Kilimo cha miti Mufindi.

Kilimo cha miti Mufindi.

Mimi nadhani hujamtendea Malila haki kwa kumwambia kuwa anaropoka na kujidai anajua, ulipaswa ukanushe au utueleweshe wasomaji kuwa ukweli ni upi. BTW mkuu Malila ni mdau wa muda mrefu pia kny huo mradi na hata aliyosema kuhusu mapanda baadhi nayajua kwa hivyo usijibu kwa hamaki, tueleweshe tu mkuu

Asante kwa kuchangia,
Watz wenzangu ni vizuri tukijenga tabia ya kusema ukweli hata kama unauma. Kwa kuwa na maelezo nusu nusu tunaumizana sana. Kama angekuwa na uhakika na anacho kisema angeweka hadharani kama mimi nilivyofanya, jf na hasa jukwaa la uchumi ni sehemu ya ukombozi, tusaidiane. Igeleke na Kibengu kuna ardhi ya hatari ndugu zangu. Niko ktk vijiji hivyo mwaka wa saba sasa. Igeleke manpower ni tatizo pia.

Tuokoe muda, kama una nia ya kuwasaidia wenzako wapande miti basi watafutie ardhi Kipanga, Lulanda,Ibwanzi na Ukami. Huko ardhi ipo na nzuri pamoja na manpower. Igeleke wanunue wenyeji kwa sababu za kiusalama.
 
Biashara zipo nyingi tu ambazo waweza fanya bila kupigwa lakini hizi za miti acha kuwaingiza watu mkenge, naongea ukweliambao nimeona kwa macho yangu labda uhamie huko huko....! nd yale yale ya wakulima wa Mbozi, mtu anakopesha fedha na pembejeo kwa wakulima halafu wakati wa mazao kuvunwa wakulima wanatakiwa kulipa ile mikopo cha ajabu na kushangaza wanamua yule mtu anayewadai na aliyewakopesha kwa nia nzuri tu. Tuwe makini wapendwa mavuno ya miaka 10 si mchezo!

Lakini hujataja hata biashara moja ambayo mtu anaweza kufanya bila kupata changamoto ktk dunia ya leo na hasa Tz yetu. Nitajie moja tu, usiseme ziko nyingi.
 
Lakini hujataja hata biashara moja ambayo mtu anaweza kufanya bila kupata changamoto ktk dunia ya leo na hasa Tz yetu. Nitajie moja tu, usiseme ziko nyingi.

ni majibu mepesi sana watu huwa wanatoa..kila biashara ina changamoto zake na kupigwa kupo!!
Kikubwa ni kutake calculated risk!!
 
Changamoto zipo katika biashara zote, na changamoto ni sehemu ya biashara. kuwekeza katika maeneo yasiyo hamishika ni vizuri na ni mawazo mazuri pia lakini kumbuka hayo mashamba unayosema ni ya koo au familia fulani ambapo wewe mwekezaji huingii mkataba na hao wote ila unaingia mkataba na baadhi ya watu katika koo hizo au familia hizo. Binadamu tuna tamaa sana na kutoheshimu makubaliano, nilishawai pelekwa huko kipindi fulani lakini nilipewa dondoo tu na baadhi ya watu ambao wanauzoefu na hii biashara, umakini ni kitu ambacho kinatakiwa sana katika huu uwekezaji.Bony Voyage
 
Kwa hiyo hoja yako ni ipi hapo, kutapeliwa ama miaka 10 ni mingi.

Yaonekana bado kuwa watu hawajitambui ama bado watoto wa shule humu.

Ina mana hujawahi kununua shamba ama kiwanja? Na je taratibu za kuuziwa mali isiyohamishika hauijui? Ama wataka tukupe elimu kwanza taratibu za kufuata katika ununuaji wa mali zisizohamishika?

Upande wa muda sio tatizo kwa mwekezaji mwenye muono wa mbali kama uwezo wako ni wa kuwekeza upate mia mbili baada ya siku mbili, ni juu yako. Ila kwa mwenye malengo ya badae msiwakatishe tamaa, wapeni moyo kama wana nia na sio lazima kupitia kwangu bali hata kama wewe wafahamu kuhusu kitu waweza mshauri pia ama ukampa direction ya uwekezaji bt, unapoponda na kuwatisha halafu huwapi mawazo wafanye nini mbadala unakuwa hujakamilika.

Tupo kwa ajili ya kubadilishana mawazo ya kimaendeleo sio kupondana wala kutishana ndugu.

NB: Unapotoa angalizo ama walakini wa jambo fulani jaribu kutoa na wazo mbadala ili mawazo yako yakamilike.
Futa kauli hiyo.
 
ukiuza miti ya nguzo kwa wanunuzi inakula kwako kwani wananunua kwa elf 30-35 wakati ukikata na kusafirisha mwenyewe hadi kwa merebu,sao hill au new forest, bei ni kunazi 85 kwa nguzo ndogo kabisa, laki 120,150, 200mpaka laki 250 kulingana na size ya unene wa nguzo, urefu na ilivyonyooka. sasa piga hesabu uja nguzo 100 za laki 250,000x 100 #25 ,000,000 je katika shamba la nguzo 1000 japo sio zote zitatoka nguzo tuseme inapata nguzo 940 una shilingi ngapi?
 
ukiuza miti ya nguzo kwa wanunuzi inakula kwako kwani wananunua kwa elf 30-35 wakati ukikata na kusafirisha mwenyewe hadi kwa merebu,sao hill au new forest, bei ni kunazi 85 kwa nguzo ndogo kabisa, laki 120,150, 200mpaka laki 250 kulingana na size ya unene wa nguzo, urefu na ilivyonyooka. sasa piga hesabu uja nguzo 100 za laki 250,000x 100 #25 ,000,000 je katika shamba la nguzo 1000 japo sio zote zitatoka nguzo tuseme inapata nguzo 940 una shilingi ngapi?
 
Asante kwa kuchangia,
Watz wenzangu ni vizuri tukijenga tabia ya kusema ukweli hata kama unauma. Kwa kuwa na maelezo nusu nusu tunaumizana sana. Kama angekuwa na uhakika na anacho kisema angeweka hadharani kama mimi nilivyofanya, jf na hasa jukwaa la uchumi ni sehemu ya ukombozi, tusaidiane. Igeleke na Kibengu kuna ardhi ya hatari ndugu zangu. Niko ktk vijiji hivyo mwaka wa saba sasa. Igeleke manpower ni tatizo pia.

Tuokoe muda, kama una nia ya kuwasaidia wenzako wapande miti basi watafutie ardhi Kipanga, Lulanda,Ibwanzi na Ukami. Huko ardhi ipo na nzuri pamoja na manpower. Igeleke wanunue wenyeji kwa sababu za kiusalama.

Asante mkuu kwa ufafanuzi mzuri, maana mradi bila usalama ni dalili mbaya, waweza poteza thamani ya rasilimali yako uliyoiwekeza bila kutaraji.
 
Kuna wataalamu wa hii biashara walisema Iringa maeneo yamejaa coz watu wengi maeneo/ mashamba ni ya watu kule sema hayajaendelezwa so kuwa mwangalifu unaweza kuwa umeuziwa eneo la mtu ukampandia

na utapeli wa ardhi siku hizi uko modern sana kwani matapeli wanaondoa trace na signs zote za kuonyesha kuwa eneo lile ni la mtu

kuweni waangalifu sana however hii biashara nataka kuifanya pia research yangu ndio baadhi ya majibu niliyokutana nayo
 
Back
Top Bottom