwenyo soko ipoje?
Nasubiri jibu nami nataka kulima, huku Mtwara nilisikia tenga moja linauzwa kwa Tsh. 20,000/- hadi 30,000/-. Nitafanya utafiti zaidi ili nipate bei halisi.
 
Wakuu nimevutiwa sana na kilimo cha mihogo naomba mwenye uzoefu anisaidie tafadhali ni wakati gani namaanisha maimu hasa hupandwa na pia mbegu bora na changamoto zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…