Kilimo cha miti hakina faida kwa sasa. Ni biashara kichaa!

Kilimo cha miti hakina faida kwa sasa. Ni biashara kichaa!

Bei ya miti hasa aina ya"Pine" imeporomoka mno mashambani, japo bei za mbao mijini hazijashuka. Huwezi amini ekari moja ya miti(Iliyostawi vizuri) ya miaka 10 ni kati ya mil.1.2 hadi 1.5. Siku za nyuma ekari moja ingeweza kuuzwa mil.5. au zaidi.
Visingizio vya wafanyabiashara ni kupanda kwa gharama za usafilishaji na miti kuwa mingi.

Ieleweke kuwa Miti ina gharama nyingi kuanzia ununuzi wa shamba,kusafisha shamba , kuandaa mashimo,ununuzi wa miche,gharama ya upandaji,na kusafisha miti hasa miaka 5 ya mwanzo. Hapo hapo kuna hatari (Risk) ya moto " Wild fire". Mfano msimu huu wa 2021baadhi ya maeneo ya Kilolo na Mufindi zaidi ekari 1000 zimeungua kwa moto.

Wale wazee wa kuaminishwa na "motivational speakers" kwamba miti ni utajiri tambueni kwa sasa kilimo cha miti ni umaskini tena wa mda mrefu. Fikiria unasubiri kwa miaka zaidi ya 10 aaafu unaambulia kijihela ambacho ni mshahara wa mtu wa mwezi mmoja. This is insane!
Hamia kwenye parachichi
 
Hatari kabisa,nikisikia hizi taarifa huwa napata huzuni sana,sasa tuwekeze wapi?tuuze bangi!!??
Mi nawaza tu,binti yangu wa miaka 12,atafanya kazi gani miaka 20 ijayo!!
Kazi itapatikana tu.Mungu Mwenyezi aliyemuumba na kisha kumruhusu aishi atamsaidia.
 
Ila mimi siachi ndio kwanza naongeza 15 hectares somewhere daah huu msoto viva Maisha 2030+. Kuchekwa kawaida
By that time miti itakuwa imeshavunwa sana na wengi watakuwa walishakata tamaa ya kupanda huku mahitaji yakiwa makubwa sana,kwa hiyo itakuwa full kupeta.
 
Hatari kabisa,nikisikia hizi taarifa huwa napata huzuni sana,sasa tuwekeze wapi?tuuze bangi!!??
Mi nawaza tu,binti yangu wa miaka 12,atafanya kazi gani miaka 20 ijayo!!
muwekekeze kwenye tehama hukk ndo kutakuwa na kazi kubwa kwa baadae
 
Bei ya miti hasa aina ya"Pine" imeporomoka mno mashambani, japo bei za mbao mijini hazijashuka. Huwezi amini ekari moja ya miti(Iliyostawi vizuri) ya miaka 10 ni kati ya mil.1.2 hadi 1.5. Siku za nyuma ekari moja ingeweza kuuzwa mil.5. au zaidi.
Visingizio vya wafanyabiashara ni kupanda kwa gharama za usafilishaji na miti kuwa mingi.

Ieleweke kuwa Miti ina gharama nyingi kuanzia ununuzi wa shamba,kusafisha shamba , kuandaa mashimo,ununuzi wa miche,gharama ya upandaji,na kusafisha miti hasa miaka 5 ya mwanzo. Hapo hapo kuna hatari (Risk) ya moto " Wild fire". Mfano msimu huu wa 2021baadhi ya maeneo ya Kilolo na Mufindi zaidi ekari 1000 zimeungua kwa moto.

Wale wazee wa kuaminishwa na "motivational speakers" kwamba miti ni utajiri tambueni kwa sasa kilimo cha miti ni umaskini tena wa mda mrefu. Fikiria unasubiri kwa miaka zaidi ya 10 aaafu unaambulia kijihela ambacho ni mshahara wa mtu wa mwezi mmoja. This is insane!
Vipi kuhusu palachichi,nasikiaga huko watu wanasifia kwamba ni better kuliko miti
 
Hatari kabisa,nikisikia hizi taarifa huwa napata huzuni sana,sasa tuwekeze wapi?tuuze bangi?

Mi nawaza tu,binti yangu wa miaka 12,atafanya kazi gani miaka 20 ijayo!!
Awe programmer au finance guru
 
Miaka 20 ijayo miti/mbao/ nguzo za miti zitakua hazina soko sababu teknolojia inakwenda kasi sana. Mfano sasahivi kuna plastic bar ambazo hutumika kama m badala wa mbao. Tanesco wenyewe wanaachana na nguzo, square pipes na round zinatumika badala ya papi

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
Mbao zina matumizi mengi sana boss, furnitures na ujenzi wa nyumba mbao ni lazima
 
Pine, parachichi, tikitimaji yote hiyo ni biashara kichaa.
Huku kwenye starehe zetu tunahangaika sana maana kitimoto na mbuzi havipatikani na vimekuwa bei mbaya sana, jaribu hapo tunahangaika sana , kina Mangi wamekuwa greed wanataka faida yote itoke kwenye supu na michemsho
 
Nehemia One Pvt Co Ltd ni kampuni Inayo zalisha na kuuza miche ya mdalasini Kwa wawekezaji Kwa sh. 2600 Kwa mche.
Kampuni imeamua kuwaonesha fursa wawekezaji wa kitanzania kutokana na soko lake kukua Kwa kasi mno
Kwa mujibu wa taaasisi ya utafiti ya persistence market research, soko la MDALASINI litafikia Dola za kimarekani bilioni 1.15 mwaka 2030.

Uhitaji kwenye soko la kimataifa linatokana na matumizi makubw a kwenye viwanda vya dawa, vipodozi na viungo vya chakula.

UZALISHAJI

Ekari moja hupandwa miche Kati ya 380 Hadi 400 kitaalamu.
Miti hii inapenda udongo wa tifutifu au kichanga~tifutifu wenye maji wastani na mvua wastani kwenye joto la wastani wa digrii za sentigredi 27 na katika muinuko wa Mita 10 Hadi 1300 kutoka usawa wa bahari

Mdalasini halihitaji mbolea wala dawa hasa kwenye nchi za kitropiki kama Tanzania. Rutuba asili pekee hutosha kuzalisha.
Miti hii haistawi kwenye maeneo yanayotuamisha maji Kwa mda mrefu katika mwaka.

Mikoa inayofaa kuzalisha ni Morogoro, pwani, tanga, rukwa, ruvuma, mbeya, kigoma, Kagera, maeneo ya kuzunguka ziwa Viktoria, na Zanzibar. Baadhi ya mikoa Kati ya iliyotajwa ndio wameamua kuwekeza huko.

MASOKO YA NDANI NA NJE
Kampuni ya Nehemia One Pvt Co Ltd inamuunganiko na wafanyabiashara zaidi ya 300 wa viungo katika MASOKO ya vyakula yaliyo katika majiji na baadhi ya mini ya tanzania. Pia kampuni Ina muunganiko na makampuni ya kitanzania zaidi ya 80 ambayo hutafuta magome ya mdalasini ili kupeleka MASOKO ya nje ya Tanzania.

Kuna makampuni yanakuja Tanzania kupitia TANTRADE kuanzisha viwanda vya kuchakata mdalasini na viungo vingine Ila wanakwamishwa na upatikanaji mdogo wa mdalasini

Makampuni kama Csi kutoka nchi za falme za kiarabu yametangaza kununua mdalasini lakini hawapati kiwango kinachohitajika.

Mdalasini unaolimwa Tanzania unakidhi asilimia 20 Hadi 28 ya soko la ndani pekee hivo kufanya asilimia kubwa kuagizwa kutoka nchi za bara la Asia ka.a Vietnam., Malysia, India na China.

Bei ya wanunuzi wa ndani Kwa kilo ya magome ya mdalasini ni Tshs 8500 Kwa kilo na wanunuzi wa nje ni 9500 Hadi 10000 Kwa kilo na bei hizi zinatarajiwa kupanda saana ifikapo 2030. Bei tajwa ni zilizopo sokoni tangu 2018 mpaka 2022 kutokana na namna ambavyo kampuni yetu unafanya mauzo

UVUNAJI NA MAPATO.
Mdalasini unaweza kuvunwa kuanzia miaka mitatu tangu kupanda na inakawaida ya kuchipua baada ya kuvunwa hivyo uvunaji wake ni wa mwendelezo kila baada ya miaka mitatu Hadi itakapofikisha umri wa Kati ya miaka 35 na 40.

Jinsi mdalasini unavyozidi kuishi shambani, ndivyo thamani yake hupanda kutokana na uwingi wa magome yatakayo zalishwa, ladha na ubora wa harufu ya magome

Kama mdalasini ukiachwa kuanzia miaka 8 tangu kupanda MAVUNO Kwa mti ni wastani wa kilo za magome zisizo pungua 35.

Kwa ekari yenye miti 380 itatoa kilo 13300 (tani 13.3) ambazo zikiuzwa Kwa shilingi 8500 kila kilomoja zinazalisha kiasi cha shilingi milioni miamoja kumi na tatu na hamsini elfu (113,050,000) ambayo ni MAPATO ghafi.

Karibu uninue au kuiweka oda ya miche na utapewa muongozo wa namna ya kuzalisha shambani. Soko lake linasubiri wazalishaji.!

Piga au watssap +255699589177
+255762967548
Email: nehemiahedward7@gmail.com
Bei ya mche ni 2600

Ushauri. Waweza anza na miche michache sio lazima uwekeze ekari nyiingi kama uwezi wa kuwekeza ni mdogo.
 
Mi kwenye Kilimo ningepanda Mpunga na Maharage,Na nikipata kisehemu kidogo napanda Pilipili.
 
Back
Top Bottom